“Mei 25–31. Mosia 29–Alma 4: ‘Walikuwa Imara na Wasiohamishika,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Mei 25–31. Mosia 29–Alma 4,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020
Mei 25–31.
Mosia 29–Alma 4
“Walikuwa imara na wasiohamishika”
Katika enzi za Alma, mwalimu wa injili hakuwa anafikiriwa “ana ubora wowote kuliko mwanafunzi; na hivyo wote walikuwa sawa” (Alma 1:26). Unapojiandaa kufundisha, tafakari jinsi kanuni hii inavyotumika kwako na darasa lako.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Washiriki wa darasa wametambua milinganisho sambamba kati ya matukio yaliyoelezwa katika Mosia 29–Alma 4 na mambo ambayo yanatokea katika ulimwengu wa leo au maisha yao wenyewe. Wapatie dakika chache kuzirejea upya sura kupata mfano. Watake washiriki kile walichokipata na mtu fulani aliyeketi karibu nao.
Fundisha Mafundisho
Tunaweza kuwa na ushawishi chanya katika jumuiya zetu.
-
Kama washiriki wa darasa wangefanikiwa kutokana na majadiliano jinsi ya kushawishi jumuiya moja kwa moja, ungeweza kuwataka kufikiri juu ya mada ambazo jumuiya yako inakabiliana nazo na kuorodhesha chache ubaoni (epuka majadiliano ya kila kitu ya mada hizi). Washiriki wa darasa wangeweza kurejea upya Alma 2:1–7 kutafuta ni kitu gani Wanefi walikabiliana nacho na nini walifanya kukihusu. Nini kingeweza kutokea kama “watu wa kanisa” hawakufanya sauti zao zisikike? Kipi kingine tunajifunza kuhusu kuwa raia wema kutoka maelezo haya, kutoka Mosia 29:26–27, na kutoka hadithi katika “Nyenzo za Ziada”? Washiriki wa darasa wanaweza kutaka kufikiri juu ya kitu fulani watakachofanya kushawishi jumuiya zao moja kwa moja kuhusu mojawapo ya mada zilizopo ubaoni
Tunaweza kutambua na kukataa mafundisho ya uongo.
-
Mfano wa Gidioni kumpinga Nehori ungeweza kuvutia darasa lako. Labda ungeweza kumtaka mtu fulani kabla kurejea historia ya Gidioni na kuishiriki na darasa (ona Mosia 19:1–8.); 20:15–22; 22:1–9; Alma 1:2–9). Kwa msingi wa urejeo huu, washiriki wa darasa wangeweza kuorodhesha baadhi ya tabia za ushawishi za Gidioni. Kwa mfano, wakati Gidioni aliposikia mafundisho ya uongo ya Nehori, Gidioni alimpinga Nehori “na maneno ya Mungu” (mstari 9). Katika mafunzo yao binafsi, washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamepata maandiko ambayo yanakanusha mafundisho ya Nehori waliyoyapata katika Alma 1:3–6. Watake kushiriki maandiko waliyoyapata. Maandiko kadha pia yamependekezwa katika “Nyenzo za Ziada.” Tunawezaje kuwa zaidi kama Gidioni katika ulinzi wetu wa ukweli?
-
Mafundisho ya uongo ya Nehori katika Alma 1:3–6, yanaweza kutusaidia kugundua mbinu ambazo Shetani anazitumia kutudanganya. Kwa mfano, mara kwa mara anaficha uongo wake kwenye ukweli. Fikiria kuwataka washiriki wa darasa kupekua Alma 1:3–4 na kutambua uongo ambao shetani alimwambia na kweli alizozitumia kuufanya uvutie. Ni baadhi ya uongo upi uliochanganywa na ukweli ambao hudanganya watu leo? Tunawezaje kusaidia familia zetu na wapendwa wetu kutofautisha kati ya kweli na kosa?
-
Washiriki wa darasa wangeweza kuimba au kusoma wimbo kuhusu unyenyekevu, kama vile “Be Thou Humble” (Nyimbo, na. 130), na jadili jinsi ujumbe wake unavyotofautiana na ujumbe wa Nehori katika Alma 1:2–9. Wangeweza pia kutofautisha kile Nehori alichofundisha kuhusu walimu wa injili na kile Alma na viongozi wengine wa Kanisa walichofundisha na walichoonesha kwa mfano (ona Alma 1;26; 4:15–20). Nini ilikuwa sababu ya Nehori kufanya hivyo? Jinsi gani ilikuwa tofauti na ya Alma? Watie moyo washiriki wa darasa kutafakari motisha yao wenyewe ya kuhudumia katika Kanisa. Nini Alma 1:26 inapendekeze kuhusu wajibu wetu kama wanafunzi?
Kiburi kinaweza kutusababishi “tushindwe katika kuendelea [kwetu].”
-
Kujadili Alma 1 na Alma 4 kunaweza kusaidia washiriki wa darasa kuelewa jinsi kiburi kinaathiri vyote watu binafsi na Kanisa. Ungeweza kuligawa darasa katika makundi mawili na kulitaka kundi moja kujifunza kuhusu hali ya Kanisa kama ilivyoelezwa katika Alma 1:19–30, wakati kundi lingine linajifunza kuhusu hali ya Kanisa miaka michache badaaye, ilivyoelezwa katika Alma 4:6–15. Litake kila kundi kushiriki jinsi Kanisa na waumini wake walivyokuwa kulingana na mistari waliyosoma. Wanaweza kupanga pamoja njia bunifu kufanya hivi—kwa mfano, wangeweza kuchora picha au kutayarisha tamthilia fupi. Baada ya makundi kushiriki wao kwa wao, watake kujadili kile walichojifunza kuhusu athari za kiburi kwenye Kanisa na waumini wake na baraka za unyenyekevu. Ni masomo gani maelezo haya yanayo kwa ajili yetu leo”
“Neno la Mungu” na “ushuhuda safi” vinaweza kubadili mioyo.
-
Watu wengi wanaweza kuhusisha na jinsi Alma alivyohisi wakati alipokuwa “amehuzunika sana” (Alma 4:15) kuhusu uovu na mateso ya watu wake. Labda washiriki wa darasa wangeweza kufikiria kuhusu mpendwa wao ambaye wana wasiwasi naye na wanaye akilini mwao wanaposoma Alma 4:12–20. Baada ya washiriki wa darasa kusoma, unaweza kuuliza maswali kama haya kushawishi majadiliano ya mistari: Nini kilileta furaha kwa watu katika hali zao ngumu? Kishazi “Roho wa Bwana hakumwacha” kina maana gani kwako? (Alma 4:15). Ni dhabihu gani Alma alizifanya kusaidia watu wake, na dhabihu gani wakati mwingine tunatakiwa tuzifanye? Ni mifano gani tuliyoiona yenye nguvu ya “ushuhuda safi”? (Alma 4:19). Tunawezaje kushiriki shuhuda zetu bila kutoa muhadhara au kuwa wenye kuhukumu? Unaweza kuwapa washiriki wa darasa muda kuandika ujumbe wa ushuhuda kwa wapendwa wao.
-
Labda washiriki wa darasa wangenufaika kwa kujadili “ushuhuda safi” ni nini. Video “Apostle Testimony Montage” (ChurchofJesusChrist.org) ina baadhi ya mifano mizuri sana. Jinsi gani shuhuda hizi, au zingine tulizozisikia, “zinatukoroga [sisi] katika kutukumbusha juu ya kazi [yetu]”? (Alma 4:19). Jinsi gani shuhuda hizi zinatusaidia kushinda kiburi na mabishano?
Himiza Kujifunza Nyumbani
Ungeweza kuwalezea washiriki wa darasa kwamba katika Alma 5–7 watasoma “ushuhuda safi” wa Alma na kuona athari zake juu ya watu (ona Alma 4:19).
Nyenzo za Ziada
“Fanya ushawishi wako uonekane.”
Mara baada ya Dada Belle S. Spafford alipoitwa kama Rais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama mnamo mwaka 1945, viongozi wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama walialikwa kuhudhuria mkutano wa baraza la wanawake maarufu wa kimataifa. Viongozi wakuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama wamekuwa washiriki wa baraza hili kwa miaka mingi, lakini walihisi hivi karibuni wamekuwa wakitendewa vibaya na baraza hili. Baada ya majadiliano na washauri wake, Dada Spafford alipendekeza kwa Rais George Albert Smith, Rais wa Kanisa, kwamba Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama ukomeshe uanachama wake katika baraza hili.
Walipokuwa wanajadiliana mapendekezo, Dada Spafford alisema, “Unajua, Rais Smith, hatupati chochote kutoka kwenye baraza hili.
Baadae alisimulia:
“Rais alinitazama kwa mshangao. Alisema, ‘Dada Spafford, siku zote unafikiri kwa masharti ya nini unapata? Hufikirii ni vyema wakati mwingine kufikiri kwa masharti ya nini unatakiwa utoe? Ninaamini, ’aliendelea, ‘kwamba wanawake wa Kimormoni wana kitu fulani cha kutoa kwa wanawake wa ulimwengu, na kwamba wanaweza pia kujifunza kutoka kwao. Kuliko kukomesha ushiriki wenu, ninapendekeza kwamba wachukuwe baadhi ya washiriki wako wenye uwezo wa bodi na mrudi kwenye mkutano huu.’
“Kisha alisema kwa msisitizo, ‘Fanyeni ushawishi wetu uonekane’” (Belle S. Spafford, A Woman’s Reach [1974], 96–970.
Dada Spafford alitii ushauri huu. Alihudumu kwa miaka mingi katika baraza na hatimaye alichaguliwa kama mmoja wa viongozi wake.