Njoo, Unifuate
Mei 11–17. Mosia 18–24: “Tumeingia kwenye Agano na Yeye”


“Mei 11–17. Mosia 18–24: ‘Tumeingia kwenye Agano na Yeye,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Mei 11–17. Mosia 18–24,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Watu wa Limhi wanatoroka

Minerva K. K. Teichert (1888‑1976), Kutoroka kwa Mfalme Limhi na Watu Wake, 1949‑1951, mafuta juu ya ubao, 35 7/8 x 48 inchi. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, 1969

Mei 11–17

Mosia 18–24

Tumeingia kwenye Agano na Yeye

Unaposoma Mosiah 18–24, fikiria kuhusu watu unaowafundisha. Unajua nini kuhusu wao? Roho Mtakatifu anaweza kuvutia mawazo yako na kukusaidia kutambua kweli za injili ambazo zinaweza kuhusika kwao.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kupendekeza baadhi ya kanuni au kauli za kweli, ambazo walizipata wakati wa kujifunza kwao Mosia 18–24. (Baadhi ya kanuni zimeorodheshwa kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.) Watie moyo kushiriki mistari kutoka Mosia 18–24 ambayo inafundisha kanuni hizi. Ni uzoefu gani wameupata kwa kweli hizi?

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mosia 18:1–16

Ubatizo unajumuisha agano la kumtumikia Mungu na kusimama kama shahidi Wake.

  • Unaposoma Mosia 18 na kujiandaa kufundisha, unaweza kuhisi msukumo kuwasaidia washiriki wa darasa kurejea upya na kutafakari agano lao la ubatizo. Hii hapa ni njia moja ungeweza kufanya hivyo: Waalike washiriki wa darasa kufanya kazi pamoja kuorodhesha ubaoni vifungu vya maneno vingi kadri wanavyoweza kukumbuka vinavyohusiana na maelezo ya Alma ya agano la ubatizo. Wakati wanapomaliza, washiriki wa darasa wangeweza kusoma Mosia 18:8–10 na kuongeza chochote kwenye orodha ambacho pengine kimekosekana. (Wanaweza pia kuongeza vifungu vya maneno kutoka M&M 20:37, 77, na 79.) Inaweza kusaidia kuwauliza nini kila kifungu cha maneno kinamaanisha na nini wanaweza kufanya kutunza sehemu hiyo ya agano la ubatizo. Ni kwa jinsi gani Bwana anatubariki tunapojitahidi kutunza sehemu yetu ya agano?

  • Wakati wafuasi wa Alma walipojiandaa kubatizwa, Alma aliwafundisha kwamba kuja “katika zizi la Mungu” kulihitaji kufanya agano la kumfuata na kuwatunza watoto Wake (ona Mosia 18:8–9). Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wakati wao au mtu fulani wanayemjua aliimarishwa kwa mtu mwingine kutimiza agano la ubatizo lililoelezwa katika Mosia 18:8–10. Kwa mfano, ni lini mtu fulani amewafariji au kuwasaidia kubeba mizigo yao? Ni kwa jinsi gani uzoefu huu umetupatia msukumo wa kutunza agano letu? Ungeweza pia kuwakumbusha washiriki wa darasa kuhusu jinsi Abinadi alivyosimama “kama [shahidi] wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote” (Mstari wa 9). Tunaweza kujifunza nini kutokana na mfano wake tunapotafuta kutimiza sehemu hii ya agano letu la ubatizo?

ubatizo baharini

Tunapobatizwa, tunafanya agano la kumtumikia Mungu na wengine.

Mosia 18:17–31

Watu wa Mungu wana umoja.

  • Mosia 18:17–31 inaelezea amri Alma alizowapa watu wake kuwasaidia kuwa na umoja kama waumini wa Kanisa la Kristo. Kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiri kuhusu jinsi amri hizi zinavyotumika kwao, ungeweza kuwaomba kuchambua mistari hii katika makundi madogo na kutengeneza orodha ya amri wanazopata. Ni kwa jinsi gani kufuata amri hizi kungeweza kuwasaidia washiriki wa kata kuhisi wenye umoja zaidi? Je kuna malengo yoyote ambayo washiriki wa darasa lako wangeweza kuweka kibinafsi au kama kundi kufuata mfano wa watu wa Alma?

  • Baadhi ya Watu hujiuliza, kwa nini tunahitaji kanisa? Kuwasaidia washiriki wa darasa kujibu swali hili, ungeweza kuchora ramani ya jengo la Kanisa ubaoni na kuandika swali hili chini yake. Washiriki wa darasa kisha wangechunguza Mosia 18:17–31 na kuandika ubaoni majibu yanayowezekana wanayoyapata katika mistari hii. Wanaweza pia kupata majibu kwenye dondoo kutoka kwenye mazungumzo ya Mzee Christofferson katika “Nyenzo za Ziada.” pengine ungewaruhusu washiriki wachache wa darasa waigize jinsi watakavyomjibu rafiki ambaye haamini kwamba kanisa lenye utaratibu ni muhimu. Kwa nini tunashukuru kuwa Kanisani?

  • Wakati tungependa kufikiri kwamba kila mtu anahisi kukaribishwa kanisani, kwa bahati mbaya, sio kila mmoja anahisi hivyo. Tunajifunza nini kutoka kwa watu wa Alma katika Mosia 18:17–31 ambacho kinaweza kutusaidia kutengeneza mahali ambapo wote wanahisi kuwa wa mahali hapo?

Mosia 21–24

Bwana anaweza kufanya mizigo yetu miepesi.

  • Mizigo washiriki wa darasa lako wanayobeba ni tofauti na ile iliyobebwa na watu wa Limhi au watu wa Alma walipokuwa utumwani. Bali jumbe za matukio haya zinahusika kwa kila mmoja anayehisi kuzidiwa na shida au hali ya matatizo tofauti. Waalike washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza kutoka Mosia 21–24 kuhusu jinsi Mungu anavyoweza kutusaidia katikati ya majaribu yetu. (Kwa muhtasari wa maelezo haya, ona L. Tom Perry, “Nguvu ya Ukombozi,” Ensign au Liahona, Mei 2012, 94–97.) Washiriki wa darasa wangeweza pia kushiriki nyakati ambapo wao, kama watu wa Alma, walipata uzoefu wa utimizwaji wa ahadi ya Mungu kwamba Ataifanya mizigo yao kuwa miepesi na kuwatembelea katika mateso yao (ona Mosia 24:14).

  • Ingeweza kuwa yenye maana kwa washiriki wa darasa kutumia dakika chache kuandika changamoto binafsi walizokabiliana nazo na kutafakari jinsi Bwana anavyowasaidia kubeba mizigo yao. Je, kuna vifungu vya maneno kutoka Mosia 21–24 ambavyo vinawapa msukumo kumgeukia Bwana wakati wa shida? Ni kwa jinsi gani ahadi ya Bwana kwa watu wa Alma katika Mosia 24:14 ina uhusiano na agano tunalofanya kwa Bwana wakati wa ubatizo? (ona Mosia 18:8–10).

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwapa msukumo washiriki wa darasa kusoma Mosia 25–28, waombe kufikiria kuhusu mtu fulani wanayemjua ambaye amepotea kutoka kwenye injili. Waambie kwamba wanaposoma sura hizi, wangeweza kupata umaizi wa jinsi ya kumsaidia mtu huyo kurudi.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kwa nini tunahitaji Kanisa?

Mzee D. Todd Christofferson alisema: “Ninaelewa kwamba kuna baadhi ya watu ambao wanajifikiria ni washika dini au watu wa kiroho na hali wanakataa kushiriki kanisani au hata haja ya taasisi kama hiyo. Desturi ya kidini kwao ni ya binafsi hasa. Ilhali Kanisa ni uumbaji wa Yule ambaye ni kiini cha mambo yetu ya Kiroho—Yesu Kristo. Inastahili kutulia ili kufikiria kwa nini anachagua kutumia kanisa, Kanisa Lake, Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, kufanikisha kazi Yake na ya Baba Yake.”

Mzee Christofferson kisha alishiriki sababu za Bwana kuanzisha Kanisa (ona “Kwa nini Kanisa,” Ensign au Liahona, Nov. 2015, 108–11):

  • “Kuhubiri habari njema za injili ya Yesu Kristo na kusimamia ibada za wokovu—kwa maneno mengine, kuwaleta watu kwa Kristo.”

  • “Kujenga jumuiya ya Watakatifu ambayo itasaidiana katika ‘njia hii nyembamba iliyosonga ambayo inaelekea uzima wa milele’ [2 Nefi 31:18]. … Tukiungana katika imani, tunafundishana na kuadilishana na kujitahidi kufikia kipimo kamili cha ufuasi.”

  • “Kuwa na mkusanyiko wa kila wiki wa kupumzika na kurejea upya, muda na mahali pa kuweka kando ulimwengu—Sabato.”

  • “Kufanikisha vitu vinavyohitajika ambavyo haviwezi kufanikishwa na watu binafsi au makundi madogo [ikijumuisha] kushugulikia umaskini, … [kupeleka] injili ulimwenguni kote … [kujenga na kuendesha] mahekalu, nyumba za Bwana, ambamo ibada za muhimu na maagano yanaweza kufanyika.”

  • Kufanya zipatikane funguo za ukuhani, ambazo kwazo “maofisa wa ukuhani wa Kanisa wanahifadhi usafi wa mafundisho ya Mwokozi na uadilifu wa ibada Zake za kuokoa, … kusaidia kutayarisha wale wanaotaka kuzipokea, kuamua sifa na ustahili wa wale wanaoomba, na kisha kuzifanya … [na] kutambua vyote ukweli na uongo.”