Njoo, Unifuate
Mei 4–10. Mosia 11–17: “Nuru … Ambayo Haiwezi Kuwekwa Giza”


“Mei 4–10. Mosia 11–17: ‘Nuru … Ambayo Haiwezi Kuwekwa Giza,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Mei 4–10. Mosia 11–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Abinadi akishuhudia kwa Mfalme Nuhu

Abinadi Mbele ya Mfalme Nuhu, na Andrew Bosley

Mei 4–10.

Mosia 11–17

“Nuru … Ambayo Haiwezi Kuwekwa Giza”

Fikiria mfano wa Abinadi wa kufundisha injili. Je, unapata nini katika Mosia 11–17 ambacho kinaweza kukusaidia kuwa mwalimu bora?

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Kuwaruhusu washiriki wa darasa kushiriki kitu fulani walichojifunza katika mafunzo yao binafsi au ya kifamilia, ungeweza kuwataka kukamilisha sentensi ifuatayo: kama ningekuwa na mstari mmoja wa kuchagua kutoka Mosia 11–17 kushiriki na mpendwa wangu, utakuwa ni .

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mosia 11–1317

Tunaweza kusimama kwa ajili ya ukweli, hata wakati tunaposimama peke yetu.

  • Ingawa hamna uwezekano kwamba washiriki wa darasa lako watatishwa na kifo kwa ajili ya ushuhuda wao, wanaweza kukabiliana na upinzani kwa ajili ya imani zao. Labda wangeweza kupata matukio au vifungu katika Mosia 11–13 na 17 ambavyo vinawapa ujasiri wa kusimama kwa ajili ya ukweli. Nini kiliwapa Abinadi na Alma ujasiri wa kuwa wakakamavu? Tunawezaje kuwa imara zaidi na thabiti katika kulinda ukweli? Dondoo katika “Nyenzo za Ziada” zinaweza kutoa baadhi ya mawazo.

  • Kusaidia darasa lako kujifunza kutoka mifano mingine ya kulinda ukweli kwa ujasiri, ungeweza kuandika Watu Waliosimama Imara Kwa Ajili ya Ukweli ubaoni. Unaweza kuanza na kumjadili Abinadi ukiwataka washiriki wa darasa kushiriki baadhi ya vitu ambavyo vinawavutia kuhusu Abinadi wanaposoma kumhusu yeye wiki hii. Kisha wangeweza kutaja watu wengine wanaume na wanawake—kutoka kwenye maandiko, familia zao, au uzoefu binafsi—ambao wanahisi ni mifano ya kusimama imara kwa ajili ya ukweli. Tunahisi vipi kuvutiwa kufanya kwa sababu ya mifano hii?

Mosia 12:19–37

Tunapojifunza neno la Mungu, tunahitaji kutumia mioyo yetu kuelewa.

  • Wakati walipojifunza Mosia 12:18–37 wiki hii, washiriki wa darasa wanaweza kuwa walipata umaizi kuhusu inamaanisha nini kutumia mioyo yetu kuelewa neno la Mungu. Fikiria kuwataka wachache wao kushiriki mawazo yao. Au Labda ungeweza kutumia baadhi ya muda darasani kuchambua mistari hii pamoja na kujadili kile walichopendekeza kuhusu jinsi ya kufanya mafunzo ya injili yawe ya maana zaidi. Kwa mfano, kwa nini ni muhimu kuelewa vyote sheria ya Mungu na “kuitii”? (Mosia 12:29).

  • Ni nini washiriki wa darasa lako wanaweza kujifunza kwa kutofautisha fikra na utekelezaji wa makuhani wa Nuhu na mtizamo tunaopaswa kuchukua kwenye mafunzo yetu wa injili? Watake kusoma Mosia 12:19–37, wakitafuta ukosoaji ambao Abinadi aliupaza kuhusu makuhani wa Nuhu. Nini Abinadi angesema kuhusu mafunzo yetu ya injili leo? Watake washiriki wa darasa kushiriki kile wanachofanya ambacho kinawasaidia kutumia mioyo yao kuelewa na kuongeza maana kubwa kwenye kujifunza injili kwao.

    Picha
    Baba na mwana wakisoma maandiko

    Mafunzo ya injili ya kufaa yanahusisha kutumia mioyo yetu ili kuelewa.

Mosia 13:28–15:11

Wokovu unakuja kupitia kwa Yesu Kristo na Upatanisho Wake.

  • Kuthibitishia hadhara ya wenye kushuku kuhusu ujio wa Masiya, Abinadi alinukuu utabiri wa kusisimua kutoka Isaya (ona Mosia 14). Kuna njia kadha washiriki wa darasa wanaweza kurejea upya sura hii. Wanaweza kusoma mistari michache na kuijadili, au ungeweza kugawa darasa katika makundi madogo ya majadiliano kuzungumza kuhusu mistari yenye maana, pamoja na tanbihi, kugundua utambuzi wa ziada. Wahimize kushiriki kile wanachojifunza kuhusu Mwokozi kutoka sura hii.

  • Je, washiriki wa darasa lako wanaelewa inamaanisha nini kwamba Yesu Kristo “alitosheleza matakwa ya haki”? Mosia 15:9. Kuwasaidia kupata uelewa mzuri zaidi, unaweza kuanza kwa kusoma pamoja “Justice” na “Merciful, Mercy” katika mwongozo kwa maandiko (Scripture.ChurchofJesusChrist.org) au “Justice”na ”Mercy” kwenye topic.ChurchofJesusChrist.org. Labda mtu fulani angeweza kujitolea kuandika ufafanuzi mfupi wa kila neno ubaoni. Kisha ungeweza kusoma Mosia 15:1–9 pamoja. Jinsi gani Yesu Kristo alitosheleza matakwa ya haki? Ananyoosha vipi huruma yake kwetu? Video zilizopendekezwa katika “Nyenzo za Ziada” tumia hadithi na analojia kuelezea huruma ya Mwokozi; kuangalia moja ya video hizi kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kufikiria analojia zingine ambazo zinaonesha jinsi Yesu Kristo alivyotosheleza matakwa ya haki.

Mosia 11; 12:33–37; 13:11–26

Sheria zinapaswa kuandikwa katika mioyo yetu.

  • Unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa umuhimu wa kuwa na amri “zimeandikwa katika mioyo [yetu]” kwa kuwauliza nini wanafikiri msemo huu unamaana gani. Kisha watake kutofautisha amri alizofundisha Abinadi katika Mosia 12:33–37 na 13:11–26 pamoja na dhambi walizokuwa wanazifanya Mfalme Nuhu na watu wake (ona Mosia 11: 1–7, 13–15). Jinsi gani kuwa na amri “zimeandikwa katika mioyo [yetu]” ni tofauti na kuwa tu mzoefu nazo. (Mosia 13:11). Tunajuaje kama amri zimeandikwa katika mioyo yetu? Ni mifano gani tunaweza kushiriki?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Je, washiriki wa darasa wakati wowote wamehisi kama Adinadi alivyohisi—kwamba juhudi zao kushiriki injili zilikuwa bure? Waambie kwamba katika Mosia 18–26 watasoma kuhusu wingi wa tunda wa juhudi za Abinadi.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mafunzo ya kinabii kuhusu kusimama imara kwa ajili ya ukweli.

Rais Russell M. Nelson alifundisha: “Wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo wako tayari kujitokeza, kusema kwa ukakamavu, na kuwa tofauti na watu wa ulimwengu. … Hakuna kitu rahisi au cha kujiendesha chenyewe kuhusu kuwa wafuasi wenye nguvu. Lengo letu lazima liwe kujikita kwa Mwokozi na injili Yake. Ni vigumu kiakili kujitahidi kumtazama Yeye katika kila wazo. Bali wakati tunapofanya hivyo, wasiwasi wetu na hofu hukimkia” (“Kuleta Nguvu ya Yesu Kristo katika Maisha yetu,” Ensign au Liahona, Mei 2017,40–41).

Rais Thomas S. Monson alisema: “Acha daima tuwe jasiri na tayari kusimama imara kwa ajili ya kile tunachoamini na kama ni lazima tusimame peke yetu katika mchakato, na tufanye hivyo kwa ujasiri, tukiimarishwa na ufahamu kuwa kwa kweli kamwe hatuko peke yetu tunaposimama na Baba yetu wa Mbinguni” (“Dhubutu Kusimama Peke Yako,” Ensign au Liahona, Nov.2011, 67).

Rais Gordon B. Hinckley alifundisha: Paulo aliandika kwa Timotheo: ‘Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu’ (2 Tim. 1:7–8) Ningependa kwamba kila mshiriki wa kanisa hili angeyaweka maneno haya pale atakapoweza kuyaona kila asubuhi anapoanza siku yake. Yangetupa ujasiri wa kusema kwa ukakamavu, yangetupa imani ya kujaribu, yangeimarisha imani yetu ya Bwana Yesu Kristo” (Mafundisho ya Marais wa Kanisa: Gordon B. Hinckley [2016], 338).

Video kuhusu haki na huruma kwenye ChurchofJesusChrist.org.

  • “Handlel’s Messiah: Debtor’s Prison”

  • “Mpatanishi”

  • “Pale Haki, Upendo, na Rehema Hukutana”

Chapisha