Njoo, Unifuate
Mei 18–24. Mosia 26–28: “Waliitwa Watu wa Mungu”


“Mei 18–24. Mosia 25–28: ‘Waliitwa Watu wa Mungu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Mei 18–24. Mosia 25–28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Malaika anamtokea Alma na wana wa Mosia

Kuongoka kwa Alma Mdogo, na Gary L. Kapp

Mei 18–24.

Mosia 25–28

“Waliitwa Watu wa Mungu”

Njia nzuri zaidi kujiandaa kufundisha kuhusu Mosia 25–28 ni kusoma sura hizi na kuishi kwa kanuni zinazofundisha. Utakapofanya hivyo, Roho anaweza kukutia moyo kufundisha kile kitakachokuwa muhimu zaidi kwa ajili ya washiriki wako wa darasa.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kuwa wanajitahidi kuwa na mafunzo thabiti ya maandiko kibinafsi na kifamilia. Je, uzoefu wa washiriki wengine wa darasa utasaidia? Labda ungeweza kuanza darasa lako kwa kuwataka washiriki wa darasa kushiriki kitu fulani walichofanya katika mafunzo yao binafsi au na familia ambacho kilifanya vizuri.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mosia 26:15–31; 27: 23–37

Mungu kwa uhuru husamehe wale wanaotubu.

  • Toba na msamaha ni mada zinazorudiwarudiwa katika sura hizi. Ungeweza kutafiti mada hizi kwa kuandika Toba na Msamaha kwenye ubao na kuwataka washiriki wa darasa kuorodhesha chini ya vichwa hivyo vya habari kile kinachokuja akilini wanapofikiri juu ya maneno haya. Kisha wangeweza kuchambua Mosia 26:22–24, 27–31; na 27:23–37 kwa maneno na vishazi ambavyo vinafundisha kuhusu toba na msamaha. Washiriki wa darasa wangeweza kuongeza maneno haya na vishazi kwenye orodha ubaoni. Jinsi gani Mungu anahisi kuhusu wale wanaotubu na kutafuta msamaha?

  • Baadhi ya watu wanaweza kushangaa kama toba yao imekuwa ya kutosha kwa Mungu kuwasamehe. Kusaidia yeyote katika darasa lako ambaye anaweza kuhisi hivyo, ungeweza kuwataka washiriki wa darasa kufikiria kwamba wao ni Alma Mkubwa na kwamba mshiriki wa Kanisa katika Zerahemla amewauliza jinsi ya kupata msamaha wa dhambi zake (labda ungeigiza maonesho haya). Alma alijifunza nini kutoka kwa Bwana katika Mosia 26;15–31 ambacho kingeweza kumsaidia mshiriki huyu wa Kanisa? (Ona pia Moroni 6:8; M&M 58:42–43). Kauli hii kutoka kwa Rais Henry B. Eyring pia inasaidia: “kama umehisi ushawishi wa Roho Mtakatifu leo, unaweza kuchukua kama ushahidi kwamba Upatanisho unafanya kazi katika maisha yako.” (“Gifts of the Spirit for hard Times,” Ensign, Juni 2007, 23).

Mosia 27:8–24

Mungu anasikia sala zetu na atazijibu kulingana na mapenzi yake.

  • Wengi wetu tunaweza kulinganisha hisia za Alma Mkubwa, ambaye mwanawe alikuwa “anaasi dhidi ya Mungu” (Mosia 27:11). Labda washiriki wa darasa wangeweza kujadili jinsi wanaweza kutumia kauli katika Mosia 27:8–24 kutoa matumaini kwa mtu fulani ambaye ana familia yenye mwanafamilia mkaidi. Kuelewa kwamba hatuwezi kudai muujiza au kupuuza uhuru wa mtu fulani, tunaweza kufanya nini kwa njia ya kufaa kumwombea wakati mpendwa wetu anapotea? (ona pia Alma 6:6).

Mosia 27:8–28: 4

Wanaume wote na wanawake lazima wazaliwe mara ya pili.

  • Haya ni baadhi ya maswali ambayo yangeweza kusaidia washiriki wa darasa kujifunza kuhusu kuzaliwa mara ya pili: Inamaanisha nini kuzaliwa mara ya pili kiroho? (ona Kamusi ya Biblia, “Kuongoka”). Tunajitahidi vipi kufanya kuelekea wengine wakati tumezaliwa mara ya pili kiroho? Kuwasaidia washiriki wa darasa kujibu maswali haya, ungeweza kuwataka kupekua Mosia 27:22–28:4 kwa ajili ya ishara kwamba Alma na wana wa Mosia wamezaliwa mara ya pili kiroho.

  • Kila mmoja ana hadithi ya wongofu, kama vile Alma alivyosema, “wote binadamu … wote lazima wazaliwe mara ya pili” (Mosia 27:25; italiki zimeongezwa). Labda washiriki wa darasa wachache wangeweza kushiriki jinsi walivyoongolewa kwenye injili ya Yesu Kristo—kama kupitia matukio ya nguvu ya kiroho katika maisha yao au kupitia mchakato wa polepole, wakati mwingine usioeleweka ambao unaweza kutambulika tu katika baada ya jambo kutokea. Ungeweza pia kuwapa muda washiriki wa darasa kurekodi uzoefu wao. (Kama huna muda wa kufanya hivi darasani, ungeweza kupendekeza kwamba wafanye hivyo nyumbani.) Kusisitiza kwamba wongofu wetu unapaswa kuwa endelevu, ungeweza kupendekeza kwamba washiriki wa darasa kwa vipindi warejee upya kile walichoandika na kuongeza uzoefu mpya.

  • Alma na wengine katika maandiko yote wametumia sitiari ya kuwa wamezaliwa mara ya pili kuelezea mabadiliko ambayo injili ya Yesu Kristo inaleta katika maisha yetu. Mzee David A. Bednar alifananisha mabadiliko haya kwa tango kuwa achali (ona “Nyenzo za Ziada”) Kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari kile mifananisho hii inafundisha kuhusu wongofu, ungeweza kuleta tango na achali darasani. Au ungemtaka mtu fulani kumleta mtoto mchanga na kujadili kwa nini kuzaliwa ni analogia mzuri kwa kile kilichitokea kwa Alma na wana wa Mosia (Ona Mosia 27:23–28:7.)

Picha
Alma Mdogo akiwa anabebwa hadi nyumbani kwa baba yake

Baba Yake Alishangilia, na Walter Rane

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Kuwa tia moyo washiriki wa darasa kusoma Mosia 29–Alma 4 wiki ijayo, unaweza kutaja kwao kwamba katika sura hizi, watu wa Nefi walipewa sauti katika serikali yao. Tunaweza kujifunza nini kutokana na uzoefu wao tunapojaribu kushawishi jamii zetu kila siku.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Mchakato wa maisha.

Mzee D. Todd Christofferson alifundisha: “Kuzaliwa mara ya pili, tofauti na kuzaliwa kwetu kimwili, ni zaidi ya mchakato kuliko tukio. Na kushiriki katika mchakato huo ni lengo kuu la maisha ya muda” (“Kuzaliwa Mara ya Pili.,” Ensign au Liahona, Mei 2008, 78).

Kuongoka na achali.

Mzee David A. Bednar alishiriki mfano ufatao kufananisha kuzaliwa mara ya pili kiroho na matango achali:

“Achali ni tango ambalo limebailishwa kulingana na viungo maalum na hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza katika mchakato wa kubadili tango kuwa achali ni kuandaa na kusafisha. …

“Hatua zinazofuata katika mchakato huu wa mabadiliko ni kutumbukiza na kukoleza matango katika maji yaliyokifu chumvi kwa muda mrefu.… Matango yanaweza tu kuwa achali kama yametumbukizwa yote kabisa katika maji yaliyokifu ya chumvi kwa muda na kipindi kilichoshauriwa. Mchakato wakukoleza polepole unabadili asili ya tango na kuleta uonekano mwangavu na ladha tofauti ya achali. Kunyunyiza mara moja au kuchovya katika maji yaliyokifu chumvi haiwezi kuleta mabadiliko ya muhimu. Bali, kuzamishwa kabisa kwa uthabiti na uendelevu kunatakiwa kwa ajili ya mabadiliko yanayotamaniwa kutokea.

“Hatua ya mwisho katika mchakato kufungwa lakiri achali iliyokolezwa katika madumu ambayo yamefishwa vijidudu na kusafishwa. Achali zinafungwa katika madumu ya usindikaji, na kufunikwa na maji yaliyokifu ya chumvi yanayochemka, na kutengenezwa katika kopo la maji yanayochemka. Uchafu wote lazima utolewe kutoka mwote achali na chupa kwa hiyo bidhaa iliyokwisha tengenezwa inaweza kulindwa na kuhifadhiwa. …

“Kama vile tango lazima litayarishwe na kusafishwa kabla halijabadilishwa kuwa achali, kwa hiyo wewe na mimi tunaweza kuandaliwa na ‘maneno ya imani na mafundisho mazuri’ (1 Timotheo 4:6) na mwanzo kusafishwa kupitia ibada na maagano yakisimamiwa na mamlaka ya ukuhani wa Haruni. …

“Kama vile tango linavyobadilishwa kuwa achali linapozamishwa katika na kukolezwa na maji yaliyokifu ya chumvi, kwa hiyo wewe na nini tunazaliwa mara ya pili tunafyonzwa na injili ya Yesu Kristo. … Awamu hii ya mchakato wa mabadiliko huhitaji muda, kuendelea kuwepo na subira. …

“… Utaratibu wa birika la maji–yanayochemka unawezesha achali kuwa vyote kulindwa na kuhifadhiwa kwa muda wa vipindi virefu. Katika njia inayofanana na hii, polepole tunakuwa tuliosafishwa na kutakaswa wakati wewe na mimi tumesafishwa katika damu ya mwana kondoo, tumezaliwa mara ya pili, na kupokea ibada na kuheshimu maagano ambayo yamesimamiwa na mamlaka ya Ukuhani wa Melkizediki” (“Ye Must Be Born Again,” Ensign au Liahona, Mei 2007, 19–21).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jiandae ukiwa unawawazia watu akilini “Unapojitayarisha, acha uelewa wako juu ya wale unaowafundisha kuongoza mipango yako. … Walimu walio kama Kristo hawatumii mtindo au mbinu moja tu; wao hufanya kila juhudi kuwasaidia watu kujenga imani yao katika Yesu Kristo na kuzidi kuwa kama Yeye” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi 7).

Chapisha