Njoo, Unifuate
Aprili 27–Mei 3. Mosia 7–10: “Kwa Nguvu za Bwana”


“Aprili 27–Mei 3. Mosia 7–10 : ‘Kwa Nguvu za Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Aprili 27–Mei 3. Mosia 7–10,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Amoni akimfundisha Mfalme Limhi

Minerva K. Teichert (1888‑1976), Amoni mbele ya Mfalme Limhi, 1949‑1951, mafuta juu ya ubao, 35 15/16 x 48 inchi. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young, 1969.

Aprili 27–Mei 3

Mosia 7–10

“Kwa Nguvu za Bwana”

Muhtasari huu unaweza kuwa nyenzo ya thamani, lakini unapaswa kuongezea, sio kubadilisha, uvuvio unaopokea wakati ukijifunza Mosia 7–10.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kila baada ya kipindi fulani inaweza kusaidia kujadili kama darasa baraka ambazo washiriki wa darasa wanapokea wanapojitahidi kufanya nyumba zao kitovu cha kujifunza kwao injili. Ni mistari gani kutoka Mosia 7–10 ambayo washiriki wa darasa waliitafakari au kujadili katika nyumba zao kwa kipindi cha wiki? Ni kwa jinsi gani hii iliathiri maisha yao?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mosia 7:14–33

Kama tutamgeukia Bwana, kumwamini, na kumtumikia, Atatukomboa.

  • Washiriki wa darasa walipojifunza Mosia 7:14–33, uzoefu wa watu wa Limhi waweza kuwa umewapa msukumo kutubu na kumgeukia Bwana kwa ajili ya ukombozi. Ili kutia msukumo majadiliano, ungeweza kumwalika mshiriki wa darasa kuja darasani akiwa amejiandaa kutoa muhtasari wa jinsi watu wa Limhi walivyoingia utumwani. Wachache wengine wangeweza kushiriki kile walichojifunza kutoka kwa Limhi kuhusu kuwa na imani na matumaini katika Mwokozi. Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye vikumbushaji vya Limhi juu ya jinsi Mungu alivyowakomboa watu wake? (ona mstari 19–20). Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki maelezo ya maandiko au uzoefu binafsi ambao umewapa msukumo kumwamini Mungu.

  • Washiriki wa darasa lako wana nafasi za kuwapa msukumo wengine kumgeukia Mungu wakati wanapokuwa katika utumwa wa dhambi au kuteseka kutokana na mateso mengine. pengine ingewasaidia kujifunza jinsi Limhi alivyowapa msukumo watu wake. Wangeweza kwanza kusoma maelezo katika Mosia 7:20–25 juu ya utumwa wa watu wa Limhi na kufikiria juu ya mtu fulani wanayemjua anayekabiliwa na utumwa wa dhambi. Kisha wangeweza kutambua kweli ambazo Limhi alifundisha katika Mosia 7:18–20, 33 ili kuwasaidia watu wake. Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Limhi tunapowatia moyo wapendwa wetu kumwamini Mungu?

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema msaada Mungu anaotupatia wakati wa dhiki, mngeweza kuimba pamoja na kujadili wimbo “Mkombozi wa Israeli” (Nyimbo za Kanisa, na. 6) au wimbo mwingine ambao unaelezea jinsi Mwokozi anavyotukomboa. Ni nini Mosia 7:17–20; Etheri 12:27; na 2 Wakorintho 12:7–10 zinaongezea kwenye uelewa wetu? pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambapo walikombolewa na Bwana, hata katika njia ndogo, kwa sababu walionesha imani Kwake.

Mosia 7:26–27

Mtu ameumbwa kwa mfano wa Mungu.

  • Katika mistari hii, Limhi alielezea baadhi ya kweli zilizofundishwa na Abinadi ambazo zilikuwa ngumu kwa watu kuzikubali. Ni kweli zipi washiriki wa darasa wanaweza kutambua katika mistari hii? Ni kwa jinsi gani kweli hizi zinaathiri jinsi tunavyomwona Mungu na sisi wenyewe?

Mosia 8:12–19

Bwana anatoa manabii, waonaji, na wafunuzi kwa manufaa ya binadamu.

  • Amoni alipata nafasi ya kueleza kwa Limhi majukumu ya mwonaji na kushuhudia umuhimu wa manabii, waonaji, na wafunuzi. Unaweza kutaka kufafanua kwamba katika siku yetu, Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wamethibitishwa kama manabii, waonaji, na wafunuzi. Ni kwa jinsi gani sisi, kama Amoni, tunaweza kuzungumza kwa ujasiri kuhusu haja ya kuwa na manabii, waonaji, na wafunuzi? (ona Mosia 8:13–18). pengine washiriki wa darasa wangeweza kupanga tangazo kwenye mitandao ya kijamii ambalo lingesaidia wengine kuelewa jukumu la nabii, mwonaji, na mfunuzi katika siku yetu. Ni nini tulisikia katika mkutano mkuu wa hivi karibuni ambacho tungeweza kushiriki na rafiki zetu, wana familia, na majirani ili kuwafundisha kuhusu haja ya kuwa na manabii?

  • Kama matokeo ya kusoma Mosia 8:12–19, wewe au washiriki wengine wa darasa mnaweza kutaka kuelezea ushuhuda wenu wa manabii, kama Amoni alivyofanya au shukrani zenu kwa ufunuo kupitia manabii, kama Limhi alivyofanya (ona Mosia 8:19).

  • Nabii Joseph Smith ni mwonaji anayesimama mwanzoni mwa kipindi hiki cha maongozi ya Mungu (ona M&M 21:1). Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kile wanachojifunza kutokana na maelezo ya Amoni kuhusu mwonaji (ona Mosia 8:13–18). Kisha wangeweza kujadili jinsi ambavyo Joseph Smith alikuwa mwonaji. (D&C 135:3 and Moses 6:36 Ingeweza kuwa yenye msaada katika majadiliano haya.)

Mosia 9:14–19; 10:6–10

Tunaweza kukabiliana na changamoto zetu “Kwa Nguvu za Bwana.”

  • Maneno “kwa nguvu za Bwana” yanatokea mara mbili katika kumbukumbu ya Zenivu ya watu wake na vita vyao na Walamani—katika Mosia 9:14–19 na 10:6–10. pengine washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza mistari hii na kushiriki kile wanachohisi maneno haya yanamaanisha. Ni kwa jinsi gani tunafikia “nguvu za Bwana”? Watie moyo washiriki wa darasa kushiriki uzoefu ambapo walikabiliana na changamoto kwa mafanikio kwa nguvu za Bwana.

Mosia 10:11–17

Chaguzi zetu zinaweza kushawishi vizazi.

  • Ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma kimya kimya Mosia 10:11–17 na kutafuta jinsi Walamani walivyoathirika kwa chaguzi na imani za mababu zao. Hii inapendekeza nini kuhusu athari ambazo chaguzi zetu zinaweza kuwa nazo kwa wengine? Ni kwa jinsi gani tungetaka sisi wenyewe na familia zetu kuelezewa katika kizazi kimoja au viwili? pengine washiriki wa darasa wangeweza kuandika baadhi ya mambo ambayo wangependa yajumuishwe kwenye maelezo kama hayo.

  • Somo rahisi la vitendo—kama vile mstari wa dhumna—ungeweza kusaidia kuonesha athari ambazo chaguzi za watu zinaweza kuleta kwa vizazi vyao vya baadae. Kisha ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma Mosia 10:11–17 na kujadili jinsi imani na mitazamo ya Walamani ilivyoathirika kwa kiasi kikubwa kwa chaguzi zilizofanywa na mababu zao karne nyingi zilizopita. Hadithi ya Mzee Donald L. Hallstrom, inayopatikana katika “Nyenzo za Ziada,” ni mfano mwingine ambao ungeweza kushiriki. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kufikiria hadithi kutoka kwenye maisha yao au kwenye historia ya familia zao kuhusu mtu mmoja mwenye haki akishawishi vizazi kwa wema.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wiki hii washiriki wa darasa walijifunza kuhusu athari hasi ambazo chaguzi za Walamani zilikuwa nazo kwa watoto wao. Wafahamishe washiriki wa darasa kwamba katika Mosia 11–17 watasoma kuhusu mtu mmoja ambae uadilifu wake ulibadili maisha ya wengi.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Chaguzi zetu zinaweza kuathiri vizazi.

Mzee Donald L. Hallstrom alishiriki jinsi uaminifu wa mababu zake ulivyobariki vizazi vya baadae:

“Mababu zangu upande wa baba walikuwa na watoto wawili, mvulana (baba yangu) na binti. … [Binti yao] aliolewa mwaka 1946 na miaka minne baadae alikuwa anatarajia mtoto. Kuna kitu fulani maalum sana kwa wazazi kutumainia binti (katika mfano huu binti pekee) kujifungua kwa mara ya kwanza. Hakuna aliyejua kwamba alikuwa na mapacha. Kwa huzuni, Yeye na mapacha walikufa wakati wa kujifungua.

“Mababu zangu walivunjika mioyo. Huzuni yao, hata hivyo, mara moja iliwageuza kwa Bwana na Upatanisho Wake. Bila kufikiria sana juu ya kwa nini hili lingeweza kutokea na ni nani angeweza kulaumiwa, walifokasi kwenye kuishi maisha ya uadilifu. Mababu zangu kamwe hawakuwa na utajiri; hawakuwa kamwe miongoni mwa tabaka la kijamii la watu wenye uwezo; kamwe hawakuwa na nafasi za juu katika Kanisa—walikuwa tu Watakatifu wa Siku za Mwisho waaminifu. …

“Uaminifu wa Babu Art na Bibi Lou, hususani walipokabiliwa na matatizo, sasa umeathiri vizazi vinne ambavyo vimefuata. Moja kwa moja na kwa kiasi kikubwa sana, ulimuathiri kijana wao (baba yangu) na mama yangu wakati binti pekee wa wazazi wangu, mtoto wao wa mwisho, alipokufa kutokana na matatizo yaliyosababishwa na kujifungua. Katika umri wa miaka 34 , alifariki siku 10 baada ya kujifungua mtoto, akiacha watoto  4, wa kuanzia siku 10 hadi umri wa miaka 8. Kwa mfano ambao walikuwa wameuona katika kizazi kilichopita, wazazi wangu—bila kusita—walimgeukia Bwana kwa ajili ya faraja” (“Mgeukie Bwana,” Ensign au Liahona, Mei 2010 78–79).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Sikiliza. “Kusikiliza ni tendo la upendo. … Muombe Baba wa Mbinguni akusaidie kuelewa kile washiriki wa darasa lako wanachosema. Unapotoa usikivu wa makini kwa jumbe zao zinazozungumzwa na zisizozungumzwa, utakuja kuelewa vyema mahitaji yao, mashaka yao, na matamanio yao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 34).

Chapisha