Njoo, Unifuate
Aprili 20–26. Mosia 4–6: “Mabadiliko Makuu”


April 20–26. Mosia 4–6: ‘Mabadiliko Makuu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

April 20–26. Mosia 4–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Mfalme Benyamini akifundisha Watu Wake

Mnamtumikia tu Mungu Wenu, na Walter Rane

Aprili 20–26.

Mosia 4–6

“Mabadiliko Makuu”

Soma Mosia 4–6, na uandike misukumo yako ya kiroho. Unapopokea misukumo, unaweza kuuliza kama Mzee Richard G. Scott alivyopendekeza, “Kuna chochote zaidi ningetakiwa kujua?” (“To Acquire Spiritual Guidance,”,” Ensign au Liahona, Nov.2009, 8).

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni kushiriki

Alika Kushiriki

Unaweza kutaka mjadala na darasa lako kwa kuwataka kushiriki mojawapo ya mafundisho ya Mfalme Benyamini kutoka Mosia 4–5 ambayo wangependa kutumia zaidi katika maisha yao.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mosia 4:1–12

Kupitia Yesu Kristo, tunaweza kupokea na kubakiza msamaha wa dhambi zetu.

  • Baadhi ya watu wanakosea kimawazo kwamba toba inahitaji juhudi ndogo; wengine wanaamini inahitaji juhudi kubwa mno. Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa vyema nini kinahitajika kupokea msamaha wa dhambi, ungewataka kupekua mafundisho ya Mfalme Benyamini katika Mosia 4:1–12, kutafuta hali ambayo chini yake Baba wa Mbinguni anatoa ruhusa ya msamaha wa dhambi zetu. Washiriki wa darasa wanaweza kuorodhesha ubaoni kile wanachopata. Watake kufikiria analojia kusaidia kueleza kile walichojifunza. Kwa mfano, wangeweza kufananisha msamaha wa dhambi kwa mdaiwa “kusamehewa” au deni kufutwa. Au wangeweza kufananisha kubakiza msamaha wa dhambi zetu kwa kutunza kitu fulani ambacho kinahitaji matengenezo ya mara kwa mara, kama vile bustani au nyumba.

  • Fikiria kuwauliza washiriki wa darasa nini wangesema kwa mtu fulani anayeshangaa kama toba inastahili juhudi hizo. Wangemsaidia vipi mtu fulani ambaye amekata tamaa na anahisi kwamba kushinda dhambi na udhaifu haiwezekani? Ungeweza kuwatayarisha washiriki wa darasa kwa mazungumzo kama haya kwa kuwataka kutumia dakika chache kuchambua maneno ya Mfalme Benyamini katika Mosia 4:1–12 kwa ajili ya kweli ambazo zingemsaidia mtu fulani katika moja ya hali hizi. Washiriki wa darasa kisha wanaweza kushiriki kweli walizogundua pamoja na mtu fulani ambaye amekaa karibu nao.

Mosia 4:11–27

Tunapotubu, tutajazwa na upendo wa Mungu.

  • Tunajuaje kama tumepokea msamaha wa dhambi zetu? Mfalme Benyamini alielezea baadhi ya matokeo ya toba ya kweli—watake washiriki wadarasa lako kuzitafuta katika Mosia 4:13–16. Ungeweza pia kuwataka kutafakari maisha yao wenyewe na kutathmini jinsi gani wanavyoishi vyema mafundisho katika mistari hii. Ni ishara gani washiriki wa darasa wanaziona kwamba wanaongolewa? Jinsi gani uhusiano wetu na wengine unabadilika tunapokuja kwa Kristo kupitia toba? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi walivyoona hii ikitokea katika maisha yao.

  • Mosia 4:11–12 na 14–16 ingeweza kushawishi majadiliano kuhusu nini kinavutia uzazi wenye haki. Mistari hii inafundisha nini kuhusu jinsi yakuwa wazazi bora?

  • Kama unahisi kuvutiwa kuwa na majadiliano kuhusu mafundisho ya Mfalme Benyamini kuhusu kuwatunza masikini na wenye mahitaji, unaweza kuwataka washiriki wa darasa kuchukuwa zamu kusoma mistari kutoka Mosia 4:16–27. Baada ya kila mstari kusomwa, mtu aliyesoma anaweza kutoa muhtasari katika maneno yake mwenyewe kile Mfalme Benyamini alichofundisha. Ujumbe wa Mzee Jeffrey R. Holland “Si Sisi Wote ni Waombaji?” (Ensign au Liahona, Nov. 2014, 40–42) unaweza kutumika kuongezea majadiliano haya. Jinsi gani tunaweza kufuata ushauri wa Mfalme Benyamini kutofanya “Kukimbia zaidi kuliko uwezo [tulio nao]”? (Mosia 4:26–27). Jinsi gani amri “kuwapa [tulichonacho] masikini” inafanana na msamaha wa dhambi zetu?

Mosia 4:29–30

Lazima tuchunge mawazo, maneno na matendo yetu.

  • Wakati mwingine inaonekana kama ingekuwa rahisi zaidi kama Bwana angetupa orodha ya kila kitu ya kila uwezekano wa dhambi. Badala yake, Anatuambia , “Jiangalieni wenyewe… na muendelee katika imani ya kile mlichosikia kuhusu ujio wa Bwana wetu” (Mosia 4:30). Kusaidia darasa lako kujadili kanuni hii, ungeweza kuwauliza maswali kama haya: Jinsi gani mawazo, maneno na matendo yetu yanatuathiri sisi wenyewe na wengine? Inamaanisha nini “kuendelea katika imani”? Ni ushauri gani tunaweza kushiriki sisi kwa sisi kutusaidia “kujilinda” wenyewe?

Mosia 5:1–7

Roho wa Bwana anaweza kusababisha mabadiliko makuu katika mioyo yetu.

  • Kuanza majadiliano kuhusu badiliko lisilo na kifani ambalo injili ya Yesu Kristo inaweza kuleta kwenye maisha yetu, unaweza kuwataka washiriki wa darasa kushiriki baadhi ya sababu kwa nini mara kwa mara ni vigumu kufanya mabadiliko ya kudumu katika maisha yetu. Kisha watake kusoma Mosia 5:1–5, wakitafuta “mabadiliko makuu” ambayo watu wa Mfalme Benyamini walipata uzoefu wake. Ni kweli gani kuhusu mabadiliko ya mawazo tunayojifunza kutoka uzoefu wao? Fikiria kuwataka washiriki wachache wa darasa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu aliwasaidia kubadili mioyo yao. Mngeweza pia kuangalia mojawapo ya video iliyopendelezwa katika “Nyezo za Ziada.”

    Picha
    Kristo Akimponya mwanamke mgonjwa

    Mwokozi anaweza kubadili mioyo yetu na maisha yetu. Mikono Iponyayo, na Adam Abram

  • Baada ya kujadili kweli katika Mosia 5:1–7, baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kushangaa kwa nini mabadiliko yao ya mawazo hayaonekani kama ya kuvutia au mara moja kama uzoefu wa watu wa Mfalme Benyamini. Kauli kutoka kwa Mzee D. Todd Christofferson katika “Nyenzo za Ziada” inaelezea swali hili. Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Mzee Christofferson kuhusu kuongoka?

Mosia 5:5–15

Mungu ananialika kufanya maagano na Yeye.

  • Mosia 5:5–15 inaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa baraka wanazopata wakati wanapofanya na kuweka maagano na Mungu. Unaweza kuwataka kurejea upya mistari hii na maagano ya ubatizo na ibada ya sakramenti akilini na kushiriki kile wanachojifunza (Ona pia M&M 20:77, 79.)

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Washiriki wengi wa darasa lako wanaweza kuwa wanapata uzoefu au hivi karibuni wamepata uzoefu wa jitihada binafsi au majaribu. Waambie kwamba katika Mosia 7–10 watasoma kuhusu kundi la watu waliojifunza jinsi ya kumtegemea Bwana nyakati za majaribu yao.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Video kwenye ChurchofJesusChrist.org kuhusu “mabadiliko makuu” (Mosia 5:2).

  • “Mkate wa kila siku: Mabadiliko”

  • “Badiliko la Mawazo”

  • “Mabadiliko Makuu: Uongofu”

Mabadiliko mara kwa mara ni mchakato.

Mzee D. Todd Christofferson alizungumza juu ya mabadiliko makuu ya moyo yaliyoelezwa katika maandiko:

“Unaweza kuuliza, Kwa nini mabadiliko haya makuu hayatokei haraka zaidi kwangu mimi? Unapaswa kukumbuka kwamba mifano ya ajabu ya watu wa Mfalme Benyamini, Alma, na wengine kadha katika maandiko ni kama hivyo—ni ya ajabu na sio ya kawaida. Kwa wengi wetu, mabadiliko ni taratibu zaidi na yanatokea kwa muda mrefu. Kuzaliwa mara ya pili, tofauti na kuzaliwa kwetu kimwili, ni mchakato zaidi kuliko tukio. Na kujihusisha katika mchakato huo ndio lengo kuu la maisha.”

“Wakati huohuo, tusijihalalishe wenyewe katika juhudi za kawaida. Tusiridhike kubakiza kiasi kidogo cha kufanya dhambi. Acha kwa kustahili tupokee sakramenti kila wiki na kuendelea kumtegemea Roho Mtakatifu kuondoa dalili mabaki ya uchafu ndani yetu. Ninashuhudia kwamba mtakapoendelea katika njia ya kuzaliwa upya kiroho, neema ya upatanisho wa Yesu Kristo itaondoa dhambi zenu na madoa ya dhambi hizo ndani yenu, majaribu yatapoteza mvuto wake, na kupitia Kristo mtakuwa watakatifu, kama Yeye na Baba yetu walivyo watakatifu” (“Kusaliwa Tena,” Ensign au Liahona, Mei 2008, 78).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kutafuta mifano mizuri katika maandiko. Unaposoma mahubiri ya Mfalme Benyamini kwa watu wake, tafuta masomo katika mfano wake ambao unaweza kukusaidia kuwa mwalimu mzuri. Kwa mfano, Mfalme Benyamini alifanya nini kujua kama watu wake walielewa kile alichukuwa anafundisha?

Chapisha