Njoo, Unifuate
Machi 30–Aprili 12. Pasaka: “Atafufuka … Na Uponyaji katika Mabawa Yake”


“Machi 30–Aprili 12. Pasaka: ‘Atafufuka … Na Uponyaji katika Mabawa Yake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Machi 30–Aprili 12. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Picha
Kristo mfufuka pamoja na Mitume Wake

Kristo na Mitume, na Del Parson

Machi 30–Aprili 12

Pasaka

“Atafufuka … na Uponyaji katika Mabawa Yake”

Jumapili ya Pasaka ni nafasi nzuri sana kwa washiriki wa darasa lako kuimarisha shuhuda zao za Yesu Kristo na Ufufuo Wake—na kuimarisha shuhuda zao wao kwa wao. Weka hili akilini mwako unapojifunza maandiko katika kujiandaa kwa ajili ya somo hili. Tafuta mwongozo wa kiroho kuhusu kile kitakachogusa mioyo ya watu katika darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wamepata uzoefu wenye maana wiki mbili zilizopita kwa kusoma kile Kitabu cha Mormoni kinachofundisha kuhusu Ufufuo na Upatanisho wa Yesu Kristo. Wape dakika chache kutafuta kifungu ambacho kiliwavutia, na kisha waalike kushiriki kile walichokipata.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

2 Nefi 9:7–15; Alma 11:41–45; 40:21–23

Ufufuo ni muunganiko wa kudumu wa mwili na roho.

  • Kulinganisha kunaweza kuwa njia ya kufaa kufundisha kanuni za injili. pengine ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusoma 2 Nefi 9:7–15 na Alma 11:41–45 na kutambua maneno na vifungu vya maneno katika mistari hii ambavyo vinafundisha kuhusu ufufuo. Kifo kimefananishwa na nini? Ufufuo umeelezewaje? Kwa nini tunahitaji mwili uliofufuka? (Ona pia M&M 93:33–34). Washiriki wa darasa wangeweza kujadili jinsi wanavyoweza kutumia kulinganisha huku kumfundisha mtu fulani kuhusu ufufuo. Wanaposhiriki mawazo yao na darasa, ungeweza kujadiliana nao kwa nini wanathamini kweli hizi kuhusu Ufufuo.

  • Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki nyakati walipohisi shukrani kwa ajili ya ufahamu wao kuhusu Ufufuo. Ni kwa jinsi gani ufahamu huo unaweza kuathiri maisha yetu mara kwa mara? Ungeweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujibu swali hili kwa kumualika kila mmoja wao kuchunguza 2 Nefi 9:7–15; Alma 11:41–45; au Alma 40:21–23 na kuorodhesha ubaoni kweli wanazozipata kuhusu Ufufuo. Kisha ungeweza kuandika ubaoni sentensi mbili zifuatazo na kuwaomba washiriki wa darasa kutafakari kwa dakika chache kabla ya kushiriki jinsi ambavyo wangeweza kuzikamilisha: Kama nisingejua vitu hivi… na Kwa sababu ninajua vitu hivi….

Picha
Yesu akisali katika Bustani ya Gethsemane

Gethsemane, na Michael T. Malm

Mosia 3:5–7; 15:5–9; Alma 7:11–13

Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zetu, maumivu, na udhaifu.

  • Kutafakari na kujadili mateso ya Mwokozi kwa niaba yetu kunaweza kumwalika Roho na kushawishi hisia za upendo na shukrani kwa Mwokozi. Ili kuhimiza kutafakari na majadiliano kama haya, ungeweza kuchora chati ubaoni inayofanana na ile iliyopendekezwa kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na waalike washiriki wa darasa kuikamilisha wakitumia Mosia 3:5–7; 15:5–9; na Alma 7:11–13 na uzoefu wao wenyewe. Kadiri Roho anavyoelekeza, ungeweza pia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki hisia zao kuhusu kile ambacho Yesu Kristo amewafanyia.

  • Muziki mtakatifu unaweza kumwalika Roho na kuimarisha mafundisho unayofundisha. pengine washiriki wa darasa wangeweza kurejea Mosia 3:5–7; 15:5–9; na Alma 7:11–13 na kutafuta na kuimba nyimbo ambazo wanahisi zinaendana na jumbe katika mistari hii (ungeweza pia kumwalika mtu fulani kuimba au kupiga nyimbo). Kielelezo cha maandiko mwishoni mwa kitabu cha nyimbo za kanisa kinaweza kusaidia, na nyimbo zingine zimependekezwa katika “Nyenzo za Ziada.” Wahimize washiriki wa darasa kushiriki vifungu vya maneno kutoka kwenye nyimbo za kanisa na maandiko ambayo yanawasaidia kutambua dhabihu ya Mwokozi kwa kina zaidi.

Enoshi 1:1–19; Mosia 5:1–2; 27:8–28:4; Alma 24:7–19

Upatanisho wa Yesu Kristo unatutakasa na kusaidia kutukamilisha.

  • Njia moja ya kufaa kujifunza kuhusu uwezo wa Mwokozi kubadili maisha yetu ni kujifunza mifano ya jinsi alivyobadili maisha ya wengine pale walipotubu na kuja kwake. Kitabu cha Mormoni kina mifano mingi kama hiyo. pengine ungeweza kumpangia kila mshiriki wa darasa kusoma kuhusu mojawapo ya mifano hii, kama vile Enoshi (ona Enoshi 1:1–19), Watu wa Mfalme Benyamini (ona Mosia 5:1–2), Alma Mdogo (ona Mosia 27:8–28:4), au Waanti-Nefi-Lehi (ona Alma 24:7–19).), au wangeweza kufikiria mifano mingine kutoka kwenye maandiko. Kisha washiriki wachache wa darasa wangeweza kutoa muhtasari wa uzoefu waliosoma. pengine darasa lako lingefurahia kufanya hivi kwa kutoa vidokezo kusaidia darasa zima kubahatisha nani wanayemwelezea. Wangeweza pia kujadili maswali kama haya: Ni kwa jinsi gani watu katika mifano hii walibadilika? Nini ulikuwa wajibu wa Mwokozi katika badiliko lao? pengine washiriki wachache wa darasa wangeweza kuzungumza kuhusu jinsi Mwokozi alivyoleta “mabadiliko makuu … katika mioyo [yao]” (Mosia 5:2). Ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi Mwokozi anavyotubadili—na kwa nini badiliko hilo ni muhimu sana—ungeweza kushiriki pamoja na darasa analojia iliyotolewa na Rais Dallin H. Oaks katika “Nyenzo za Ziada.”

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ili kuwatia moyo washiriki wa darasa kusoma Mosia 1–3, ungeweza kuwaalika kutafakari wakati walipohisi hamu ya kufurahi baada ya kusoma au kusikia ujumbe wa injili. Waalike kutafuta kweli wanazoweza kufurahia wanaposoma Mosia 1–3.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Nyimbo za Kanisa kuhusu Upatanisho wa Mwokozi.

Video za Kwaya ya Tabernacle ikiwa Temple Square ikiimba baadhi ya nyimbo hizi zinaweza kupatikana kwenye ChurchofJesusChrist.org.

Analojia: Lazima tuwe zaidi ya wasafi.

Rais Dallin H. Oaks alishiriki analojia kueleza jinsi Mwokozi anavyotuandaa kurudi kwenye uwepo wa Mungu:

“Tunapenda kufikiria juu ya matokeo ya toba kama tu kutusafisha kutokana na dhambi, lakini huo ni mtazamo usio kamili. … Mtu anayefanya dhambi ni kama mti ambao unapinda kirahisi katika upepo. Siku ya upepo na mvua, mti unapinda sana dhidi ya ardhi kwamba majani yanachafuka kwa matope, kama dhambi. Kama tutalenga tu kwenye kusafisha majani, udhaifu katika mti ambao uliuruhusu kupinda na kuchafua majani yake unaweza kubaki. Vile vile, mtu ambaye anasikitika tu kwa kuchafuliwa na dhambi atafanya dhambi tena katika upepo mkali ujao. Wepesi wa kuhisi kurudia unaendelea mpaka pale mti unapokua umeimarishwa.

“Wakati mtu anapokuwa amepitia mchakato ambao matokeo yake ni yale ambayo maandiko yanaita ‘moyo uliopondeka na roho iliyovunjika,’ Mwokozi anafanya zaidi ya kumtakasa mtu yule kutokana na dhambi. Anampa nguvu mpya. Uimarishwaji huo ni muhimu kwetu ili kuelewa lengo la utakaso, ambalo ni kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni. Ili kuruhusiwa kuingia kwenye uwepo Wake, lazima tuwe zaidi ya wasafi. Lazima pia tuwe tumebadilishwa kutoka mtu dhaifu kimaadili ambaye amefanya dhambi kuwa mtu imara na mwenye msimamo wa kiroho ili kuishi katika uwepo wa Mungu” (“Upatanisho na Imani,” Ensign, Apr. 2010, 33–34).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ishi kwa kustahili mwongozo wa Roho. Unapoishi injili, unastahili wenza wa Roho, ambaye ni mwalimu halisi. Unapotafuta mwongozo Wake, Roho Mtakatifu atakupa mawazo na ushawishi kuhusu jinsi ya kukidhi mahitaji ya wale unaowafundisha. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 5.)

Chapisha