Njoo, Unifuate
Aprili 13–19. Mosia 1–3: “Kujazwa na Upendo kwa Mungu na kwa Watu Wote”


“April 13–19. Mosia 1–3: ‘Kujazwa na Upendo kwa Mungu na kwa Watu Wote,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“April 13–19. Mosia 1–3,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2020

Mfalme Benyamini akifundisha Watu Wake

Minerva K. Teichert (1888–1976), Mahubiri ya Mwisho ya Mfalme Benyamini, 1935, mafuta juu ya ubao, 36 x 48 inchi. Makumbusho ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Brigham Young

Aprili 13–19

Mosia 1–3

“Kujazwa na Upendo kwa Mungu na kwa Watu Wote”

Kuna kanuni nyingi katika Mosia 1–3 ambazo ungeweza kujadili na darasa lako. Sali kwa ajili ya mwongozo kujua kanuni zipi zitakuwa zenye maana sana kwa wale unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwapa washiriki wa darasa nafasi ya kuzungumza kuhusu kujifunza kwao binafsi au na familia juu ya Mosia 1–3, waalike kushiriki na mtu mwingine mstari ambao wanaona una uvuvio.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mosia 2:1–9

Kupokea neno la Mungu kunahitaji maandalizi.

  • Njia moja ya kuanza majadiliano kuhusu kujiandaa kupokea neno la Mungu ingeweza kuwa kuzungumza kuhusu matokeo ya kujiandaa—au kutokujiandaa—kwa ajili ya vitu vingine. Kwa mfano, washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu kuhusu jinsi maandalizi yao au ukosefu wa maandalizi ulivyoathiri uzoefu waliokuwa nao shuleni au kazini au baadhi ya shughuli zingine. Baada ya kushiriki, ungeweza kuwaalika nusu ya darasa kusoma Mosia 2:1–9, wakitafuta vitu ambavyo watu wa Mfalme Benyamini walifanya kujiandaa kupokea neno la Mungu. Nusu nyingine wangeweza kupekua mistari ile ile, wakitafuta vitu alivyofanya Mfalme Benyamini ambavyo vinaonesha jinsi alivyohisi kuhusu neno la Mungu na haja ya kulishiriki. Kisha liombe kila kundi kushiriki mawazo yao. Tunaweza kujifunza nini kutoka kwenye mistari hii ambacho kinaweza kutusaidia kupokea neno la Mungu?

Mosia 2:10–26

Tunapowatumikia wengine, tunamtumikia Mungu pia.

  • Mfalme Benyamini alikuwa mtumishi wa mfano kwa Mungu na kwa wale waliomzunguka. Ni kitu gani washiriki wa darasa lako wanaweza kujifunza kutoka kwake ili kiwasaidie katika juhudi zao za kuwatumikia wengine? Fikiria kuanza majadiliano kwa kuwaomba washiriki wa darasa kuorodhesha vikwazo watu wanavyokabiliana navyo wanapotoa huduma kwa wengine—kama vile sababu za kwa nini hatuhudumu au sababu ya huduma yetu kutokuwa yenye msaada kama ilivyotakiwa iwe. Kisha wangeweza kujifunza Mosia 2:10–26 na kutengeneza orodha ya kweli Mfalme Benyamini alizofundisha kuhusu kutumikia wengine ambazo zinaweza kuwasaidia kushinda vikwazo walivyoorodhesha. Ni nini watu binafsi na familia wanaweza kufanya kufokasi kwenye huduma katika maisha yao ya kila siku? Fikiria kushiriki hadithi ya Rais Thomas S. Monson katika “Nyenzo za Ziada” kama pendekezo moja.

  • Wimbo wa Kanisa kama vile “A Poor Wayfaring Man of Grief” (Nyimbo za Kanisa, na. 29) au video kama vile “The Old Shoemaker” (ChurchofJesusChrist.org) ingeweza kuimarisha ujumbe unaopatikana katika Mosia 2:17—tunapowatumikia wengine, tunamtumikia Mungu. Ni kwa jinsi gani ungeweza kutumia nyenzo kama hizo kuimarisha ujumbe wa Mfalme Benyamini? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao wameupata kwa kuwatumikia wengine au kupokea huduma kama ya Kristo kutoka kwa mtu mwingine. Kama sehemu ya mjadala wenu, fikiria kushiriki nukuu hii kutoka kwa Rais Henry B. Eyring: “Tunapotoa msaada kwa yeyote, Mwokozi anahisi ni kama tumenyoosha mkono kumsaidia Yeye” (“Je, Hii Siyo Saumu Niliyochagua?Ensign au Liahona, Mei 2015, 22). Kwa nini unafikiri tunamtumikia Mungu wakati tunapowatumikia watu wengine?

Wanawake wawili wakikumbatiana

Kuwatumikia wengine kunatusaidia kuhisi upendo wa Mungu.

Mosia 2:38–41

Furaha inakuja kutokana na kutii amri za Mungu.

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa “kutafakari juu ya hali ya baraka na furaha ya wale wanaotii amri za Mungu,” ingeweza kusaidia kuanza na ufafanuzi wa furaha. Ni kwa jinsi gani washiriki wa darasa wangeweza kuelezea furaha ambayo huja kutokana na utiifu kwa Mungu? Labda wangeweza kufikiria kwamba wana rafiki ambaye anasema kwamba yeye ni mwenye furaha bila kutii amri. Waalike kusoma Mosia 2:38–41 na kujadili jinsi ambavyo wangeweza kumsaidia rafiki yao kuelewa tofauti kati ya furaha ya kiulimwengu na furaha ya milele. Ni uzoefu au mifano gani kutoka kwenye maisha ya watu washiriki wa darasa wanaweza kushiriki ambayo inatoa mfano wa furaha ya milele?

Mosia 3:1–20

Wokovu unakuja tu “kupitia jina la Kristo, Bwana,”

  • Ujumbe wa Mfalme Benyamini ni pamoja na unabii wenye nguvu na wenye maelezo kuhusu kuzaliwa, huduma, na dhabihu ya upatanisho wa Yesu Kristo. Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki mistari kutoka Mosia 3:1–20 ambayo kwa kipekee inawavutia na kuwasaidia kumwelewa Mwokozi na wito wake. Waombe kushiriki kwa nini mistari hii inawavutia.

  • Utangulizi wa Kitabu cha Mormoni unafundisha kwamba kitabu “kinadokeza juu ya mpango wa wokovu.” Kuwasaidia washiriki wa darasa kuona jinsi mahubiri ya Mfalme Benyamini yanavyosaidia kukamilisha lengo hili la Kitabu cha Mormoni, ungeweza kuandika ubaoni Yesu Kristo Anafanya Wokovu Uwezekane. Washiriki wa darasa wangeweza kurejea Mosia 3:1–20, na kisha wewe au wao mngeweza kuorodhesha ubaoni kweli wanazojifunza kuhusu mpango wa wokovu. Waulize washiriki wa darasa nini wanajifunza kuhusu jinsi Yesu Kristo anavyofanya mpango wa wokovu uwezekane. Kisha wape washiriki wa darasa muda wa kupitia tena Mosia 3:18–19 na kushiriki kile tunacholazimika kufanya ili tuwe watakatifu na kupokea wokovu. Ni kwa jinsi gani Upatanisho wa Yesu Kristo unatusaidia kukamilisha hili? Waombe washiriki wa darasa kushiriki hisia zao kuhusu jukumu la Mwokozi katika mpango wa wokovu.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Je, washiriki wa darasa lako wamewahi wakati wowote kuwa na uzoefu wakati mafundisho yaliyofundishwa katika hubiri, somo, au maandiko yaliwabadili? Waambie kwamba katika Mosia 4–6 watasoma kuhusu athari za kuvutia ambazo kweli zilizofundishwa na Mfalme Benyamini zilileta kwa watu wake.

ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

Kuwatumikia Wengine.

Rais Thomas S. Monson alisema:

“Miaka michache iliyopita nilisoma makala iliyoandikwa na Jack McConnell, MD. Alikulia katika milima ya kusini magharibi ya Virginia katika nchi ya Marekani akiwa mmoja wa watoto saba wa mchungaji wa Kimethodisti na mama wa nyumbani. Hali zao zilikuwa duni sana. Alielezea kwamba wakati wa utoto wake, kila siku familia ilipoketi kuzunguka meza ya chakula, baba yake angewauliza kwa zamu kila mmoja, ‘Na ulifanya nini kwa ajili ya mtu fulani leo?’ Watoto walidhamiria kufanya jambo jema kwa zamu kila siku ili waweze kutoa taarifa kwa baba yao kwamba wamemsaidia mtu fulani. Dkt. McConnell anaita zoezi hili urithi wa thamani kuu wa baba yake, kwani mategemeo na yale maneno yalimvutia yeye na ndugu zake kusaidia wengine maisha yao yote. Walipokua na kupevuka, sababu yao ya kutoa huduma ilibadilika na kuwa hamu ya ndani ya kusaidia wengine.

“Licha ya kazi yenye heshima ya udaktari ya Dkt. McConnell … alianzisha shirika analoliita Volunteers in Medicine, ambalo linawapa matabibu wastaafu nafasi ya kujitolea kwenye kliniki za bure zikiwahudumia wafanyakazi wasio na bima. Dkt. McConnell alisema muda wake wa mapumziko tangu alipostaafu ‘umeyeyuka na kuwa masaa 60 ya wiki ya kazi isiyo na malipo, lakini kiwango cha nguvu [zake] kimeongezeka na kuna kuridhika katika maisha [yake] ambako hakukuwepo kabla.’ [Jack McConnell, “Na ni Nini Ulichofanya Kwa Ajili ya Mtu Fulani Leo?“ Newsweek, Juni 18, 2001, 13.] …

“Kwa vyovyote, hatuwezi sote kuwa Dkt. McConnell, kuanzisha kliniki za matibabu kuwasaidia masikini; hata hivyo, mahitaji ya wengine yapo sana, na kila mmoja wetu anaweza kufanya kitu kumsaidia mtu fulani. …

“Akina kaka na dada zangu, tumezungukwa na wale wanaohitaji usikivu wetu, himizo letu, msaada wetu, faraja yetu, ukarimu wetu—wawe wanafamilia, marafiki, jamaa, ama wageni. Sisi ni mikono ya Bwana hapa duniani, tukiwa na jukumu la kuwatumikia na kuwainua watoto Wake. Anatutegemea kila mmoja wetu. … Hebu tuweze kujiuliza swali ambalo liliwakabili Dkt. Jack McConnell na kaka zake na dada zake kila jioni kwenye meza ya chakula: ‘Je, Nimefanya nini kwa ajili ya mtu fulani leo?” ” (“Je, Nimemfanyia Nini kwa ajili ya Mtu Fulani Leo?Ensign au Liahona, Nov. 2009, 84–87).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa chombo cha Roho. Lengo lako kama mwalimu sio kuwasilisha somo bali ni kuwasaidia wengine kupokea ushawishi wa Roho Mtakatifu—ambaye ni mwalimu wa kweli. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 10.)