“Machi 30–Aprili 12. Pasaka: ‘Atafufuka … na Uponyaji Katika Mbawa Zake’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)
“Machi 30–Aprili 12. Pasaka,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020
Machi 30–Aprili 12
Pasaka
“Atafufuka … na Uponyaji Katika Mbawa Zake”
Wakati wa siku karibia na Jumapili ya Pasaka, zingatia kulenga kujifunza kwako maandiko kibinafsi na kifamilia kwenye ushuhuda wa nguvu wa Kitabu cha Mormoni kuhusu maisha, kifo, Ufufuo, na nguvu za upatanisho wa Yesu Kristo.
Andika Misukumo Yako
Mitume wa kale walikuwa majasiri katika shuhuda zao juu ya Yesu Kristo na Ufufuo Wake. Mamilioni wanaamini katika Yesu Kristo na wanajitahidi kumfuata Yeye kwa sababu ya maneno yao yaliyoandikwa katika Biblia. Lakini wengine huenda wakashangaa, kama Yesu Kristo ni Mwokozi wa dunia nzima, basi ni kwa nini mashahidi Wake waliomuona kwa macho ni watu wachache tu ambao wamekusanyika pamoja katika eneo moja dogo?
Kitabu cha Mormoni kinasimama kama shahidi mwingine, wa kuaminika kwamba Yesu Kristo ndiye Mwokozi wa dunia, “anayejidhihirisha kwa mataifa yote” (ukurasa wa Jina wa Kitabu cha Mormoni) na kutoa wokovu kwa wale wote wanaokuja Kwake. Kando na hilo, ushahidi huu wa pili pia unaweka wazi maana ya wokovu. Hii ndiyo sababu Nefi, Yakobo, Mormoni, na manabii wote walifanya kazi “kwa bidii kuchora maneno haya kwenye bamba”—kutangaza kwa vizazi vya siku zijazo kwamba wao pia “walijua kuhusu Kristo, na … walikuwa na tumaini la utukufu Wake” (Yakobo 4:3–4). Msimu huu wa Pasaka, tafakari kuhusu shuhuda zilizoko katika Kitabu cha Mormoni kwamba nguvu za Upatanisho wa Kristo ni kwa watu wote na kwa mtu binafsi—kukomboa ulimwengu wote na kukukomboa wewe.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
2 Nefi 9:6–15, 22; Alma 11:41–45; 40:21–23; 3 Nefi 26:4–5
Kwa sababu ya Ufufuo wa Yesu Kristo, watu wote watafufuliwa.
Ni desturi wakati wa Pasaka kutafakari Ufufuo wa Yesu Kristo, lakini inamaanisha nini hasa kufufuliwa? Ni umaizi gani unatolewa na Kitabu cha Mormoni kuhusu ufufuo? Pengine kama sehemu ya maadhimisho yako ya Pasaka ungeweza kuorodhesha kweli kuhusu ufufuo ambazo unazipata katika 2 Nefi 9:6–15, 22; Alma 11:41–45; 40:21–23; na 3 Nefi 26:4–5. Unaweza kuandika pia ni kwa nini unafikiria ni muhimu kujua kila moja ya kweli hizi.
Unaweza ukagundua ya kwamba kweli kuhusu ufufuo mara nyingi hufunzwa pamoja na kweli kuhusu Hukumu ya Mwisho. Tafakari kile ambacho hili linakufundisha kuhusu umuhimu wa Ufufuo katika mpango wa Wokovu.
Ona Pia Luka 24:36–43; Matendo ya Mitume 24:15; 1 Wakorintho 15:12–23.
Mosia 3:7; 15:5–9; Alma 7:11–13
Yesu Kristo alijichukulia juu Yake dhambi zangu, maumivu, na unyonge.
Biblia inafundisha wazi ya kwamba Yesu Kristo alifanya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu. Kitabu cha Mormoni, hata hivyo, kinapanua uelewa wetu kuhusu dhabihu na mateso ya Yesu Kristo katika njia muhimu. Unaweza kupata baadhi ya mafunzo haya katika Mosia 3:7; 15:5–9; na Alma 7:11–13. Baada ya kusoma vifungu hivi, zingatia kuandika kile ambacho umegundua katika chati kama hii:
Mwokozi aliteseka nini? |
Kwa nini aliteseka? |
Hii ina maana gani kwangu? |
---|---|---|
Mwokozi aliteseka nini? | Kwa nini aliteseka? | Hii ina maana gani kwangu? |
Ona pia Isaya 53; Waebrania 4:14–16.
Mosia 5:1–2; 27:8–28; Alma 15:3–12; 24:7–19
Upatanisho wa Yesu Kristo unanisafisha na kunisaidia kuwa mkamilifu.
Inaweza kusemekana ya kwamba Kitabu cha Mormoni kwa kiasi kikubwa ni historia ya watu ambao walibadilika kwa sababu ya Upatanisho wa Yesu Kristo. Kwa kweli, baadhi ya watu hao walitenda dhambi za kuhuzunisha na walikuwa maadui wa watu wa Mungu kabla ya nguvu za Mwokozi kusababisha mabadiliko makuu ndani yao kulingana na imani yao Kwake. Unaweza kusoma baadhi ya matukio haya katika Mosia 5:1–2; 27:8–28; na Alma 15:3–12; 24:7–19; pia unaweza ukafikiria kuhusu mifano mingine ya kujifunza. Ni kipi unachoona kwamba kila moja ya matukio haya yanacho cha kufanana? Umegundua tofauti zipi? Je, ni nini historia hizi zinakufundisha kuhusu jinsi Upatanisho wa Mwokozi unavyoweza kukubadilisha?
Ona Pia Alma 5:6–14; 13:11–12; 18; 19:1–16; 22:1–26; 36:16–21; Etheri 12:27; Moroni 10:32–33.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani
Unaposherehekea Pasaka pamoja na familia yako, tafuta njia ambazo mnaweza kujifunza pamoja kuhusu Mwokozi na Upatanisho Wake, pamoja na Ufufuo. Haya ni baadhi ya mawazo.
3 Nefi 11; 17
Baadhi ya familia zimegundua ya kwamba kujifunza historia ya huduma ya Mwokozi mfufuka katika bara za Amerika ni muhimu zaidi wakati wa msimu wa Pasaka. Wahimize wanafamilia kufikiria jinsi ambavyo ingekuwa kugusa makovu Yake (ona 3 Nefi 11:14–15) au kuwa mmoja kati ya wale watoto aliowabariki (ona 3 Nefi 17:21). Je, ni jinsi gani historia hii inafanya shukrani zetu kwa ajili ya Ufufuo wa Mwokozi kuwa za kina? Mchoro ambao unaonyesha historia hii unaambatana na muhtasari huu; mingine yaweza kupatikana kwenye ChurchofJesusChrist.org. Wanafamilia wako pia wanaweza kufurahia kuchora picha zao wenyewe kuhusu kile wanachosoma.
Jumbe kutoka mkutano mkuu
Katika maeneo mengi ya dunia, mkutano mkuu wa Aprili mwaka huu utafanyika wikiendi ya kabla ya Pasaka. Pengine kusikiliza jumbe kutoka kwenye mkutano kunaweza kuisaidia familia yako kufokasi kwa Mwokozi Pasaka hii. Kwa mfano, unaweza ukawaalika wanafamilia kusikiliza ili kutambua jumbe za mkutano ambazo zinatoa ushuhuda juu ya Yesu Kristo na Ufufuo Wake—hasa kutoka kwa Mitume, ambao ni mashahidi maalum wa Yesu Kristo. Kisha mnaweza kufanya mapitio ya jumbe hizi pamoja na kutambua mafundisho ambayo yanaimarisha shuhuda zenu juu ya Mwokozi.
“Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume”
Kama familia, someni “Kristo Aliye Hai: Ushuhuda wa Mitume” (Ensign au Liahona, Mei 2017, ndani ya jalada la upande wa mbele; ona pia ChurchofJesusChrist.org) na mualike kila mwanafamilia kuchagua ujumbe mmoja wa Pasaka kutoka kwenye ushuhuda huu ili ashiriki na wengine. Kwa mfano, unaweza kutengeneza mabango ya kuweka kwenye mtandao wa kijamii, juu ya mlango wako wa mbele, au dirishani kwako.
Video: Mashahidi Maalum wa Kristo
ChurchofJesusChrist.org na Gospel Library app zina mfuatano wa video unaoitwa Mashahidi Maalum wa Kristo. Unajumuisha video za kila mshiriki wa Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wakitoa ushuhuda wao juu ya Yesu Kristo. Familia yako inaweza kutazama moja au zaidi ya video hizi na kujadiliana kile ambacho zinatufundisha kuhusu kile ambacho Mwokozi amefanya kwa ajili Yetu.
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.