Njoo, Unifuate
Machi 23–29. Enoshi–Maneno ya Mormoni: Anafanya Kazi Ndani Yangu Ili Nitende Kulingana na Nia Yake


“Machi 23–29. Enoshi–Maneno ya Mormoni: Anafanya Kazi Ndani Yangu Ili Nitende Kulingana na Nia Yake,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Machi 23–29. Enoshi–Maneno ya Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2020

Picha
Enoshi akiwa kijana mdogo pamoja na baba yake, Yakobo, na mama yake

Yakobo na Enoshi, na Scott Snow

Machi 23–29

EnoshiManeno ya Mormoni

Anafanya Kazi Ndani Yangu Ili Nitende Kulingana na Nia Yake

Unaposoma Enoshi mpaka Maneno ya Mormoni, tafuta jumbe ambazo zitakuwa za manufaa kwako au kwa familia yako.

Andika Misukumo Yako

Enoshi alienda porini kuwinda wanyama, lakini alijikuta amebakia huko akisali “kwa siku nzima … na wakati wa usiku ulipofika” (Enoshi 1:3–4). Kwa sababu nafsi yake kwa kweli ilipata njaa ya kupokea msamaha wa dhambi zake, Enoshi alikuwa tayari kusali kwa muda wote ambao ingehitajika na hata kuwa na “mweleka” mbele ya Mungu (Enoshi 1:2). Hii ndiyo sala ya dhati: sio tu kuomba kile tunachohitaji lakini juhudi za dhati kuwasiliana na Mungu na kulinganisha mapenzi yetu na Yake. Wakati unaposali kwa jinsi hii, wakati sauti yako “imefika mbinguni,” unagundua jinsi alivyogundua Enoshi kwamba Mungu anakusikia, na kwa kweli anakujali, wapendwa wako, na hata maadui zako (ona Enoshi 1:4–17). Katika nyakati hizo, Mungu anaweza kukufahamisha mapenzi Yake, na utakuwa radhi na mwenye uwezo wa kutenda mapenzi Yake kwa sababu una upatanifu na Yeye. Kama Mormoni, unaweza “usijue mambo yote; lakini Bwana anajua vitu vyote … [na] anafanya kazi ndani [yako] ili utende kulingana na nia yake” (Maneno ya Mormoni 1:7).

Picha
ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Enoshi 1:1–3

Maneno ya mzazi yanaweza kuwa na ushawishi mkubwa sana.

Ni jumbe gani zipo katika mistari hii kwa ajili ya wazazi na watoto?

Enoshi 1:4–27

Sala zangu za dhati zitajibiwa.

Uzoefu wa Enoshi kwenye sala ni mojawapo ya tukio la kukumbukwa zaidi katika maandiko. Uzoefu wako huenda usiwe wa ajabu, lakini haufai kuwa wenye maana kidogo. Uzoefu wa Enoshi unaweza kuonyesha njia za kuboresha sala zako. Haya ni baadhi ya maswali ya kutafakari:

  • Ni maneno gani yanaelezea juhudi za Enoshi alipokuwa akisali?

  • Hapo awali Enoshi alisali kwa ajili ya nini? (ona Enoshi 1:4). Unaweza kujifunza nini kutokana na majibu ya Enoshi baada ya kupokea jibu? (ona Enoshi 1:5–7).

  • Ni jinsi gani Enoshi alitenda kulingana na majibu aliyopokea?

  • Unaweza kujifunza nini kutoka kwa Enoshi kuhusu jinsi ya kuwa na imani “isiyotingishika” katika Bwana? (Enoshi 1:11).

YaromuOmni

Bwana atanibariki ninaposhika amri Zake.

Mojawapo ya ahadi za Mungu iliyorudiwa sana katika Kitabu cha Mormoni ni kwamba kama Wanefi wangeshika amri, wangefanikiwa (ona 2 Nefi 1:20; Yaromu 1:9–12; Omni 1:6). Vitabu vya Yaromu na Omni vinaonyesha baadhi ya njia ambazo ahadi hii ilitimizwa. Unajifunza nini kutokana na historia hizi ambacho kitakusaidia “kufanikiwa katika nchi”?

Omni 1:14, 21

Watu wa Zarahemla walikuwa ni kina nani?

Baada ya Wanefi kutoroka nchi ya Nefi, waligundua watu wengi wakiishi mahali palipoitwa Zarahemla. Watu wa Zarahemla walikuwa wa uzao wa kundi la Waisraeli ambao, kama familia ya Lehi, walikuwa wametoka Yerusalemu na waliongozwa na Mungu hadi katika nchi ya ahadi. Miongoni mwa kikundi hicho alikuwa ni Muleki, mmoja wa wana wa Zedekia, mfalme wa Yuda ambaye alishikwa na Wababiloni takriban mwaka wa 587 Kabla ya Kuzaliwa kwa Kristo (ona Yeremia 52:1–11; Mosia 25:2; Helamani 8:21).

Baada ya watu wa Zarahemla kuwasili katika nchi ya Ahadi, walikutana na Koriantumuri (ona Omni 1:21), nusura wa Wayaredi ambaye ni wa mwisho kujulikana, ambaye hadithi yake inasimuliwa katika kitabu cha Etheri.

Maneno ya Mormoni

Ni nini Maneno ya Mormoni?

Maneno ya Mormoni ni ufupisho kati ya seti mbili za bamba ambazo kwa pamoja zinakuwa Kitabu cha Mormoni. Hapa Mormoni anatoa maelezo juu ya kumbukumbu hizi mbili, na maneno Yake yanafundisha ujumbe muhimu kuhusu kumwamini Bwana, hata wakati ambapo hatuelewi kikamilifu maagizo Yake.

Nefi alipokuwa akiandika kumbukumbu ya watu wake, Mungu alimuongoza kutengeneza seti mbili za bamba, zilizojulikana kama bamba ndogo na bamba kubwa za Nefi. Nefi hakuelewa ni kwa nini aliamuriwa kutengeneza seti mbili za bamba, lakini aliamini kwamba Bwana alikuwa na “kusudi lenye hekima … , ambalo kusudi mimi silijui” (1 Nefi 9:5; ona pia “Maelezo Mafupi Kuhusu Kitabu cha Mormoni”).

Karne nyingi baadaye, Mormoni alipokuwa akifupisha bamba kubwa za Nefi, aligundua zile bamba ndogo. Bamba ndogo zilijumuisha matukio mengi sawa na yale yaliyoelezewa katika zile bamba kubwa ambazo Mormoni alikuwa tayari amefupisha, lakini zile bamba ndogo zililenga hasa zaidi maswala ya kiroho na huduma na mafundisho ya manabii. Mungu alimtia msukumo Mormoni ajumuishe zile bamba ndogo za Nefi katika kumbukumbu yake ikiwa ni pamoja na zile bamba kubwa. Kama Nefi, Mormoni hakuelewa kusudi la Mungu la kutaka kuwa na seti zote mbili za bamba, lakini aliamini kwamba lilikuwa kwa “madhumuni ya busara” (Maneno ya Mormoni 1:7).

Leo tunajua ni nini lilikuwa lengo la Mungu. Mnamo mwaka wa 1828 baada ya Joseph Smith kutafsiri sehemu ya ufupisho wa bamba kubwa za Nefi (kurasa 116 za muswada), Martin Harris alipoteza kurasa hizo. Mungu alimuamuru Joseph kwamba asitafsiri tena sehemu hii kwa sababu watu waovu wangebadilisha maneno yale na kujaribu kumtia fedheha Joseph (ona M&M 10, kichwa cha habari cha sehemu; M&M 10:14–19, 30–45). Kwa shukrani, Mungu alikuwa amelijua hili na akatoa zile bamba ndogo, ambazo zilijumuisha historia ile iliyokuwa imepotea pamoja na zile kurasa 116 . Zile bamba ndogo zinajumuisha vitabu vinavyokuja kabla ya Maneno ya Mormoni, na ufupisho wa Mormoni wa zile bamba kubwa unaanza baada ya Maneno ya Mormoni.

Picha
Mormoni akiziunganisha bamba za dhahabu

Mormoni Akiziunganisha Bamba, na Jorge Cocco

Picha
ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Unaposoma maandiko na familia yako, Roho anaweza kukusaidia kujua kanuni zipi zisisitizwe na kujadiliwa ili kukidhi mahitaji ya familia yako. Haya ni baadhi ya mawazo.

Enoshi 1:1–17

Familia yako inaweza kutazama picha ya Enoshi akisali na wasome Enoshi 1:1–17 kwa ajili ya virai vinavyoweza kutumika kama vichwa vya habari vya picha hii. Unaweza pia kuwaomba wanafamilia wachore picha za uzoefu wa Enoshi. Ni nini tunajifunza kutoka kwa Enoshi kuhusu kutafuta msamaha?

Yaromu 1:2

Ni jinsi gani kujifunza kwetu Kitabu cha Mormoni “kumefunua kuhusu mpango wa wokovu” kwetu sisi?

Omni 1:12–22

Mistari hii inafundisha nini kuhusu umuhimu wa kuwa na neno la Mungu katika maisha yetu?

Maneno ya Mormoni 1:3–9

Tutabarikiwa kwa namna gani kwa kuweka kumbukumbu za kibinafsi na za familia? Ni jinsi gani tunaweza kufanya kumbukumbu zetu zifokasi zaidi kwa Kristo?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kufundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kusanyikeni pamoja mara kwa mara. Rais Henry B. Eyring alifundisha: “Kamwe usipoteze nafasi ya kuwakusanya watoto pamoja ili kujifunza mafundisho ya injili ya Yesu Kristo. Nyakati kama hizo ni chache sana ikilinganishwa na juhudi za adui” (“Nguvu ya Kufundisha Injili,” Ensign, Mei 1999, 74).

Picha
Enoshi akisali

Enoshi akisali, na Robert T. Barrett

Chapisha