Njoo, Unifuate
Machi 23–29. Enoshi–maneno ya Mormoni: Anafanya kazi ndani yangu ili nitende kulingana na nia Yake


“Machi 23–29. Enoshi–maneno ya Mormoni: Anafanya kazi ndani yangu ili nitende kulingana na nia Yake,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Kitabu cha Mormoni 2020 (2020)

“Machi 23–29. Enoshi–maneno ya Mormoni,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2020

Picha
Enoshi kama kijana mdogo akiwa na baba yake, Yakobo na mama yake

Yakobo na Enoshi, na Scott Snow

Machi 23–29

EnoshiManeno ya Mormoni

Anafanya kazi ndani yangu ili nitende kulingana na nia Yake

Enoshi, Yaromu, Omni, na Maneno ya Mormoni ni vitabu vifupi ambavyo vina mafunzo yenye thamani kwa watoto unaowafundisha. Tafuta mafunzo haya, na tafakari njia za kuwasaidia watoto kujifunza kuyahusu. Mawazo yaliyoko katika muhtasari huu yanaweza kusaidia.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Wasaidie watoto kukumbuka kile walichojifunza kutoka somo la wiki iliyopita. Je, walishiriki kile walichojifunza pamoja na familia zao au wengine?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Enoshi 1:1–19

Ninaweza kuzungumza na Baba wa Mbinguni kupitia sala.

Uzoefu wa Enoshi hufundisha kweli kadhaa kuhusu sala. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto kufuata mfano wa Enoshi pale wanaposali?

Shughuli za Yakini

  • Onyesha picha ya Enoshi; kwa mfano, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, ), au tumia picha Enoshi akisali (Kitabu cha Sanaa za Injili, na. 72). Waombe watoto wazungumze kuhusu kile kinachofanyika kwenye picha, na kisha shiriki uzoefu wa Enoshi pamoja nao. Ungeweza kutumia “Sura ya 11: Enoshi” (Hadithi za Kitabu cha Mormoni, 30–31, au video inayohusiana katika ChurchofJesusChrist.org).

  • Waombe watoto kushiriki mambo wanayopenda kuyazungumzia wakiwa na wazazi wao. Elezea kwamba kusali kwa Baba wa Mbinguni ndiyo jinsi wanavyoweza kuzungumza Naye. Unaposoma Enoshi 1:1–4 kwa watoto, waalike kujifanya kuwa Enoshi kwa kuigiza kuwinda, kupiga magoti kusali, na kadhalika. Eleza kuwa Baba wa Mbinguni alisikia sala ya Enoshi na kumsamehe dhambi zake.

  • Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu sala, kama vile “A Child’s Prayer” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12–13). Waalike watoto wainue mikono yao kila mara wanaposikia neno “sala” au neno lingine linalojirudia. Shuhudia juu ya nguvu ya sala katika maisha yako.

Picha
familia ikisali

Kama watoto wa Mungu, tunaweza kusali kwa Baba yetu wa Mbinguni.

Maneno ya Mormoni 1:3–8

Ninaweza kuwabariki wengine wakati ninapomsikiliza Roho Mtakatifu.

Alipokuwa akikusanya pamoja Kitabu cha Mormoni, Mormoni alishawishiwa kujumuisha bamba ndogo za Nefi. Hakujua kwa nini bamba ndogo zilihitajika, lakini leo tumebarikiwa kwa sababu alifuata ushawishi huu. Mfano huu unaweza kuwashawishi watoto kumfuata Roho.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kushiriki hadithi walizojifunza kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni mpaka sasa kwa mwaka huu (picha kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia au Kitabu cha Sanaa za Injili vinaweza kuwasaidia kukumbuka). Elezea kwamba tuna hadithi hizi kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni kwa sababu Mormoni alisikiliza wakati Roho Mtakatifu alipomwambia kuzijumuisha. Je, ni kwa nini Baba wa Mbinguni anataka sisi tuwe na hadithi hizi?

  • Shiriki hadithi kutoka kwenye magazeti ya Kanisa au kutoka kwenye ujumbe wa mkutano mkuu kuhusu mtu aliyefuata ushawishi wa Roho Mtakatifu. Au shiriki moja ya uzoefu wako mwenyewe. Waalike wanafunzi kuchora picha za hadithi. Ni kwa jinsi gani watu katika hadithi hizi walibarikiwa kwa sababu walimfuata Roho Mtakatifu?

  • Muombe muumini wa kata kutembelea darasa na kushiriki uzoefu wakati alipofuata ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ni kwa jinsi gani matendo yake yaliwabariki wengine? Elezea kwamba Baba wa Mbinguni anatutaka sisi kuwasaidia na kuwabariki wengine, kwa hivyo Yeye humtuma Roho Mtakatifu kutuongoza.

  • Imbeni kwa pamoja wimbo kuhusu Roho Mtakatifu, kama vile “The Still Small Voice” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 106–7 ). Imbeni mara kadhaa katika njia tofauti, kama vile haraka, taratibu, au kwa kunong’ona. Wakati mkinong’ona wimbo, fungua Maneno ya Mormoni 1:7, na onyesha kwamba Mormoni alimuelezea Roho Mtakatifu kama mnong’ono.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Enoshi 1:1–19

Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zangu.

Inaweza kuwa rahisi kwa sala zetu kuwa desturi au kawaida. Uzoefu wa Enoshi ni ukumbusho kwamba kupokea majibu ya sala zetu wakati mwingine huitaji “mweleka” na “vilio vingi” (Enoshi 1:2, 11).

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kufumba macho na kufikiria wanazungumza na Baba wa Mbinguni ana kwa ana. Ni nini wangependa kuzungumzia pamoja Naye? Waalike watoto kufikiria kuhusu kuzungumza uso kwa uso na Baba wa Mbinguni kila mara wanaposali.

  • Waalike watoto kufanya kazi katika jozi na kusoma Enoshi 1:1–5. Waombe kutafuta mistari hii kupata neno au kifungu cha maneno ambacho kinaelezea sala za Enoshi na kisha kushiriki kile wanachopata pamoja na darasa. Je! maneno haya hupendekeza nini kuhusu Enoshi na uzoefu wake? Acha watoto washiriki jambo lingine lolote ambalo limewavutia kuhusu sala za Enoshi. Shiriki uzoefu ambapo nafsi yako “ilipata njaa” na wewe “ukamlilia” Bwana (Enoshi 1:4). Waruhusu watoto kutafakari jambo moja wanaloweza kutenda kufanya sala zao ziwe na maana zaidi.

  • Waombe watoto kuorodhesha baadhi ya mambo ambayo hasa wanayaombea, aidha ubaoni au kwenye ukurasa wa shughuli ya wiki hii. Kisha waalike kupekua Enoshi 1:2, 9, 13–14, na 16 kwa ajili ya mambo Enoshi aliyoyaombea, na ongeza mambo hayo kwenye orodha. Jadili ni kwa jinsi gani watoto wanaweza kufuata mfano wa Enoshi katika sala zao; kwa mfano, unaweza kuongelea kuhusu kwa nini Enoshi alikuwa tayari kusali kwa ajili ya Walamani—ambao walikuwa adui zake—na waalike watoto kusali wiki hii kwa ajili ya mtu ambaye amekuwa si mkarimu kwao.

Maneno ya Mormoni 1:3–8

Ninaweza kuwabariki wengine wakati ninapomsikiliza Roho Mtakatifu.

Bwana alijua kwamba kurasa 116 zilizotafsiriwa mwanzo za Kitabu cha Mormoni zingepotea (ona M&M 10; Watakatifu, toleo la 1, sura ya 5). Kufidia upotevu huu, Yeye alimshawishi Mormoni kupitia Roho kujumuisha bamba ndogo za Nefi katika Kitabu cha Mormoni. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi watoto kufuata mfano wa Mormoni na kumsikiliza Roho?

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto kufanya zamu kusoma mistari kutoka Maneno ya Mormoni 1:3–8 mmoja baada ya mwingine, na kisha wasaidie kufupisha kile walichojifunza kutoka kwenye kila mstari. Elezea kwamba Mormoni alimfuata Roho kwa kujumuisha bamba ndogo za Nefi (ambazo tunazo sasa kama 1 Nefi mpaka Omni) ndani ya Kitabu cha Mormoni. Ni kwa jinsi gani tunabarikiwa kwa sababu Mormoni alimsikiliza Roho? Ni kwa jinsi gani Kitabu cha Mormoni kingekuwa tofauti kama asingesikiliza? Shiriki uzoefu ambapo wewe ulishawishiwa na Roho Mtakatifu kufanya jambo ambalo lilimbariki mtu fulani. Waalike watoto kushiriki uzoefu kama huo wanaoweza kuwa nao.

  • Mwalike mtoto mmoja asome Maneno ya Mormoni 1:7 na mwingine asome Mafundisho na Maagano 8:2–3. Ni nini mistari hii hufundisha kuhusu jinsi Roho Mtakatifu anavyozungumza nasi? Wasaidie watoto kutambua nyakati ambazo wamehisi ushawishi kutoka kwa Roho Mtakatifu. Tumia Moroni 7:12 kuelezea kwamba kama wazo ni zuri na linatushawishi kufanya mambo mema, linatoka kwa Baba wa Mbinguni. Kwa mfano, fikiria kuonyesha video “Maandalizi ya Thomas S. Monson: Daima Fuata Ushawishi wa Roho” (ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto kusikiliza ushawishi wa kutenda mema na kuufuata.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Wahimize watoto kuwaomba wanafamilia wao kushiriki uzoefu waliopata kutokana na sala au Roho Mtakatifu.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki. Nyimbo za msingi na nyimbo za dini zinaweza kuwasaidia watoto wa rika zote kuelewa na kukumbuka kweli za injili. Kuimba kunaweza pia kuwafanya watoto washiriki kikamilifu katika uzoefu wa kujifunza. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 22.)

Chapisha