Hadithi za Maandiko
Sura ya 11: Enoshi


Sura ya 11

Enoshi

Yakobo akimpa Enoshi bamba

Enoshi alikuwa mwana wa Yakobo. Alizihifadhi bamba na kuandika ndani yake baada ya baba yake kufariki.

Enoshi akiwinda

Siku moja Enoshi alikuwa akiwinda ndani ya msitu. Alifikiria kuhusu mafundisho ya baba yake na akataka msamaha wa dhambi zake.

Enoshi akisali

Enoshi alipiga magoti na kusali kwa Mungu. Alisali siku nzima na alikuwa angali anasali usiku ulipofika.

Enoshi akisali

Mungu alimwambia Enoshi kwamba kwa sababu ya imani yake katika Yesu Kristo, dhambi zake zilikuwa zimesamehewa.

Enoshi akisali

Kisha Enoshi alitaka Bwana awabariki Wanefi. Alisali kwa niaba yao, na Bwana akasema angewabariki ikiwa wangetii amri zake.

Walamani

Enoshi pia alitaka Bwana awabariki Walamani. Alisali kwa imani kubwa, na Bwana aliahidi kufanya kile ambacho Enoshi alimuomba.

Walamani wakipigana na Wanefi

Ingawaje Walamani walipigana na Wanefi na kujaribu kuharibu kumbukumbu zao, Enoshi alisali kwamba wangekuja kuwa watu wenye haki.

Enoshi akisali

Enoshi alisali kwamba kumbukumbu alizokuwa ameweka zingelindwa. Bwana aliahidi kwamba siku moja angewapa Walamani mafundisho ambayo yalikuwa katika kumbukumbu.

Enoshi akiwahubiria Wanefi

Enoshi aliwahubiria Wanefi. Aliwataka wamwamini Mungu na kutii amri.

Walamani wakifanya kazi

Wanefi walijaribu kuwafundisha Walamani injili, lakini hawakuwasikiliza. Walamani waliwachukia Wanefi.

Enoshi akiandika

Enoshi alitumia maisha yake kuwafundisha watu kuhusu Yesu na injili. Alimtumikia Mungu na kumpenda siku zake zote.