Sura ya 34 Helamani na Vijana Mashujaa 2000 Watu wa Amoni walikuwa wamemuahidi Mungu kwamba hawangepigana tena. Waliishi karibu na Wanefi, na Wanefi waliwalinda. Alma 53:10–12 Wakati maadui wa watu wa Amoni walipowashambulia Wanefi, watu wa Amoni walitaka kuvunja ahadi yao na kuwasaidia Wanefi. Alma 53:13 Helamani na viongozi wengine wa Wanefi hawakutaka watu wa Amoni kuvunja ahadi yao kwa Mungu. Alma 53:14–15 Vijana wadogo wa watu wa Amoni walikuwa hawajaweka ahadi. Walitaka kulisaidia jeshi la Wanefi kupigania uhuru. Alma 53:16–17 Elfu mbili kati ya hao vijana walichagua kuilinda nchi yao. Walimuomba Helamani kuwa kiongozi wao. Alma 53:18–19 Vijana hawa walikuwa thabiti, mashujaa na wenye nguvu. Pia walikuwa wakweli na wa kuaminika, na walitii amri za Mungu. Alma 53:20–21 Helamani aliongoza vijana mashujaa 2000 kwenye vita. Aliwaita wanawe, na wao walimwita baba yao. Alma 53:22; 56:46 Ingawa wana wa Helamani hawakuwa wamewahi kupigana vita, hawakuogopa. Mama zao waliwafundisha kuwa na imani katika Mungu na kujua kwamba angewasaidia. Alma 56:47 Helamani na jeshi lake walipigana vita kadhaa dhidi ya Walamani. Vijana hawa walitii yote Helamani aliyoamrisha. Alma 57:19–21 Walipigana kwa ushujaa na walisaidia kumfukuza adui. Baada ya vita Helamani alikuta kwamba wana wake wote walikuwa wamejeruhiwa lakini hakuna aliyekuwa ameuwawa. Alma 57:22, 25 Ilikuwa ni muujiza. Helamani alifurahi sana. Alijua kwamba vijana hawa walikuwa wamelindwa kwa sababu ya imani yao kubwa katika Mungu. Alma 57:26–27