Sura ya 18 Alma Mdogo Anatubu Mfalme Mosia alimteua Alma kuwa kiongozi wa Kanisa kule Zarahemla. Alma kisha akawachagua watu wengine kumsaidia kuwafundisha Wanefi. Mosia 25:19; 26:8 Alma na Mfalme Mosia walikuwa na wasi wasi kwa sababu wasioamini walikuwa wakisababisha mateso kwa waumini wa Kanisa kwa sababu ya imani yao. Mosiah 27:1 Alma alikuwa na mwana wa kiume aliyeitwa Alma. Alma Mdogo hakuamini mafundisho ya baba yake na akawa mtu muovu. Mosia 27:8 Alma Mdogo na wana wanne wa Mfalme Mosia walipigana dhidi ya Kanisa. Waliwashawishi watu wengi kuacha Kanisa na kuwa waovu. Mosia 27:8 Alma alisali kwamba mwanawe angejua ukweli na kutubu. Mosia 27:14 Alma Mdogo na wana wa Mfalme Mosia waliendelea kujaribu kuliangamiza Kanisa. Mosia 27:10 Siku moja malaika aliwatokea. Malaika alizungumza kwa sauti kubwa ambayo ilitetemesha ardhi. Mosia 27:11 Wavulana hao watano walikuwa na hofu kiasi kwamba walianguka chini. Mara ya kwanza hawakuelewa kile malaika alichokuwa akisema. Mosia 27:12 Malaika alikuwa amekuja kujibu sala za waumini wa Kanisa. Malaika alimwuliza Alma Mdogo sababu ya kupigana dhidi ya Kanisa. Mosia 27:13–14 Ardhi ilitetemeka malaika alipokuwa akimwambia Alma mdogo akome kuangamiza Kanisa. Mosia 27:15–16 Alma Mdogo na wana wa Mosia walianguka chini tena. Walikuwa wamemwona malaika, na walijua uwezo wa Mungu ulikuwa umetetemesha ardhi. Mosia 27:18 Alma Mdogo alistaajabu kiasi cha kutoweza kuzungumza. Akawa mnyonge hata kwamba hakuweza kunyosha mikono yake. Mosia 27:19 Wana wa Mosia walimbeba Alma Mdogo kumpeleka kwa baba yake na kumwelezea kilichokuwa kimetokea kwao. Mosia 27:19–20 Alma alikuwa na furaha. Alijua ya kwamba Mungu alikuwa amejibu sala zake. Mosia 27:20 Alma aliwaita watu wengi pamoja ili washuhudie yale ambayo Bwana alikuwa amemtendea mwana wake na wana wa Mosia. Mosia 27:21 Alma, pamoja na viongozi wengine wa Kanisa, walifunga na kusali na kumwomba Mungu amsaidie Alma Mdogo apate nguvu tena. Mosia 27:22 Baada ya siku mbili kuchwa na kucha, Alma Mdogo aliweza kuongea na kusimama. Mosia 27:23 Aliwaambia watu kwamba alikuwa ametubu dhambi zake na Mungu alikuwa amemsamehe. Mosia 27:24 Alifundisha kwamba kila mtu ni lazima awe mwenye haki ili aweze kuingia katika ufalme wa Mungu. Pia alielezea kuhusu uchungu mkubwa alioteseka kwa ajili ya dhambi zake. Mosia 27:25–26, 29 Alma Mdogo alikuwa na furaha kwa sababu alikuwa ametubu na Mungu alikuwa amemsamehe. Alijua Mungu Alimpenda. Mosia 27:28 Alma Mdogo na wana wa Mosia walianza kufundisha ukweli kote nchini, wakimwambia kila mtu yale waliyokuwa wameona na kusikia. Mosia 27:32 Walijaribu kurekebisha makosa waliyokuwa wamefanya. Waliwafafanulia watu maandiko na kuwafundisha kuhusu Yesu Kristo. Mosia 27:35 Mungu aliwabariki Alma Mdogo na wana wa Mosia walipokuwa wakifundisha injili. Watu wengi waliwasikiliza na wakaamini. Mosia 27:36