Scripture Stories
Sura ya 2: Lehi Anawaonya Watu


Sura ya 2

Lehi Anawaonya Watu

Picha
nabii anafundisha

Wengi kati ya watu waliokuwa wakiishi Yerusalemu miaka 600 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo walikuwa waovu. Mungu aliwatuma manabii wawaambie watubu, lakini hawakutaka kusikiliza.

Picha
Lehi na nguzo ya moto

Lehi alikuwa nabii. Alisali ili watu watubu. Alipokuwa akisali, nguzo ya moto ilitokea. Mungu alimwambia na kumwonyesha Lehi vitu vingi.

Picha
Lehi akiona ono

Lehi alirudi nyumbani na akapata ono. Alimwona Mungu akiwa amezungukwa na malaika wengi. Malaika walikuwa wakiimba na kumsifu Mungu.

Picha
Ono la Lehi

Katika ono lake Lehi alipewa kitabu kilichozungumzia kitu ambacho kingetokea katika siku zijazo. Alisoma kwamba Yerusalemu ingeangamizwa kwa sababu watu walikuwa waovu.

Picha
Lehi akizungumza na watu

Lehi aliwaambia watu kwamba Yerusalemu itaangamizwa. Pia alizungumza kuhusu ujio wa Yesu. Watu walikuwa na hasira na walijaribu kumuua Lehi, lakini Bwana alimkinga.

Chapisha