Sura ya 21 Waamlisi Amlisi alikuwa mtu mjanja, na mwovu ambaye alitaka kuwa mfalme wa Wanefi. Alikuwa na wafuasi wengi. Alma 2:1–2 Wanefi wenye haki hawakumtaka Amlisi kuwa mfalme wao. Walijua alitaka kuliharibu Kanisa la Mungu. Alma 2:3–4 Wanefi walijikusanya katika makundi kuamua kama Amlisi angekuwa mfalme. Watu wengi walipiga kura kumpinga Amlisi, na hakuwa mfalme. Alma 2:5–7 Amlisi na wafuasi wake walikasirika. Walijitenga kutoka kwa Wanefi na wakamfanya Amlisi kuwa mfalme wao, na kujiita Waamlisi. Amlisi aliwaamrisha kupigana na Wanefi. Alma 2:8–11 Wanefi wenye haki walijiandaa kujilinda wao wenyewe kwa pinde na mishale, panga na silaha zingine. Alma 2:12 Waamlisi walivamia, na Wanefi, ambao walikuwa wakiongozwa na Alma na kuimarishwa na Bwana, waliwaua wengi wa Waamlisi. Waamlisi waliobaki walikimbia. Alma 2:15–19 Alma aliwatuma wapelelezi kuwatazama waamlisi. Wapelelezi waliwaona wakiungana na jeshi kubwa la Walamani na kuwavamia Wanefi walioishi Zarahemla. Alma 2:21, 24–25 Wanefi walisali, na Mungu aliwasaidia tena. Waliwaua wengi wa wanajeshi wa jeshi la Walamani–Waamlisi. Alma 2:28 Alma na Amlisi walipigana kwa panga. Alma alisali kwamba maisha yake yangelindwa, na Mungu alimpa nguvu za kumuua Amlisi. Alma 2:29–31 Wanefi waliwafukuzia Walamani na Waamlisi nyikani. Wengi wa waliojeruhiwa walikufa na waliliwa na wanyama wa mwituni. Alma 2:36–38 Kama walamani, Waamlisi walijichora kwa rangi nyekundu, kitu ambacho kilitimiza unabii. Waamlisi walikuwa wamejitenga wao wenyewe kutoka kwenye baraka za injili. Alma 3:4, 14, 18–19