Sura ya 47
Yesu Kristo Anawabariki Wanafunzi Wake
Siku moja wakati wanafunzi walikuwa kwa pamoja wamefunga na kusali, Yesu Kristo aliwajia.
Wanafunzi walimwuliza jina watakaloliita Kanisa. Yesu alisema kwamba liitwe kwa jina Lake kwa maana ni Kanisa Lake.
Yesu Kristo aliwaelezea wanafunzi Wake kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa amemtuma duniani kutoa uhai Wake kwa ajili ya watu wote.
Alisema kila mtu ambaye anatubu, anabatizwa katika jina Lake, na kutii amri Zake hatapatikana na hatia mbele za Baba wa Mbinguni.
Mwokozi aliwaambia wanafunzi wafanye vitu walivyokuwa wameona akifanya. Alikuwa amewapa mfano.
Pia aliwaambia waandike yale waliyokuwa wameyaona na kusikia ili wengine wajue kuyahusu.
Yesu aliwauliza wanafunzi Wake kitu walichohitaji kutoka Kwake. Tisa kati yao walitaka kuwa naye baada ya maisha yao duniani kukamilika.
Yesu aliwaahidi ya kwamba watakapofikisha umri wa miaka 72, wangejiunga naye mbinguni.
Wale wanafunzi wengine watatu hawakuthubutu kuuliza kile walichokitaka, lakini Yesu alijua. Walitaka kubaki duniani na kufundisha injili hadi Yesu atakaporudi tena.
Mwokozi aliwaahidi kwamba hawangepata maumivu ya kimwili au huzuni na hawangefariki. Wangewafudisha watu injili hadi atakaporudi.
Yesu alimgusa kila mwanafunzi isipokuwa wale watatu ambao wangebaki duniani. Kisha akaondoka.
Wale wanafunzi watatu walichukuliwa mbinguni, ambapo waliona na kusikia vitu vingi vya ajabu. Walikuwa na uwezo bora wa kuelewa vitu vya Mungu.
Miili yao iligeuzwa ili wasife.
Wanafunzi watatu walirudi duniani na kuanza kuhubiri na kubatiza.
Wanefi waovu waliwatupa wanafunzi watatu gerezani na katika mashimo yenye kina, lakini uwezo wa Mungu uliwawezesha kutoroka.
Wakati walipotupwa katika tanuu na mashimo pamoja na wanyama wa mwitu, walilindwa pia na uwezo wa Mungu.
Wale wanafunzi watatu waliendelea kuhubiri injili ya Yesu Kristo miongoni mwa Wanefi. Bado wanaendelea kuhubiri injili Yake.