Sura ya 3 Lehi Anaondoka Yerusalemu Bwana alipendezwa na Lehi na usiku mmoja alizungumza naye katika ndoto. Alimwambia Lehi kwamba achukuwe familia yake na aondoke Yerusalemu. Lehi alimtii Bwana. 1 Nefi 2:1–3 Familia ya Lehi walibeba chakula na mahema. Waliiacha nyumba yao na dhahabu na fedha na kusafiri nyikani. 1 Nefi 2:4 Lehi na mkewe, Saria, walikuwa na wana wanne. Majina yao yalikuwa Lamani, Lemueli, Samu, na Nefi. 1 Nefi 2:5 Baada ya kusafiri kwa siku tatu, familia ya Lehi iliweka kambi bondeni karibu na mto. 1 Nefi 2:6 Lehi alijenga madhabahu ya mawe na kutoa sadaka kwa Mungu. Alimshukuru Mungu kwa kuiokoa familia yake kutoangamizwa. 1 Nefi 2:7 Lehi aliupa mto jina Lamani na akaliita bonde Lemueli. Lehi aliwataka wanawe wawe kama mto na bonde, daima ukitiririka kwa Mungu na imara kutii amri. 1 Nefi 2:8–10, 14 Lamani na Lemueli walidhani baba yao alikuwa mpumbavu kwa kuondoka Yerusalemu na kuacha mali yao. Hawakuamini ya kwamba Yerusalemu itaangamizwa. 1 Nefi 2:11, 13 Nefi alitaka kuelewa vitu ambavyo Lehi alikuwa ameviona. Alisali ili ajue kama baba yake alikuwa amefanya jambo zuri kuondoka Yerusalemu. 1 Nefi 2:16 Yesu Kristo alimtokea Nefi na kumweleza kwamba maneno ya Lehi yalikuwa ya kweli. Nefi aliamini na hakukaidi kama Lamani na Lemueli walivyofanya. 1 Nefi 2:16 Nefi aliwaelezea kaka zake kile ambacho Yesu alikuwa amemwambia. Samu alimwamini Nefi, lakini Lamani na Lemueli hawakumwamini. 1 Nefi 2:17–18 Bwana alimwahidi Nefi kwamba angebarikiwa kwa sababu ya imani yake. Angekuwa kiongozi wa kaka zake. 1 Nefi 2:19–22