Sura ya 15 Alma Anafundisha na Kubatiza Alma alitoroka kutoka kwa watumishi wa Mfalme Nuhu na kujificha kwa siku nyingi. Wakati amejificha, aliandika kile nabii Abinadi alikifundisha. Mosia 17:3–4 Alma alitubu dhambi zake na kwenda kwa Wanefi kwa siri, akiwafundisha wao ujumbe wa Abinadi. Alma aliwaambia watu wawe na imani kwa Yesu Kristo na watubu. Mosia 18:1, 7 Wakati wa mchana Alma alijificha katika msitu karibu na kijito kilichoitwa Maji ya Mormoni. Mosia 18:5 Wale walioamini mafundisho ya Alma walikwenda kwenye Maji ya Mormoni na walibatizwa. Alma alibatiza watu 204 kwenye Kanisa la Kristo. Mosia 18:8–10, 16–17 Alma aliwatawaza makuhani kuwafundisha watu. Aliwaambia makuhani kufundisha toba na imani katika Yesu Kristo. Aliwaambia pia lazima wasibishane lakini wawe wamoja. Mosia 18:18, 20–21. Watu wa Alma walipendana na kutumikiana. Walishiriki kila kitu walichokuwa nacho na walikuwa wenye shukrani kwamba walijifunza kuhusu Yesu Kristo, mwokozi wao. Mosia 18:29–30 Watumishi wa Mfalme Nuhu walimuona Alma akiwafundisha watu. Mfalme alisema Alma alikuwa akiigeuza mioyo ya Wanefi dhidi yake, hivyo alituma jeshi kuwauwa. Mosia 18:32–33 Mungu alimuonya Alma kwamba jeshi la Mfalme Nuhu lilikuwa linakuja. Watu walizikusanya familia zao, mifugo, na mali zingine na kutorokea nyikani. Mosia 18:34; 23:1 Mungu aliwaimarisha watu wa Alma kwamba wangeweza kutoroka kutoka kwa jeshi la Mfalme. Jeshi liliwatafuta lakini halikuwapata. Mosia 19:1; 23:2 Baada ya kusafiri nyikani kwa siku nne, watu wa Alma walifika kwenye eneo zuri ambalo lilikuwa na maji safi yakitiririka. Hapo walipanda mazao na kujenga majengo. Mosia 23:3–5 Watu walitaka Alma awe mfalme wao, lakini Alma alisema Mungu hakutaka wao wawe na mfalme. Mungu alitaka wao wawe huru. Mosia 23:6–7, 13