Sura ya 10 Yakobo na Sheremu Kabla ya Nefi kufariki alimpa ndugu yake mdogo Yakobo bamba alizokuwa ameziandika. Yakobo alikuwa mwenye haki. Yakobo 1:1–2, 8 Nefi alimwambia Yakobo aandike vitu ambavyo vingewasaidia watu kuamini katika Yesu Kristo. Yakobo 1:4–6 Nefi alimpa Yakobo uwezo wa kuwa kuhani katika Kanisa na kuwafundisha Wanefi neno la Mungu. Yakobo 1:18 Baada ya Nefi kufariki wengi kati ya Wanefi walikuwa waovu. Yakobo aliwafundisha watu na kuwaambia watubu uovu waliokuwa wakiutenda. Yakobo 1:15–17 Mwanaume mwovu aliyeitwa Sheremu alizunguka miongoni mwa Wanefi, akiwafundisha wasiamini katika Yesu Kristo. Yakobo 7:1–2 Sheremu aliwaambia watu kwamba hakungekuwepo na Kristo. Watu wengi walimwamini Sheremu. Yakobo 7:2–3 Yakobo aliwafundisha watu kuamini katika Kristo. Sheremu alitaka kubishana na Yakobo na kumshawishi kwamba hakungekuwepo na Kristo. Yakobo 7:6 Imani ya Yakobo katika Yesu Kristo haingeweza kutikisika. Alikuwa amewaona malaika na alikuwa ameisikia sauti ya Bwana. Alijua kwamba Yesu angekuja. Yakobo 7:5 Roho Mtakatifu alikuwa na Yakobo alipokuwa akishiriki ushuhuda wake wa Yesu Kristo kwa Sheremu. Yakobo 7:8–12 Sheremu alitaka kuona ishara. Alitaka Yakobo athibitishe kwamba kuna Mungu. Alitaka kuona muujiza. Yakobo 7:13 Yakobo alikataa kumuomba Mungu aonyeshe ishara. Alisema Sheremu tayari alijua kwamba kile Yakobo acholikuwa amefundisha kilikuwa kweli. Yakobo 7:14 Yakobo alisema ikiwa Mungu angempiga Sheremu, hiyo ingekuwa ishara ya uwezo wa Mungu. Yakobo 7:14 Sheremu mara moja akaanguka chini. Hakuweza kusimama kwa kipindi cha siku nyingi. Yakobo 7:15 Sheremu alikuwa mdhaifu na alijua alikuwa anakaribia kifo. Aliwaita watu pamoja. Yakobo 7:16 Aliwaambia kwamba alikuwa amedanganya. Aliwaambia waamini katika Yesu Kristo. Yakobo 7:17–19 Baada ya Sheremu kumaliza kuongea na watu, alifariki. Watu walihisi nguvu za Mungu, na waliinama kwenye ardhi. Yakobo 7:20–21 Watu walianza kutubu na kusoma maandiko. Waliishi kwa amani na upendo. Yakobo alikuwa na furaha na alijua ya kwamba Mungu alikuwa amejibu sala zake. Yakobo 7:22–23