Sura ya 42 Ishara za Kusulubiwa kwa Kristo Miaka thelathini na tatu ilikuwa imepita tangu watu walipokuwa wameziona ishara za kuzaliwa kwa Yesu Kristo. 3 Nefi 8:2 Sasa walisubiri kuona ishara ya kifo chake: siku tatu za giza. 3 Nefi 8:3 Baadhi hawakuamini kwamba ishara hii ingeonekana. Walibishana na wale walioamini. 3 Nefi 8:4 Siku moja dhoruba kali ilikuja. Kulikuwa na upepo mkali. 3 Nefi 8:5–6 Radi iliwaka, na ngurumo ilitetemesha dunia nzima. 3 Nefi 8:6–7 Mji wa Zarahemla uliwaka moto. Mji wa Moroni ulizama baharini. Mji wa Moroniha ulifunikwa na ardhi. 3 Nefi 8:8–10 Tetemeko la ardhi litetemesha dunia nzima. Barabara kuu ziliharibiwa, na majengo yakaanguka. Miji mingi iliharibiwa, na watu wengi waliuwawa. 3 Nefi 8:12–15 Dhoruba na tetemeko la ardhi vilidumu kwa takriban masaa matatu. 3 Nefi 8:19 Wakati dhoruba na tetemeko la ardhi vilipokoma, giza lilitanda nchini. Hapakuwa na mwangaza mahali popote. Watu hata waliweza kuhisi giza hilo. 3 Nefi 8:19–20 Giza lilidumu kwa muda wa siku tatu. Mishumaa haikuwaka, na watu hawakuweza kuliona jua, mwezi, au nyota. 3 Nefi 8:21–23 Watu walilia kwa sababu ya giza, uharibifu, na mauti. Walisikitika kwa kuwa hawakuwa wametubu dhambi zao. 3 Nefi 8:23–25 Kisha watu wakasikia sauti ya Yesu Kristo. 3 Nefi 9:1, 15 Yesu aliwaambia kuhusu uharibifu mkuu katika nchi. Alisema kwamba watu waovu zaidi walikuwa wameangamizwa. 3 Nefi 9:12–13 Alisema kwamba wale ambao walikuwa wamenusurika walihitaji kutubu. Kama wangefanya hivyo na kuja kwake, angewabariki. 3 Nefi 9:13–14 Watu walistaajabu baada ya kuisikia sauti hadi wakaacha kulia. Kulikuwa na kimya kwa masaa mengi. 3 Nefi 10:1–2 Kisha Yesu akazungumza tena, akisema mara nyingi alikuwa amejaribu kuwasaidia watu. Kama wangetubu hivi sasa, bado wangeweza kurudi kwake. 3 Nefi 10:3–6 Baada ya siku tatu giza liliondoka. Watu walisherehekea na kumshukuru Bwana kwa Shangwe. 3 Nefi 10:9–10