Sura ya 16
Mfalme Limhi na Watu Wake Wanatoroka
Walamani waliwashika wengi kati ya Wanefi ambao hawakuwa wametoroka pamoja na Mfalme Nuhu. Walamani waliwachukua na kuwapa ardhi lakini wakawa wanawatoza ushuru mwingi.
Wanefi walimfanya Limhi awe mfalme wao mpya. Limhi alikuwa mwana wa Mfalme Nuhu, lakini hakuwa mwovu kama baba yake. Alikuwa mtu mzuri.
Mfalme Limhi alijaribu kufanya amani na Walamani, lakini waliendelea kuwalinda Wanefi na kuwa wakatili kwao.
Siku moja Mfalme Limhi aliwaona watu wasiojulikana nje ya mji. Alisababisha wawekwe gerezani. Watu hawa wasiojulikana walikuwa Wanefi kutoka Zarahemla.
Kiongozi wao aliitwa Amoni. Mfalme Limhi alikuwa na furaha kumwona. Alijua kwamba Amoni angeweza kuwasaidia watu wake kutoroka kutoka kwa Walamani.
Mfalme Limhi aliwaita watu wake pamoja. Aliwakumbusha ya kwamba uovu wao ndiyo sababu walikuwa wakizuiliwa na Walamani.
Aliwaambia watu wake watubu, wamwamini Mungu, na kutii amri. Kisha Mungu angewasaidia kutoroka.
Wanefi waligundua ya kwamba Walamani ambao walilinda mji kawaida walikuwa wakilewa wakati wa usiku.
Usiku huo Mfalme Limhi aliwapelekea walinzi divai nyingi kama zawadi.
Mfalme Limhi na watu wake waliweza kupita kando ya walinzi waliokuwa wamelewa na kutoroka.
Amoni alimuongoza Mfalme Limhi na watu wake kupitia nyikani hadi Zarahemla, ambapo walikaribishwa.