Sura ya 28 Wazoramu na Rameumtomu Wazoramu kwa wakati fulani walikuwa waumini wa Kanisa la Mungu lakini walikuja kuwa waovu na walikuwa wakiabudu sanamu. Alma 31:1, 8–9 Wanefi walitaka kuwazuia Wazoramu kujiunga na Walamani, kwa hivyo Alma na baadhi ya waisionari wengine walienda kuhubiri neno la Mungu kwa Wazoramu. Alma 31:4, 11 Wamisionari hawa walishangazwa na kukasirishwa na jinsi ambavyo Wazoramu walikuwa wakiabudu katika makanisa yao, yaliyoitwa sinagogi. Alma 31:12 Katikati ya Kanisa, Wazoramu walikuwa wamejenga jukwaa refu lililoitwa Rameumtomu. Kulikuwa na nafasi ya mtu mmoja tu kusimama juu yake. Alma 31:13, 21 Wazoramu walifanya zamu kusimama pale, walinyosha mikono kuelekea mbinguni na kwa sauti kubwa kukariri sala inayofanana. Alma 31:14, 20 Katika sala hii, Wazoramu walisema Mungu hana mwili; yeye ni roho tu. Pia walisema kwamba hakungekuwepo na Kristo. Alma 31:15–16 Wazoramu walidhani kwamba Mungu alikuwa amewachagua wao pekee kuokolewa katika ufalme wa Mungu. Walishukuru kwa kuwa watu wake wapendwa. Alma 31:17–18 Baada ya kila Mzoramu kusali, walienda nyumbani na hawakusali au kuzungumza tena kuhusu Mungu kwa wiki mzima. Alma 31:12, 23 Wazoramu matajiri walipenda dhahabu na fedha, na walijigamba kuhusu utajiri wao hapa duniani. Alma alihuzunika kuona jinsi walivyokuwa waovu. Alma 31:24–25 Alma alisali kwa ajili yake na wamisionari wake kuwa na nguvu, faraja, na mafanikio katika kazi yao. Alma 31:26, 32–33 Baada ya kuomba msaada kwa ajili ya kuwarejesha Wazoramu kwenye ukweli, Alma na wale wamisionari wengine walijazwa na Roho Mtakatifu. Alma 31:34–36 Wamisionari kisha walielekea katika sehemu tofauti kuhubiri. Mungu aliwabariki kwa chakula na mavazi na kuwaimarisha katika kazi yao. Alma 31:37–38 Wazoramu waliokuwa maskini hawakukubaliwa ndani ya makanisa. Watu hawa walianza kuwasikiliza wamisionari. Alma 32:2–3 Wengi walimwuliza Alma kile walichopaswa kufanya. Alma aliwaambia kwamba hawakuhitaji kuwa ndani ya kanisa ili wasali au wamwabudu Mungu. Alma 32:5, 10–11 Aliwaambia wawe na imani kwa Mungu. Kisha Amuleki akawafundisha kuhusu Yesu Kristo na mpango wa Mungu kwa ajili ya watoto wake. Alma 32:17–21; 34:8–9 Wamisionari waliondoka, na Wazoramu waliokuwa wamewaamini wakafukuzwa kutoka mjini. Waaminifu walienda kuishi katika nchi ya Yershoni na watu wa Amoni. Alma 35:1–2, 6 Ingawaje Wazoramu waovu waliwatolea vitisho watu wa Amoni, watu wa Amoni waliwasaidia Wazoramu wenye haki na kuwapa chakula, mavazi, na ardhi. Alma 35:8–9