Sura ya 35 Kapteni Moroni na Pahorani Kapteni Moroni alifurahi kusikia kwamba Helamani na jeshi lake waliweza kutwaa tena sehemu kubwa ya ardhi ya Wanefi kutoka kwa Walamani. Alma 59:1 Lakini Helamani na jeshi lake walihitaji msaada. Hawakuwa na wanajeshi wa kutosha kulinda miji mingi. Alma 58:32 Kapteni Moroni aliandika barua kwa Pahorani mwamuzi mkuu na gavana. Alimuomba Pahorani atume wanajeshi zaidi kulisaidia jeshi la Helamani. Alma 59:3 Walamani waliuvamia mji wa Wanefi ambao Helamani alikuwa ameuchukua. Waliwauwa wengi wa Wanefi na kuwafukuza waliobaki kutoka kwenye mji. Alma 59:5–8 Akiwa ameukasirikia uongozi wa serikali kwa sababu hawakutuma msaada, Moroni aliandika barua nyingine kwa Pahorani. Alma 59:13; 60:1 Kapteni Moroni aliandika kwamba watu wengi walikuwa wameuwawa kwa sababu Pahorani hakutuma wanajeshi zaidi. Alma 60:5 Kwa vile Pahorani hakutuma haraka watu zaidi na chakula, Moroni angechukua jeshi lake mpaka Zarahemla na kuchukua kile jeshi lake lilichokihitaji. Alma 60:34–35 Punde Moroni alipokea barua kutoka kwa Pahorani. Alikuwa na huzuni kwamba Moroni na jeshi lake walikuwa wakiteseka. Alma 61:1–2 Pahorani alimwambia Moroni kwamba kundi la Wanefi waovu walioitwa watu wa mfalme hawakumtaka yeye kuwa mwamuzi mkuu. Walikuwa wamemlazimisha yeye na wale waliomuunga mkono kutoka nje ya Zarahemla. Alma 61:3–5 Pahorani aliongeza kwamba alikuwa akikusanya jeshi kujaribu kuuchukua tena mji wa Zarahemla. Alma 61:6–7 Watu wa mfalme walikuwa wamemchagua mfalme kuwa kiongozi wao na walikuwa wameungana na Walamani. Alma 61:8 Pahorani hakuwa na hasira juu ya kile Moroni alichokuwa amekiandika. Alitaka Wanefi kuwa huru pia. Alma 61:9 Alimuomba Moroni kuleta watu wachache kumsaidia na akasema kama Moroni angekusanya watu zaidi njiani, jeshi lililoungana lingeweza kuuchukua tena mji wa Zarahemla. Alma 61:15–18 Kapteni Moroni alikuwa na furaha kwamba Pahorani bado alikuwa mwaminifu kwa nchi yake na bado alitaka uhuru kwa ajili ya watu. Alma 62:1 Akiwa na watu wachache, Moroni alikwenda kukutana na Pahorani. Alibeba bendera ndogo ya uhuru, na maelfu ya wanaume waliungana nao njiani. Alma 62:3–5 Jeshi la muungano la Moroni na Pahorani lilisonga kuelekea Zarahemla. Walimuua mfalme wa Wanefi waovu na kuwateka watu wake. Alma 62:7–8 Kisha Moroni alituma chakula na wanajeshi 12,000 kusaidia majeshi ya Wanefi. Majeshi haya yaliwafukuza Walamani, na kulikuwa na amani tena katika nchi. Alma 62:12–13, 38–42