Sura ya 39 Nefi Anapokea Nguvu Kuu Nefi alitembea kuelekea nyumbani kwake, akitafakari kuhusu kile Bwana alichomwonyesha na kuhusu uovu wa Wanefi. Alihuzunika kwa sababu ya uovu wao. Helamani 10:1–3 Bwana alizungumza na Nefi na kumsifia kwa kuwa mtiifu na kwa kufanya kazi kwa bidii kufundisha injili. Helamani 10:4 Nefi alipewa nguvu za kufanya chochote. Bwana alijua angetumia nguvu hii kwa haki. Helamani 10:5 Bwana alimwambia Nefi kuwaonya Wanefi kwamba kama hawangetubu, wangeangamizwa. Nefi alikwenda mara moja kuwaonya watu. Helamani 10:11–12 Wanefi hawakumwamini Nefi. Walijaribu kumtupa gerezani, lakini nguvu za Mungu zilimlinda. Helamani 10:15–16 Nefi alitangaza neno la Mungu kwa Wanefi wote. Helamani 10:17 Lakini watu walizidi kuwa waovu zaidi na kuanza kupigana wao kwa wao. Helamani 11:1 Nefi alisali kwa ajili ya njaa, akiamini kwamba ukosefu wa chakula ungewanyenyekeza Wanefi na kuwasaidia kutubu. Helamani 11:3–4 Baa la njaa lilikuja. Hakukuwa na mvua, kwa hivyo ardhi ilikauka na mazao hayakukua. Watu waliacha kupigana. Helamani 11:5–6 Wanefi walikuwa na njaa, na wengi wao walikufa. Wale waliobaki walianza kumkumbuka Bwana na kile ambacho Nefi aliwafundisha. Helamani 11:6–7 Watu walitubu dhambi zao na kisha waliwaomba waamuzi wao kumuomba Nefi asitishe baa la njaa. Waamuzi wakienda kwa Nefi Helamani 11:8–9 Wakati Nefi alipowaona watu kwamba walikuwa wanyenyekevu na wametubu, alimuomba Bwana kumaliza baa la njaa. Helamani 11:9–12 Bwana alijibu sala ya Nefi, na mvua ilianza kunyesha. Punde mazao yalianza kukua tena. Watu walimshukuru Mungu na kujua kwamba Nefi alikuwa ni nabii. Helamani 11:17–18 Wengi wa Wanefi walijiunga na Kanisa. Walikuwa matajiri, na miji yao ikakua. Kulikuwa na amani katika nchi. Helamani 11:20–21 Kisha baadhi ya Wanefi ambao hapo awali walijiunga na Walamani waliwavamia Wanefi. Helamani 11:24 Wanefi walijaribu kuwashinda maadui wao, ambao walikuwa Wanyang’anyi wa Gadiantoni, lakini hawakuweza kwa sababu wao wenyewe walikuwa waovu tena. Helamani 11:26, 28–29 Wakati wanefi walipokuwa wema, Bwana aliwabariki. Walipokuwa na kiburi na kumsahau Bwana, aliwapa matatizo ili kuwasaidia kumkumbuka. Helamani 12:1–3