Scripture Stories
Sura ya 44: Yesu Kristo Anawabariki Watoto


Sura ya 44

Yesu Kristo Anawabariki Watoto

Picha
Kristo na watoto

Yesu Kristo aliwaambia Wanefi wawalete watoto wao kwake. Watoto waliketi chini karibu na Yesu.

Picha
Yesu akisali pamoja na watoto

Mwokozi aliwaambia watu wapige magoti. Kisha akapiga magoti na kumwomba Baba wa Mbinguni.

Picha
watu wakitabasamu

Sala ya Mwokozi ilikuwa ya ajabu kiasi kwamba haikuweza kuandikwa. Iliwajaza Wanefi na shangwe.

Picha
Yesu akizungumza na watu

Baada ya sala yake Yesu alisema kwamba Wanefi wangebarikiwa kwa sababu ya imani yao.

Picha
Yesu

Alihisi upendo na furaha nyingi hadi akalia.

Picha
Yesu anawabariki watoto

Kisha akawachukua watoto na kuwabariki kila mmoja. Aliomba kwa Baba wa Mbinguni kwa ajili yao na akalia tena.

Picha
Yesu pamoja na watoto

Yesu aliwaambia Wanefi wawatazame watoto wao.

Picha
malaika wakiwa wamewazingira watoto

Watu wakiwa wanatazama, malaika walishuka kutoka mbinguni na kuwazingira watoto. Watoto na malaika walikuwa wamezingirwa na moto.

Chapisha