Sura ya 19 Wana wa Mosia Wanakuwa Wamisionari Mosia alikuwa na wana wanne: Amoni, Haruni, Omneri, na Himni. Walikuwa pamoja na Alma Mdogo wakati malaika alipomtokea. Mosia 27:11, 34 Wana wa Mosia walikuwa wametubu dhambi zao na walihuzunika kwa ajili ya taabu waliyokuwa wamesababisha. Walijua injili ilikuwa ya kweli, na walitaka kuwafundisha wengine. Mosia 27:35–36 Kila mmoja wa wana wa Mosia alikataa kuwa mfalme. Badala yake, walitaka kuhudumu kama wamisionari kwa Walamani na kushiriki nao baraka za injili. Mosia 28:1, 10; 29:3 Mfalme Mosia alisali aweze kujua ikiwa alipaswa kuwaruhusu wana wake waende. Mungu alimwambia awaruhusu waende, na wangelindwa. Walamani wengi wangeamini ujumbe wao. Mosia 28:6–7 Wana wa Mosia walienda kuwafundisha Walamani. Walifunga na kusali ili wawe wamisionari wazuri. Mosia 28:9; Alma 17:9