Sura ya 41 Ishara za kuzaliwa kwa Kristo Nefi, mwana wa Helamani, alimpa kumbukumbu takatifu na maandiko mwanawe mkubwa, Nefi 3 Nefi 1:2 Wanefi waliona ishara kuu na maajabu ambayo manabii walikuwa wamesema yangetokea kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. 3 Nefi 1:4 Lakini baadhi ya Wanefi walisema wakati wa Yesu kuzaliwa tayari ulikuwa umepita. Waliwadhihaki wale walioendelea kuuamini unabii wa Samweli Mlamani. 3 Nefi 1:5–6 Watu walioamini katika Yesu Kristo na manabii walihuzunika na kudhani kwamba kitu fulani kingeuzuia unabii usitimie. 3 Nefi 1:7 Watu waliutazamia kwa uaminifu usiku ambao hauna giza, ambao ulikuwa ni ishara kwamba Yesu Kristo angezaliwa. 3 Nefi 1:8 Wale ambao hawakuamini katika Yesu Kristo walichagua siku ya kuwauwa walioamini kama ishara isingeonekana. 3 Nefi 1:9 Nefi alihuzunika kwa sababu ya uovu wa wale ambao hawakuamini katika Mwokozi. 3 Nefi 1:10 Nefi alisali siku nzima kwa ajili ya watu ambao wangeuwawa. 3 Nefi 1:11–12 Bwana alimfariji Nefi na kumwambia kwamba usiku huo usingekuwa na giza. Yesu angezaliwa siku iliyofuata huko Bethlehemu. 3 Nefi 1:13 Usiku huo jua lilitua, lakini hakukuwa na giza. Ishara ya kuzaliwa kwa Kristo ilionekana. Watu walishangazwa. 3 Nefi 1:15 Wale waliokuwa wamepanga kuwauwa waaminio walianguka ardhini na kuonekana kama wafu. 3 Nefi 1:16 Waliogopa kwa sababu walikuwa waovu. Sasa walijua kwamba Mwokozi angezaliwa na kwamba manabii walikuwa sahihi. 3 Nefi 1:17–18 Kulikuwa na mwanga usiku mzima. Jua lilipotoka asubuhi iliyofuata, watu walijua kwamba Yesu Kristo angezaliwa siku hiyo. Unabii ulikuwa umetimia. 3 Nefi 1:19–20 Nyota mpya ilitokea kwenye anga, kama vile manabii walivyosema ingetokea. 3 Nefi 1:21 Shetani bado aliwafanya watu kutoamini ishara ambayo waliiona, lakini wengi waliamini. 3 Nefi 1:22 Nefi na viongozi wengine wa Kanisa waliwabatiza wote ambao waliamini na kutubu. 3 Nefi 1:23 Kulikuwa na habari njema katika nchi kwa sababu maneno ya manabii yalikuwa yametimizwa. Yesu Kristo alikuwa amezaliwa. 3 Nefi 1:26