Maneno ya Kujua
A
-
madhabahuSehemu takatifu, eneo lililonyanyuliwa kwa mchanga au miamba ambapo sala au sadaka hutolewa kwa Mungu
-
malaikamjumbe kutoka kwa Mungu
-
Vazi la kivitaVazi ambalo wanajeshi huvaa kujilinda wao wenyewe katika vita.
-
jeshiKundi la wanajeshi wakijiandaa kupigana
-
mshaleSilaha yenye ncha iliyochongoka itumikayo kuwindia au vitani
B
-
ubatizoIbada ambapo mtu mwenye mamlaka kutoka kwa Mungu humzamisha mtu mwingine majini kabisa na kumnyanyua mtu huyo tena kutoka majini. Ubatizo unahitajika ili kuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo.
-
mashuaBoti kubwa iliyotumika kubeba watu au vitu
-
aminiKuhisi au kujua kwamba kitu fulani ni kweli
-
barikiKumpa mtu kitu ambacho kitamsaidia. Kubariki sakramenti ni kumuomba Mungu kukubali mkate na maji kama ishara ya Yesu Kristo.
-
kipofukutoweza kuona
-
utumwakutokuwa huru, na kutakiwa kufanya kazi siku nzima kwa manufaa ya mtu fulani
-
upindeFimbo ndefu yenye kamba iliyofungwa katika kila ncha yake ambayo hutumika kurusha mishale
-
bamba za shabaKumbukumbu ya amri za Mungu na matendo yake kwa mababu wa Lehi
-
jengakutengeneza au kuunda kitu
C
-
kapteniKiongozi wa jeshi
-
runguZana iliyotumika kupigia wanyama au watu
-
amrikitu ambacho Mungu huwaambia watu Wake kufanya ili waje kuwa na furaha
-
aganoahadi takatifu kati ya Mungu na watu
-
sulubishaKumuua mtu kwa kumpigilia kwa misumari msalabani
D
-
kiziwikutoweza kusikia
-
angamizaKuharibu au kumaliza kitu kabisa, kama vile mji au maisha
-
mwanafunzimtu anayemfuata Yesu na kujaribu kuwa kama Yeye.
-
ndotohadithi ambayo huwa katika mawazo ya mtu wakati amelala
-
kulewaUkosefu wa kujidhibiti kutokana na kunywa pombe sana
E
-
torokaKwenda mbali na mtu
-
uzima wa mileleKuishi milele na Mungu
-
uovuKitu ambacho ni kibaya
F
-
imanikuamini katika Yesu Kristo
-
uaminifuKuendelea kutii amri
-
baa la njaaUkosefu wa chakula usababishwao na kukosekana kwa mvua na kushindwa kuota kwa mazao
-
kufungaKutokula wala kunywa wakati ukitafuta msaada wa kiroho
-
kujazwa na Roho MtakatifuKuwa na Roho Mtakatifu kuweka ukweli kwenye mawazo na akili za mtu
-
kusameheKusahau vitu vibaya ambavyo mtu amevifanya na kumpenda mtu
-
uhuruKuwa na uwezo wa kufanya maamuzi
G
-
habari njemaJumbe za matumaini na faraja kutoka kwa Mungu
-
bamba ya dhahabuKumbukumbu iliyoandikwa kwenye bati nyembamba za dhahabu. Moroni alizificha bamba hizi katika Mlima Kumora, na Joseph Smith baadaye alizifukua.
-
injilimafundisho ya Yesu Kristo
-
Roho MkuuJina la Mungu kutoka kwa Walamani
H
-
ponyakufanya mtu aliye mgonjwa ama aliye umia kuwa mzima
-
mbingunimahali ambapo Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanaishi
-
unyenyekevuKuwa wa kufundishika na wa kutafuta kutenda mapenzi ya Mungu
I
-
sanamuKitu ambacho watu hukiabudu ambacho si Mungu
-
fimbo ya chumaAlama katika ndoto ya Lehi ambayo huwakilisha neno la Mungu
J
-
jiungekuwa sehemu ya kikundi
-
mwamuziKiongozi ambaye huamua nini sheria humaanisha au jinsi watu wanavyotakiwa kuzishika
-
Kiti cha hukumuWadhifa katika serikali ya Wanefi ambayo mwamuzi mkuu alikwa nao
K
-
MfalmeKiongozi juu ya kikundi cha watu
L
-
kiongoziMtu ambaye huongoza kikundi cha watu
-
LiahonaChombo cha mviringo cha shaba Mungu alichowapa familia ya Lehi kuwaonyesha njia ya kuelekea nyikani. Kilifanya kazi pale tu familia ya Lehi ilipokuwa yenye haki.
-
uhuruUhuru wa kufanya uchaguzi
M
-
mshirikimtu ambaye yuko katika kanisa ama kikundi
-
muujizaTukio lisilo la kawaida au tukio linaloonyesha uwepo wa nguvu za Mungu
-
mmisionariMtu ambaye anafundisha injili ya Yesu Kristo
O
-
tiikufanya kile ambacho kinatakiwa au kimeamriwa.
-
tawazaKutoa nguvu ya ukuhani na mamlaka
-
ibadaUtaratibu mtakatifu au kitendo ambacho kina maana ya kiroho, kama vile ubatizo au sakramenti
P
-
amaniHisia tulivu au wakati ambapo hakuna vita
-
tesaKusema vitu vya uwongo juu ya mtu fulani na kujaribu kuwaumiza
-
bambaVipande vyembamba vya metali ambavyo watu walitumia kuandikia mafundisho ya Mungu na historia za watu
-
Kula njamaKuweka mpango mwovu dhidi ya mtu fulani
-
nguvuNguvu ya wema au uovu, mara nyingi msaada maalum au nguvu kutoka kwa Mungu
-
salikuzungumza na Mungu, kumpa shukrani na kumuomba baraka
-
ukuhanimamlaka ya kutenda katika jina la Mungu
-
gerezaSehemu iliyotumika kuwaweka watu ambao wametenda makosa.
-
ahadiNadhiri au utayari wa kutenda kitu au kuwa mtu fulani
-
unabiiKuelezea tukio kabla halijatokea
-
nabiiMtu aliyeitwa na Mungu kuwaambia watu mapenzi ya Mungu
-
adhibuKusababisha au kuruhusu vitu vibaya kutokea kwa mtu fulani. Watu mara nyingi wanaadhibiwa wakati hawamtii Mungu.
R
-
MwasiKutotii au kwenda kinyume na amri
-
tubuKuhisi huzuni kutokana na tendo au wazo na kuahidi kutolirudia
-
fufukaKumrudishia mtu au kitu uhai
-
hakiKitu ambacho ni cha Mungu Watu wenye haki ni wale ambao wanafuata amri za Mungu.
-
johoNguo ndefu ya ifunikayo mwili mzima
S
-
sakramentiIbada ambapo wanaume ambao wana ukuhani hubariki na kupitisha mkate na maji kwa watu wengine. Sakramenti huwakumbusha watu kuhusu Yesu Kristo.
-
dhabihuKuacha kitu cha thamani kwa ajili ya Mungu
-
Ondoa ngozi ya juu ya kichwaKukata ngozi ya juu ya kichwa cha mtu fulani
-
mtumishiWatu ambao hutumikia au kufanya kazi kwa mtu fulani kama vile mfalme
-
NgaoSehemu ya vazi la kivita ambayo hulinda sehemu ya juu ya mwili wa askari dhidi ya upanga na silaha zingine
-
dhambiKuvunja amri
-
watumwaWatu ambao wanalazimishwa kufanya kazi kwa ajili ya watu wengine
-
kombeoSilaha itumikayo katika kurusha mawe
-
askariMtu ambaye anapigana katika jeshi
-
mkukiFimbo ndefu, yenye ncha kali itumikayo kuchomea
-
ibakuchukua kitu ambacho ni cha mtu mwingine
-
Piga kwa jiweKurusha vipande vya miamba kwa mtu mpaka anapofariki
-
upangaKipande kirefu cha metali, chenye makali kitumikacho kukata au kuchana
-
sinagogiAina ya jengo ambapo watu hukusanyika kumwabudu Mungu
T
-
hekalunyumba ya Mungu.
-
ushuhudaHisia au ushahidi kwamba injili ni ya kweli
-
Bendera ya uhuruUjumbe ambao kapteni Moroni aliuandika kuwahamasisha watu wake kuulinda uhuru wao
-
mnaraJengo refu au jukwaa refu ambapo watu wanaweza kusimama
-
tafsiriKubadilisha maneno kutoka lugha moja kwenda nyingine
-
Mti wa uzimaMti katika ndoto ya Lehi ambao unawakilisha upendo wa Mungu
-
kweliKitu fulani ambacho kweli kilitokea au ambacho ni kizuri au sahihi
U
-
FahamuKujua au kuelewa wazo fulani
-
Urimu na thumimuNyenzo maalum ambazo Mungu huwapa manabii kuwasaidia wao kutafsiri na kupokea ufunuo
V
-
thabitiKujua na kulinda kilicho cha kweli
-
onoAina ya ufunuo
W
-
vitaMapigano kati ya maadui au majeshi yanayopingana
-
silahaKitu fulani knachotumika kudhuru au kuua watu wengine kama vile upanga au mkuki
-
uovuKitu ambacho si cha Kiungu Mtu mwovu humpenda Shetani na hatii amri za Mungu.
-
nyikaSehemu wazi kubwa ya nchi ambayo haina miji au watu
-
abuduKupenda au kumfuata mtu au kitu