Sura ya 53 Moroni na Mafundisho Yake Baada ya Mormoni kufariki, Moroni alibaki peke yake. Alimalizia kumbukumbu ambazo baba yake alikuwa amempa yeye. Mormoni 8:1, 3 Moroni alijua bamba za dhahabu siku moja zingetolewa kutoka kwenye ardhi. Mormoni 8:16 Maneno yaliyoko kwenye bamba za dhahabu yanashuhudia kuhusu Yesu Kristo. Yanatoa ushuhuda na kufundisha watu jinsi ya kuishi kwa haki. Mormoni 9:11–12, 27 Walamani waovu walimuua kila Mnefi ambaye alikataa kumkana Yesu Kristo. Moroni 1:2 Moroni kamwe asingemkana Yesu Kristo. Alihama hama, akijificha kutoka kwa Walamani. Moroni 1:3 Moroni aliandika mengi zaidi kwenye bamba za dhahabu, hasa kwa Walamani wa siku za Mwisho. Moroni 1:4 Aliandika vitu vingi muhimu, ikijumuisha maneno ya sala za sakramenti. Moroni 4; 5 Moroni aliandika kwamba wanaoweza kubatizwa ni wale tu walio radhi kutubu dhambia zao na kumtumikia Yesu Kristo. Moroni 6:1–3 Moroni alitaka kila mtu amwamini Yesu Kristo na waweze kumfahamu. Alisema kila kilicho kizuri kinatoka kwa Kristo. Moroni 10:18, 30 Moroni aliandika kwamba kama watu watampenda Mungu na kumfuata, wanaweza kuwa wakamilifu. Moroni 10:32 Moroni alijua kwamba baada ya kufariki angefufuliwa na angeishi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Moroni 10:34