Sura ya 27 Korihori Mtu mmoja aliyeitwa Korihori alikuja Zarahemla. Hakuwa na imani katika Yesu Kristo na alihubiri kwamba kile ambacho manabii walisema kuhusu Mwokozi kilikuwa si kweli. Alma 30:6, 12–14 Korihori aliwaambia watu walikuwa wapumbavu kuamini kwamba Yesu angekuja duniani na kuteseka kwa ajili ya dhambi zao. Alma 30:16 Alisema watu hawawezi kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao kwa sababu hakuna maisha baada ya kifo. Watu wengi walimwamini Korihori. Wakageuka kuwa waovu. Alma 30:17–18 Korihori alijaribu kuwahubiria watu wa Amoni, lakini hawakumsikiliza. Walimfunga na kumpeleka kwa Amoni, ambaye alimlazimisha kuondoka mjini. Alma 30:19–21 Korihori alienda katika nchi ya Gideoni, lakini watu waliokuwa huko pia walikataa kumsikiliza. Mwamuzi mkuu alimpeleka kwa Alma. Alma 30:21, 29 Alma alimuuliza Korihori kama aliamini katika Mungu. Korihori alisema la. Alma alishuhudia ya kwamba kuna Mungu na kwamba Kristo angekuja. Alma 30:37–39 Korihori alimtaka Alma atende muujiza ili athibitishe kwamba kuna Mungu. Korihori alisema angesadikishwa kwamba kuna Mungu ikiwa angeona ishara ya uwezo wa Mungu. Alma 30:43 Alma alimwambia Korihori kwamba alikuwa amekwisha kuziona ishara nyingi za uwezo wa Mungu kupitia maandiko na shuhuda za manabii wote. Alma 30:44 Alma alisema kwamba dunia na vitu vyote vilivyo juu yake na mwendo wa sayari zilizo mbinguni pia ni ishara kwamba kuna Mungu. Alma 30:44 Korihori bado alikataa kuamini. Alma alikuwa na huzuni kwa sababu ya uovu wa Korihori na akamuonya kwamba nafsi yake ingeweza kuangamizwa. Alma 30:45–46 Korihori bado alitaka ishara kuthibitisha kwamba kuna Mungu. Alma alisema ishara kutoka kwa Mungu ingekuwa kwamba Korihori hangeweza kusema. Alma 30:48–49 Baada ya Alma kusema haya, Korihori hakuweza kuzungumza. Alma 30:50 Korihori aliandika kwamba alijua hii ilikuwa ishara kutoka kwa Mungu na kwamba daima alikuwa anajua kuna Mungu. Alimuomba Alma asali na kuiondoa ile laana. Alma 30:52, 54 Alma alijua ya kwama kama Korihori angeweza kusema tena angewadanganya watu tena. Alma alisema kwamba Bwana angeamua kama Korihori angezungumza tena. Alma 30:55 Bwana hakumrudishia Korihori uwezo wake wa kusema. Korihori alikwenda nyumba hadi nyumba, akiomba chakula. Alma 30:56 Mwamuzi mkuu alituma barua kote nchini ikisema kilichompata Korihori. Aliwaambia wale ambao walikuwa wamemwamini Korihori watubu. Watu walitubu. Alma 30:57–58 Korihori alienda kuishi na Wazoramu. Siku moja alipokuwa akiombaomba, alikanyagwa hadi kufa. Alma 30:59