Sura ya 51 Wayaredi Wanasafiri Kwenda Nchi ya Ahadi Wakati Wayaredi walipopiga hema ufukoni, kaka wa Yaredi alisahau kusali. Bwana alimjia katika wingu na kumwambia atubu. Etheri 2:14 Kaka wa Yaredi alitubu na alisali. Bwana alimsamehe kaka wa Yaredi lakini alisema lazima asitende dhambi tena. Etheri 2:15 Bwana alimwambia kaka wa Yaredi kutengeneza mashua ya kuwapeleka watu wake kwenda nchi ya ahadi. Etheri 2:16 Bwana alimwambia kaka wa Yaredi jinsi ya kutengeneza mashua. Etheri 2:16–17 Mashua zilikuwa hazipitishi hewa hivyo maji yasingeweza kuingia ndani. Etheri 2:17 Kaka wa Yaredi alijiuliza ni kwa vipi watu wangeweza kupumua ndani ya mashua. Alimuuliza Bwana ni nini alipaswa kufanya. Etheri 2:19 Bwana alimwambia kutengeneza shimo juu na chini ya kila mashua. Tundu lingeweza kufunuliwa na kuacha hewa kuingia na kufungwa kuziba maji yasiingie. Etheri 2:20 Kaka wa Yaredi alimwambia Bwana kwamba mashua zilikuwa na giza ndani. Bwana alimwambia kutafakari jinsi ya kuwa na mwanga ndani ya mashua. Etheri 2:22–23 Mwanga kwa ajili ya mashua usingeweza kutoka katika moto au madirisha kwa sababu yangevunjika. Etheri 2:23 Kaka wa Yaredi alikwenda mlimani na kuchonga mawe madogo 16 toka kwenye mwamba. Mawe yalionekana kama kioo safi. Alichonga mawe mawili kwa ajili ya kila mashua nane. Etheri 3:1 Kaka wa Yaredi alibeba mawe mpaka kwenye kilele cha mlima. Huko alisali kwa Bwana Etheri 3:1 Kaka wa Yaredi alimuomba Bwana kugusa mawe kwamba yatoe mwanga ndani ya mashua. Etheri 3:4 Bwana aligusa kila jiwe kwa kidole Chake. Etheri 3:6 Kwa sababu kaka wa Yaredi alikuwa na imani kubwa, aliona kidole cha Bwana. Kilionekana kama kidole cha mwanadamu. Etheri 3:6, 9 Kisha Bwana akijionyesha kwa kaka wa Yaredi. Etheri 3:13 Yesu alisema watu wanaomwamini watapata uzima wa milele. Etheri 3:14 Yesu alimfundisha na kumwonyesha kaka wa Yaredi vitu vingi. Yesu alimwambia kuviandika vile alivyoviona na kusikia. Etheri 3:25–27 Kaka wa Yaredi alibeba yale mawe kutoka mlimani. Aliweka jiwe moja katika kila mwisho wa mashua. Yalitoa mwanga ndani ya mashua. Etheri 6:2–3 Wayaredi waliingia katika mashua pamoja na wanyama na chakula. Bwana alisababisha upepo mkali kusukuma mashua kuelekea nchi ya ahadi. Etheri 6:4–5 Bwana aliwalinda katika bahari yenye dhoruba. Walimshukuru Bwana na kuimba sifa Kwake. Etheri 6:6–10 Baada ya siku 344 kwenye maji, mashua zilifika ufukoni mwa nchi ya ahadi. Etheri 6:11–12 Wakati Wayaredi walipotoka nje ya mashua, walipiga magoti na kulia machozi ya furaha. Etheri 6:12 Wayaredi walijenga miji na kupanda mazao katika nchi ya ahadi. Waliwafundisha watoto wao kumsikiliza Bwana na kutii maneno Yake. Etheri 6:13, 16–18