Sura ya 30 Alma Anawashauri Wanawe Alma hakuwa na furaha kwa sababu ya jinsi ambavyo Wanefi walikuwa wamekuwa waovu. Alizungumza na kila mmoja wa wanawe kuhusu kuishi kwa njia ya haki. Alma 35:15–16 Alma alimwambia Helamani, mwanawe mkubwa , amwamini Mungu. Alimwambia kuhusu malaika ambaye Mungu alikuwa amemtuma kumwambia Alma aache kuangamiza Kanisa. Alma 36:3, 6 Kwa siku tatu Alma alikuwa ameteseka kwa sababu ya majuto yake. Kisha akakumbuka mafundisho ya baba yake kuhusu Yesu, na akajua dhambi zake zingeweza kusamehewa. Alma 36:16–17 Alma alisali kwa ajili ya msamaha, na shangwe ilichukua nafasi ya uchungu katika nafsi yake. Alisamehewa kwa sababu alikuwa na imani katika Yesu Kristo na alikuwa ametubu. Alma 36:18–20 Kuanzia wakati huo Alma alikuwa amewafundisha wengine injili ili waweze kuhisi shangwe sawa na ile aliyokuwa amehisi. Mungu alikuwa amembariki Alma kwa sababu ya imani yake kwa Mungu. Alma 36:24, 27 Alma alimpa Helamani maandiko matakatifu na kumwambia aendelee kuandika historia ya watu wao. Alma 37:1–2 Alma alimwambia kwamba kama angetii amri, Mungu angembariki na kumsaidia kulinda maandiko hayo. Alma 37:13, 16 Alma pia alimwambia Helamani asali kila asubuhi na usiku na kuzungumza na Mungu kuhusu kila kitu alichokuwa akifanya ili Mungu aweze kumsaidia kwa kumuongoza. Alma 37:36–37 Alma alikuwa na furaha kwa ajili ya mwanawe Shibloni, ambaye alikuwa mmisionari jasiri kwa Wazoramu. Shibloni alikuwa amebaki mwaminifu hata wakati ambapo alikuwa amepigwa kwa mawe. Alma 38:3–4 Alma alimkumbusha Shibloni kwamba njia pekee ya kuokolewa ni kupitia kwa Yesu Kristo. Alma kisha akawatia moyo wanawe waendelee kufundisha injili. Alma 38:9–10 Koriantoni mwana wa Alma hakuwa ametii amri. Hakuwa mmisionari mwaminifu wakati alipokuwa akiwafundisha Wazoramu. Alma 39:2–3 Kwa sababu ya kile ambacho Koriantoni alikuwa amefanya, Wazoramu hawangeamini mahubiri ya Alma. Alma 39:11 Alma alimwambia Koriantoni kwamba watu hawawezi kuficha dhambi zao kwa Mungu na kwamba Koriantoni alihitaji kutubu. Alma 39:8–9 Alma aliwafundisha wanawe kwamba kila mtu atafufuliwa lakini ni wenye haki tu ndiyo watakaoishi na Mungu. Alma 40:9–10, 25–26 Maisha haya ni wakati wa watu kutubu na kumtumikia Mungu, Alma alisema. Alma 42:4 Akimkumbusha Koriantoni kwamba alikuwa ameitwa kuwa mmisionari, Alma alimwambia arudi kwa Wazoramu na kuwafundisha watu watubu. Alma 42:31 Alma na wanawe waliendelea kufundisha injili. Walifundisha kwa uwezo wa ukuhani. Alma 43:1–2