Sura ya 49 Mormoni na Mafundisho Yake Miaka mingi baada ya Yesu Kristo kuwatembelea Wanefi, kundi dogo la watu liliacha Kanisa na kujiita Walamani. 4 Nefi 1:20 Hatimaye karibu watu wote walikuwa waovu, wote Wanefi na Walamani. 4 Nefi 1:45 Mtu mwenye haki, Amaroni, alikuwa na kumbukumbu takatifu. Roho Mtakatifu alimwambia azifiche kwamba ziwe salama. 4 Nefi 1:48–49 Amaroni alimwambia Mormoni, mvulana wa miaka 10, wapi kumbukumbu zilikuwa zimefichwa. Amaroni alijua angeweza kumwamini Mormoni. Mormoni 1:2–3 Wakati alipokuwa na miaka 24, Mormoni aliweza kuchukua bamba za Nefi na kuandika kuhusu watu wake. Mormoni 1:3–4 Wakati Mormoni alipokuwa na miaka 11, vita ilianza kati ya Wanefi na walamani. Wanefi walishinda, na kulikuwa na amani tena. Mormoni 1:6, 8–12 Lakini Wanefi walikuwa waovu sana kwamba Bwana aliwachukua wanafunzi watatu, jambo ambalo lilihitimisha miujiza na uponyaji. Roho Mtakatifu hakuwaongoza tena watu. Mormoni 1:13–14 Wakati Mormoni alipokuwa na miaka 15 Yesu Kristo alimtembelea. Mormoni alijifunza zaidi kuhusu Mwokozi na wema Wake. Mormoni 1:15 Mormoni alitaka kuwafundisha watu, lakini Yesu alimwambia asifanye hivyo kwa sababu watu walikuwa waovu sana. Mioyo yao ilikuwa dhidi ya Mungu. Mormoni 1:16–17 Punde vita nyingine ilianza Mormoni alikuwa mkubwa na mwenye nguvu, na Wanefi walimchagua yeye kuongoza jeshi lao. Mormoni 2:1 Wanefi walipigana na Walamani kwa miaka mingi. Mormoni alijaribu kuwatia moyo watu wake kupigana kwa ajili ya familia na nyumba zao. Mormoni 2:23 Wanefi walikuwa waovu sana, kwamba Bwana asingewasaidia. Mormoni 2:26 Mormoni aliwaambia Wanefi wangelindwa kama tu wangetubu na kubatizwa. Lakini watu walikataa. Mormoni 3:2–3 Walijivuna kuhusu nguvu zao wenyewe, wakisema wangewauwa walamani wote. Kwa sababu ya uovu wa Wanefi, Mormoni alikataa kuwaongoza. Mormoni 3:9–11 Walamani walianza kuwashinda Wanefi katika kila vita. Mormoni aliamua kuliongoza jeshi tena. Mormoni 4:18; 5:1 Alijua Wanefi waovu wasingeshinda vita. Hawakutubu wala kusali kwa ajili ya msaada waliouhitaji. Mormoni 5:2 Mormoni alichukua kumbukumbu zote kutoka kwenye mlima ambapo Amaroni alikuwa amezificha na kuwaandikia watu ambao siku moja wangezisoma. Mormoni 4:23; 5:9, 12 Alitaka kila mtu, ikijumuisha Myahudi, kujua kuhusu Yesu Kristo, kutubu na kubatizwa, na kuishi injili na kubarikiwa. Mormoni 5:14; 7:8, 10 Roho alimtia msukumo Mormoni kuweka bamba ndogo za Nefi, ambazo zilikuwa zimebeba unabii wa kuja kwa Kristo, na bamba za Mormoni. Maneno ya Mormoni 1:3–7 Mormoni aliwaongoza Wanefi kwenye mji wa Kumora, ambapo walijiandaa kupigana na Walamani tena. Mormoni 6:4 Mormoni alikuwa akizeeka. Alijua hii ingekuwa vita ya mwisho. Hakutaka Walamani wazipate kumbukumbu takatifu na kuziharibu. Mormoni 6:6 Hivyo alimpa mwanawe Moroni, bamba za Mormoni, na kuficha bamba zilizobaki katika Mlima Kumora. Mormoni 6:6 Walamani waliwavamia Wanefi na kuwauwa wote isipokuwa Wanefi 24. Mormoni alikuwa amejeruhiwa. Mormoni 6:8–11 Mormoni alihuzunika kwamba Wanefi wengi walikuwa wamekufa, lakini alijua kuwa walikufa kwa sababu ya kumkataa Yesu. Mormoni 6:16–18 Mormoni alikuwa amejaribu kuwafundisha Wanefi ukweli. Alikuwa amewaambia jinsi gani ilikuwa muhimu kuwa na imani katika Yesu Kristo. Moroni 7:1, 33, 38 Alikuwa amejaribu kuwafundisha kuwa na tumaini kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo na kuwa na hisani, ambayo ni upendo msafi wa Kristo. Moroni 7:40–41, 47 Na mormoni alikuwa ameandika barua kwa mwanaye , Moroni, ambaye alikuwa amefundisha injili kwa Wanefi. Moroni 8:1–2 Mormoni aliandika barua kuhusu uovu wa kuogofya wa Wanefi. Alimwambia Moroni kubakia mwaminifu katika Yesu Kristo. Moroni 9:1, 20, 25 Walamani walimuua Mormoni na Wanefi wote isipokuwa Moroni aliyemalizia kuandika kumbukumbu. Mormoni 8:2–3