Sura ya 52 Kuangamizwa kwa Wayaredi Wayaredi waliongezeka kwa idadi na kuwa matajiri. Walimchagua mfalme kuwa kiongozi wao. Etheri 6:18, 22, 27–28 Miaka mingi ilipita, na Wayaredi wakawa waovu. Mungu aliwatuma manabii wawaambie watubu au la wangeangamizwa. Etheri 11:1 Watu hawakuwasikiliza manabii. Walijaribu kuwaangamiza. Etheri 11:2 Kulikuwa na vita na njaa katika nchi. Wayaredi wengi walifariki. Etheri 11:7 Mungu alimtuma nabii mwingine, aliyeitwa Etheri. Alihubiri kutoka asubuhi hadi jioni, akiwaambia Wayaredi wamwamini Mungu na kutubu. Etheri 12:2–3 Etheri aliwaambia Wayaredi kwamba kama wangemwamini Mungu, siku moja wangeishi na Baba wa Mbinguni katika ulimwengu bora. Etheri 12:4 Etheri aliwaambia Wayaredi vitu vingi muhimu, lakini hawakumuamini. Walimlazimisha aondoke mjini. Etheri 12:5; 13:13 Etheri alijificha pangoni mchana ili asije akauawa. Usiku alitoka na akajionea yaliyokuwa yakitendeka kwa Wayaredi. Etheri 13:13–14 Alimaliza kuandika historia ya Wayaredi akiwa mafichoni. Etheri 13:14 Bwana alimtuma Etheri kwa Koriantumuri, ambaye alikuwa mfalme muovu wa Wayaredi. Etheri alimwambia atubu au la angeishi kuona watu wake wote wakiangamizwa. Etheri 13:16–17, 20–21 Koriantumuri na watu wake hawakutubu. Alijaribu kusababisha kuuawa kwa Etheri, lakini Etheri alikimbia na kujificha pangoni. Etheri 13:22 Watu walikuwa waovu hadi Bwana akailaani nchi. Hawangeweza kuviweka vifaa au panga zao chini kwa sababu siku iliyofuata vitu hivyo vingekuwa havipo tena. Etheri 14:1 Wayaredi wote walipigana katika vita, ikijumuisha wanawake na watoto. Koriantumuri aliongoza jeshi moja na mwanaume aliyeitwa Shizi akaliongoza lingine. Etheri 14:19–20; 15:15 Koriantumuri na Shizi wote wawili walikuwa watu waovu. Roho Mtakatifu aliwaacha Wayaredi kwa sababu ya uovu wao. Shetani alikuwa na nguvu juu yao. Etheri 15:19 Wayaredi walipigana hadi Koriantumuri na Shizi wakawa ndio pekee waliobaki. Wakati Shizi alipozirai kwa kupoteza damu nyingi, Koriantumuri alikata kichwa chake. Etheri 15:29–30 Utabiri wa Etheri ulikuwa umetimizwa: Koriantumuri alikuwa Myaredi wa pekee aliyekuwa hai. Alivumbuliwa na watu wa Zarahemla. Omni 1:21 Etheri alimaliza kuandika historia ya Wayaredi. Walikuwa wameangamizwa kwa sababu ya uovu wao. Kumbukumbu za Wayaredi baadaye zilipatikana kupitia Wanefi. Etheri 15:33