Scripture Stories
Sura ya 8: Kuvuka Bahari


Sura ya 8

Kuvuka Bahari

Picha
familia ikipakia vitu

Bwana alimwambia Lehi kuibeba familia yake kwenye merikebu ambayo waliitengeneza. Waliijaza kwa matunda, nyama, na asali na mbegu za kupanda katika nchi ya ahadi.

Picha
Merikebu ikielea

Upepo mkali uliisukuma merikebu kuelekea nchi ya ahadi.

Picha
Lamani na Lemueli wanamfunga Nefi

Lamani, Lemueli, na baadhi ya wengine walianza kuwa waovu. Wakati Nefi alipowaambia kuacha uovu, walimkasirikia na wakamfunga kwa kamba.

Picha
Merikebu katika dhoruba

Kwa sababu ya uovu wao, Liahona iliacha kufanya kazi. Hawakujua ni upande upi wangeiongoza merikebu. Dhoruba kali ilisukuma merikebu kurudi nyuma kwa siku tatu.

Picha
Lehi na Saria

Lehi aliwaambia Lamani na Lemueli wamfungue Nefi, lakini hawakumsikiliza. Lehi na Saria walihuzunika sana mpaka kwamba wakaugua.

Picha
Watu wakibishana.

Mke na watoto wa Nefi walilia. Waliwaomba Lamani na Lemueli wamfungue Nefi, lakini walikataa.

Picha
Merikebu karibu kuzama

Katika siku ya nne dhoruba ilikuwa kali zaidi. Merikebu ilikuwa karibu kuzama.

Picha
Lamani na Lemueli

Lamani na Lemueli walijua kwamba Mungu ameruhusu dhoruba. Waliogopa kwamba wangezama.

Picha
Nefi na familia yake

Hatimaye Lamani na Lemueli walitubu na kumfungua Nefi. Japokuwa viwiko vyake na vifundo vilikuwa vimevimba na vyenye maumivu kutokana na kamba, Nefi hakunung’unika.

Picha
Nefi akishikilia Liahona

Kisha Nefi akaichukua Liahona, na ikafanya kazi tena. Nefi akasali, na upepo ukakoma. Bahari ikawa shwari.

Picha
Nefi akiiongoza merikebu

Nefi akaiongoza merikebu, na ikaelekea tena uelekeo wa nchi ya ahadi.

Chapisha