Sura ya 43 Yesu Kristo Anawatokea watu wa Nefi Wanefi wengi walikusanyika karibu na hekalu kule Neema. Walistaajabishwa na mabadiliko makuu nchini. 3 Nefi 11:1 Watu walikuwa wakizungumza kuhusu Yesu Kristo na ishara ya kifo chake. 3 Nefi 11:2 Wakiwa wanazungumza, walisikia sauti tulivu kutoka mbinguni. Ilisababisha mioyo yao kuwaka. 3 Nefi 11:3 Mara ya kwanza hawakuitambua sauti hiyo, lakini wakati ilipozungumza mara ya tatu, waliielewa. 3 Nefi 11:4–6 Sauti ilikuwa ya Baba wa Mbinguni. Ilimtambulisha Yesu Kristo na kuwaambia watu wamsikilize. 3 Nefi 11:7 Yesu Kristo alishuka chini kutoka mbinguni na kusimama miongoni mwa watu. Walikuwa na uwoga wa kuzungumza kwa maana hawakuelewa kilichokuwa kikitendeka. Walidhania Yesu alikuwa malaika. 3 Nefi 11:8 Aliwaambia kwamba alikuwa Yesu Kristo, ambaye manabii walisema atakuja. 3 Nefi 11:10 Yesu aliwaambia watu waje na waguse alama ubavuni mwake na katika mikono na miguu, ambapo alipigiliwa misumari msalabani. 3 Nefi 11:14 Yesu aliwataka watu wajue kwamba alikuwa Mungu wao na kwamba alikuwa amekufa kwa ajili ya dhambi zao. 3 Nefi 11:14 Mmoja baada ya mwingine watu waligusa alama ubavuni, mikononi, na miguuni mwa Yesu. Watu walifahamu kwamba alikuwa Mwokozi. 3 Nefi 11:15 Kisha watu walimsifu Yesu na kuinama miguuni mwake na kumwabudu. 3 Nefi 11:17 Yesu alimwita Nefi na watu wengine 11 waende kwake. Aliwapa nguvu za ukuhani na kuwafundisha njia sahihi ya kubatiza. 3 Nefi 11:18, 21–26; 12:1 Aliwaambia Wanefi wamwamini, watubu na watii amri. Kama hawangefanya hivyo, hawangeweza kuingia katika ufalme wake. 3 Nefi 12:19–20 Aliwafundisha Wanefi jinsi ya kuomba kwa Baba wa Mbinguni. Pia aliwafundisha kuhusu kufunga na akasema wangesamehewa kama wangesameheana. 3 Nefi 13:6–18 Baada ya kuwafundisha watu vitu vingi, Yesu aliwaambia waende nyumbani na kufikiria na kusali kuhusu kile alichokuwa amesema. 3 Nefi 17:1–3 Wanefi walianza kulia. Hawakutaka Yesu aondoke. 3 Nefi 17:5 Yesu aliwapenda Wanefi. Aliwaambia wawalete kwake watu waliokuwa wagonjwa au waliokuwa wameumia ili aweze kuwaponya. 3 Nefi 17:7 Yesu aliwaponya hawa watu. Kila mtu aliinama na kumwabudu. 3 Nefi 17:9–10