Scripture Stories
Sura ya 36: Hagothi


Sura ya 36

Hagothi

Picha
Wanefi wakisafiri

Takriban miaka 55 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, maelfu ya wanaume, wanawake, na watoto Wanefi waliondoka Zarahemla na kusafiri kaskazini.

Picha
Hagothi anajenga merikebu kubwa

Mmoja wao, mwanaume kwa jina Hagothi, alijenga merikebu kubwa na kuishusha kuelekea bahari ya magharibi.

Picha
Wanefi wakipakia merikebu kubwa

Wanefi wengi walichukua vyakula na vifaa na kung’oa nanga kuelekea kaskazini katika merikebu yake.

Picha
mashua juu ya maji

Hagothi kisha alijenga merikebu zingine ambazo ziliwasafirisha watu kwenda nchi iliyokuwa upande wa kaskazini. Merikebu ya kwanza ilirudi na kuwabeba hata watu wengi zaidi.

Picha
merikebu mbili majini

Merikebu nyingine moja iling’oa nanga. Hakuna merikebu yeyote ambayo ilirudi tena, na Wanefi hawakuwahi kufahamu kilichowatokea watu wale.

Chapisha