Scripture Stories
Sura ya 46: Yesu Kristo Anawafundisha na Kusali pamoja na Wanefi


Sura ya 46

Yesu Kristo Anawafundisha na Kusali pamoja na Wanefi

Picha
watu wakitembea usiku

Wanefi ambao walimuona Yesu Kristo waliwaambia rafiki zao angekuja tena siku iliyofuata. Watu wengi walifanya kazi sana kufika pale ambapo Yesu angekuwepo.

Picha
Watu wakisali

Asubuhi iliyofuata Nefi na wanafunzi wengine walilifundisha kundi ambalo lilikuwa limekusanyika. Wanafunzi kisha walisali kwamba wangeweza kupokea Roho Mtakatifu.

Picha
Wanafunzi wakibatizwa

Nefi alikwenda majini na akabatizwa. Kisha aliwabatiza wanafunzi wengine.

Picha
Malaika kutoka mbinguni

Baada ya kuwa wamebatizwa, wanafunzi walipokea Roho Mtakatifu. Moto ulionekana kuwazunguka, na malaika walishuka kutoka mbinguni na kuwahudumia.

Picha
Yesu na malaika

Wakati malaika wakiwa na wanafunzi, Yesu alikuja na kusimama miongoni mwao.

Picha
Wanefi wakisali

Kristo aliwaambia Wanefi wote kupiga magoti ardhini. Aliwaambia wanafunzi wake wasali.

Picha
Yesu akisali

Wakati wakisali, Yesu alikwenda mbali kidogo na watu na kupiga magoti na kusali kwa Baba wa Mbinguni.

Picha
Yesu akisali

Yesu alimshukuru Baba wa Mbinguni kwa kuwapa wanafunzi Roho Mtakatifu. Kisha aliomba kwa ajili ya Roho Mtakatifu kupewa kwa yoyote ambaye aliamini maneno ya wanafunzi.

Picha
Yesu akiwabariki wanafunzi

Yesu aliwabariki wanafunzi wake walipokuwa wakisali. Alitabasamu kwao, na walikuwa wenye kung’aa kama uso na nguo zake.

Picha
Yesu akisali pamoja na wanafunzi

Yesu alisali tena kwa ajili ya wanafunzi. Alifurahishwa na imani yao kuu.

Picha
Yesu akizungumza na watu

Kristo aliwaambia watu kuacha kusali lakini waendelee kusali katika mioyo yao. Kisha aliwapa sakramenti.

Picha
Yesu akibariki mkate

Hakuna yoyote aliyekuwa ameleta mkate au divai, lakini Mwokozi alivileta kimiujiza.

Picha
Joseph Smith ameshikilia maandiko

Yesu Kristo aliwaambia Wanefi kwamba injili yake ingeletwa tena duniani katika siku za mwisho.

Picha
Kristo akizungumza na Nefi

Aliwaambia wajifunze maandiko, na alimwambia Nefi aandike katika kumbukumbu utimizwaji wa sehemu za unabii zilizobaki za Samueli Mlamani.

Picha
Yesu akifundisha kutoka kwenye maandiko

Kisha Yesu alifundisha watu kutoka kwenye maandiko. Aliwaambia kufundishana vitu ambavyo aliwafundisha.

Picha
Nefi akibatiza

Yesu alirudi mbinguni, na wanafunzi wake waliwafundisha watu. Wale walioamini walibatizwa na kupokea Roho Mtakatifu.

Picha
Wanefi wakibeba maboga

Wanefi walianza kutii amri zote.

Chapisha