Sura ya 33
Watu wa Mfalme dhidi ya Watu Huru
Baadhi ya Wanefi walimtaka mwamuzi mkuu, Pahorani, kubadili baadhi ya sheria.
Wakati Pahorani alipokataa, watu walimkasirikia na wakataka kumuondoa Pahorani kama mwamuzi mkuu. Walitaka kuwa na mfalme, na si waamuzi.
Wakijiita watu wa mfalme, walitumaini kwamba mmoja wao angekuwa mfalme na kuwa na nguvu juu ya watu.
Watu waliokuwa wakimtaka Pahorani kama mwamuzi mkuu waliitwa watu huru. Walitaka kuwa huru kuishi na kuabudu kama wapendavyo.
Watu walipiga kura kati ya watu huru na watu wa mfalme. Wengi wao walipigia kura upande wa watu huru.
Wakati huohuo, Amalikia alikuwa akikusanya jeshi kubwa la Walamani kuwashambulia Wanefi.
Wakati watu wa mfalme waliposikia kwamba Walamani wanakuja, walifurahia na wakakataa kuilinda nchi yao.
Kapteni Moroni aliwakasirikia watu wa mfalme kwa kutopigana. Alikuwa amefanya kazi sana kuwaweka Wanefi kuwa huru.
Alimuomba gavana mamlaka ya kuwafanya watu wa mfalme wapigane na Walamani au wauwawe.
Wakati Gavana, Pahorani, alipompa Moroni mamlaka haya, Moroni aliliongoza jeshi lake dhidi ya watu wa mfalme.
Wengi wa Watu wa mfalme waliuwawa; baadhi wakafungwa gerezani. Waliobaki walikubali kusaidia kuilinda nchi yao dhidi ya Walamani.