Sura ya 32 Kapteni Moroni na Bendera ya Uhuru Mtu mwovu aliyeitwa Amalikia alitaka kuwa mfalme wa Wanefi. Wanefi wengi waliacha Kanisa kumfuata. Alma 46:1, 4–5, 7 Kama Amalikia angekuwa mfalme, angejaribu kuharibu Kanisa la Mungu na kuchukua uhuru wa watu. Alma 46:9–10 Wakati Kapteni Moroni, kiongozi wa majeshi ya Wanefi, aliposikia juu ya mpango wa Amalikia kuwa mfalme, alikasirika. Alma 46:11 Moroni alichana koti kutengeneza bendera. Juu yake aliandika ujumbe kuwakumbusha watu kulinda dini, uhuru, na amani yao. Alma 46:12 Moroni aliweka bendera kwenye mlingoti na kuiita bendera ya uhuru. Kisha alivaa vazi lake la kivita, akapiga magoti kusali. Alma 46:13 Alimuomba Mungu kuwalinda wale walioamini katika Yesu Kristo na kusali kwa ajili ya uhuru katika nchi, wakiiita nchi ya uhuru. Alma 46:16–18 Moroni alienda kati ya watu. Akipeperusha bendera, aliwaita kuja na kusaidia kuulinda uhuru. Alma 46:19–20 Watu walikuja kutoka kila sehemu zote za nchi. Waliahidi kutii amri za Mungu na kupigana kwa ajili ya uhuru. Alma 46:21–22, 28 Wakati Amalikia alipoona jinsi Wanefi walivyojiunga na Moroni, aliogopa. Yeye na wafuasi wake walikwenda kuungana na Walamani. Alma 46:29–30 Moroni na jeshi lake walijaribu kuwazuia, lakini Amalikia na baadhi ya wafuasi wake walitoroka. Alma 46:31–33 Moroni aliweka bendera ya uhuru katika kila mnara katika nchi ya Wanefi. Wanefi walikuwa na uhuru wao tena na amani. Alma 46:36–37