Hadithi za Maandiko
Watu wa Kujua


Watu wa Kujua

HaruniMwana wa Mfalme Mosia na mmisionari kwa Walamani

AbinadiNabii aliyetumwa kumfundisha Mfalme Nuhu, ambaye alisababisha Abinadi kuuwawa kwa kuchomwa moto

AdamuMtu wa kwanza duniani

AlmaKuhani wa mfalme Nuhu ambaye aliamini mafundisho ya Abinadi na baadaye alikuwa kiongozi wa Kanisa

Alma MdogoMwana wa Alma ambaye aliasi na kujaribu kuharibu Kanisa lakini alipata badiliko la moyo na alianza kufundisha injili. Alikuja kuwa kiongozi wa Kanisa na mwamuzi mkuu wa kwanza.

AmalikiaMtu mwovu aliyetaka kuwa mfalme wa Wanefi lakini ambaye angechukua uhuru wa watu. Wakati aliposhindwa kuwa mfalme, aliondoka na kujiunga na Walamani.

AmlisiMtu mwovu aliyetaka kuwa mfalme wa Wanefi. Wakati alipokataliwa kuwa malme, yeye pamoja na wafuasi wake waliondoka, waliwashambulia Wanefi, na kisha walijiunga na Walamani.

WaamlisiWafuasi wa amlisi. Walijichora kwa alama nyekundu kwenye mapaji ya nyuso zao na walijiungana Walamani.

AmaroniMtu mwenye haki ambaye alimpa Mormoni kumbukumbu kwamba ziwe salama.

Amoni1Kiongozi wa kikundi cha Wanefi kutoka Zarahemla waliokwenda kwenye nchi ya Nefi na kuwasaidia Wanefi waliokuwa huko kutoroka

Amoni2Mmoja kati ya wana wa Mosia waliolinda mifugo ya mfalme Lamoni dhidi ya wezi. Alifundisha na kuwaongoa wengi wa Walamani wakati wa umisionari wake.

Watu wa AmoniWalamani walioongoka kutokana na wana wa Mosia. Walizika silaha zao za kivita na kuweka agano kamwe kutopigana tena

AmulekiMmisionari mwenza wa Alma Mdogo. Walifungwa gerezani lakini walitumia nguvu za Mungu kufanya kuta za gereza kuanguka.

AmuloniKuhani mwovu wa Mfalme Nuhu ambaye alifanywa mtawala juu ya watu wa Alma. Aliwafanya wafanye kazi sana na alitishia kumuua yoyote aliyekamatwa akisali.

Anti-Nefi–Lehi(ona Watu wa, Amoni)

Mfalme, BenyaminiMfalme mwenye haki aliyesimama kwenye mnara kuwafundisha watu wake kuhusu Yesu Kristo

Kaka wa YarediNabii aliyemuomba Yesu kugusa mawe 16 ili kwamba yatoe mwanga katika mashua ambazo Wayaredi walitumia kusafiri kwenda nchi ya ahadi

KoriantoniMwana wa Alma Mdogo ambaye hakuwa mmisionari mwaminifu na mwenye haki

KoriantumuriMfalme mwovu ambaye alikuwa Myaredi wa mwisho kuishi

EnoshiMwana wa Yakobo ambaye alisali siku nzima na usiku. Alisali kwa ajili ya Wanefi na Walamani.

EtheriNabii ambaye aliwaonya Wayaredi watubu na aliandika kuhusu kuangamizwa kwao

HawaMwanamke wa kwanza duniani

Watu huruWanefi waliotaka uhuru wa kuishi na kuabudu wapendavyo. Walitawaliwa na waamuzi, na si mfalme.

GideoniMnefi mwenye haki ambaye alilinda Kanisa wakati Nehori alipoanza kufundisha uongo kwa watu. Nehori alimuua.

HagothiMnefi mtengeneza meli ambaye alichukua wengi wa Wanefi kwenda katika nchi iliyokuwa kaskazini

HelamaniMwana mkubwa wa Alma Mdogo. Alipewa bamba na kuambiwa kuandika historia ya watu wake. Pia alikuwa kiongozi wa vijana mashujaa 2,000.

Himni Mwana wa Mfalme Mosia na mmisionari kwa Walamani

IshmaeliMtu kutoka Yerusalemu ambaye alisafiri kwenda nchi ya ahadi pamoja na familia ya Lehi. Binti zake waliolewa na wana wa Lehi.

YakoboMwana wa Lehi na Saria. Alikabiliana na Sheremu, ambaye alisema Kristo hayupo.

WayarediWaliomfuata Yaredi na kaka yake ambao waliondoka Babeli na kusafiri kwenda nchi ya ahadi kwa mashua

YusufuMwana mwenye haki wa Lehi na Saria ambaye alizaliwa nyikani

Joseph Smith, Mdogo.Nabii wa siku za mwisho ambaye alitafsiri Kitabu cha Mormoni kutoka kwenye bamba za dhahabu

Watu wa mfalmeWanefi ambao walitaka kutawaliwa na mfalme na si waamuzi. Wakati waliposhindwa kuwa na mfalme, walijiunga na Walamani na kuwashambulia Wanefi.

KorihoriMtu mwovu aliyetaka ishara kuthibitisha kwamba Mungu anaishi. Mungu alimpa Korihori ishara kwa kuchukua sauti yake.

LabaniMtu mwovu huko Yerusalemu ambaye hakutaka kuwapa wana wa Lehi bamba za shaba.

LamaniMwana mkubwa wa Lehi na Saria. Alimkuwa mwovu na mkaidi dhidi ya Mungu.

Lamani, MfalmeMfalme mwovu wa Walamani ambaye alimpa Zenivu na Wanefi waliomfuata miji miwili lakini kisha aliwavamia

WalamaniUzao au wafuasi wa Lamani na Lemueli au watu ambao walikataa injili

Lamoni, MfalmeMfalme wa Walamani ambaye alifundishwa injili na aliiamini. Amoni2 alilinda mifugo ya mfalme dhidi ya wezi.

Lamoni, baba wa MfalmeMfalme wa Walamani ambaye alifundishwa injili na aliiamini. Alisema angetubu dhambi zake zote ili kumjua Mungu.

Lehi1Nabii ambaye alionya kwamba Yesrusalemu ingeangamizwa. Alisikiliza wakati Mungu alipomwambia kuichukua familia yake kwenda nyikani.

Lehi2mwana wa Helamani. Yeye pamoja na kaka yake, Nefi, walitupwa gerezani na kuzungukwa na moto.

LemueliMwana mwovu wa Lehi na Saria

Limhi, MfalmeMwana mwema wa Nuhu Mfalme mwovu. Yeye na watu wake walikuwa watumwa wa Walamani lakini walitoroka

Mariamumama yake Yesu

MormoniKiongozi wa jeshi la Wanefi na mmoja wa nabii wa mwisho wa Wanefi. Alikiweka pamoja Kitabu cha Mormoni.

MoroniMwana wa Mormoni na nabii wa mwisho wa Wanefi. Alifukia bamba za dhahabu na baadae alimtokea Joseph smith kama malaika.

Moroni, KapteniKiongozi mwenye haki wa jeshi la Wanefi. Alitengeneza bendera ya uhuru na kuliambia jeshi lake kupigania uhuru wao.

Mosia, MfalmeMfalme wa mwisho wa wanefi. Alikuwa na wana wanne.

NehoriMtu mwovu aliyepinga kwa ujasiri Kanisa la Mungu. Alimuua Gideoni na yeye aliuwawa.

Nefi1Mwana mwenye haki wa Lehi na Saria. Alipata bamba za shaba kutoka kwa Labani na kutengeneza meli ambayo ilibeba familia yake kwenda nchi ya ahadi.

Nefi2mwana wa Helamani. Yeye na kaka yake, Lehi, walitupwa gerezani na walizungukwa na moto. Nefi alisababaisha baa la njaa ili kuwafundisha watu watubu.

Nefi3Mtu mwenye haki aliyechaguliwa na Yesu Kristo kuwa mwanafunzi na kiongozi wa Kanisa

WanefiWafuasi wa Nefi au watu walikubali injili

Nuhu, MfalmeMfalme mwovu wa Wanefi ambaye alipenda utajiri na aliwafundisha watu wake kuwa waovu. Watu wake mwenyewe walimuua kwa kumchoma moto.

OmneriMwana wa Mfalme Mosia na mmisionari kwa Walamani

PahoraniMwamuzi mkuu wa Wanefi ambaye alimsaidia Kapteni Moroni kuwashinda wanefi waovu

SamuMwana mwenye haki wa Lehi na Saria

Samueli MlamaniNabii ambaye alitoa unabii kwa wanefi kuhusu ishara za kuzaliwa na za kufa kwa Yesu Kristo

SariaLehi1 mke wa

SeantumuKaka wa Seezoramu na aliyemuua Seezoramu

SeezoramuMwamuzi mkuu ambaye aliuwawa na kaka yake

SheremuMnefi mwovu aliyetaka ishara kwanza kabla ya kuamini katika Yesu Kristo

ShiziMyaredi mwovu ambaye aliongoza jeshi dhidi ya Koriantumuri na alikuwa ni mmoja wa Wayaredi wa mwisho kuishi

Wana wa MosiaWana wa Mosia: Haruni, Amoni,2 Himni, na Omneri, ambao walikuwa wamisionari thabiti kwa Walamani

Vijana mashujaa elfu mbiliJeshi la vijana wa Amoni liliongozwa na Helamani. Walipigana ili kwamba wazazi wao, waliokuwa wameingia kwenye la agano kutopigana, wasipigane.

ZeezromuMwanasheria ambaye alimuahidi Amuleki fedha ili kusema kwamba Mungu hayupo. Alma Mdogo alimfundisha injili, na alitubu

ZenivuKiongozi mwenye haki ambaye alichukua kundi la Wanefi kutoka Zarahemla kwenda nchi ya Nefi, ambapo waliwekwa utumwani na Lamani Mfalme mwovu

ZerahemnaKingozi wa Walamani ambaye alipigana na Wanefi na alitaka Wanefi wawe watumwa wake. Alikatwa ngozi ya juu ya kichwa katika vita dhidi ya jeshi la Kapateni Moroni.

ZoramuMtumishi wa Labani ambaye alisafiri na familia ya Lehi kwenda nchi ya ahadi

WazoramuWatu waovu ambao mwanzo walikuwa watu wa kanisa la Mungu. Walisali ndani ya masinagogi wakisimama kwenye jukwaa lilioitwa Rameumtomu.