Scripture Stories
Sura ya 4: Bamba za Shaba


Sura ya 4

Bamba za Shaba

Picha
Lehi akizungumza na Nefi

Lehi alimwambia Nefi kwamba Bwana aliwataka yeye na kaka zake kurudi Yerusalemu. Walitakiwa kupata bamba za shaba kutoka kwa mtu aitwaye Labani

Picha
bamba za shaba

Bamba za shaba zilikuwa ni kumbukumbu muhimu . Zilizungumzia kuhusu mababu wa Lehi na zilikuwa na maneno ya Mungu yaliyofunuliwa kupitia manabii.

Picha
Lamani na Lemueli

Lamani na Lemueli hawakutaka kurudi kuchukua Bamba za shaba. Walisema ingekuwa ni vigumu sana kufanya hivyo. Hawakuwa na imani katika Bwana.

Picha
Lehi akiongea na Nefi

Nefi alitaka kumtii Bwana Alijua Bwana angemsaidia yeye na kaka zake kupata bamba za shaba kutoka kwa Labani.

Picha
Lamani, Lemueli, Samu na Nefi

Lamani, Lemueli, Samu na Nefi walisafiri kurudi Yerusalemu kufuata bamba za shaba

Picha
Lamani akiongea na Labani

Lamani alikwenda kwa Labani

Picha
Lamani akikimbia

Labani alikasirika na hangempa Lamani bamba za shaba. Labani alitaka kumuua Lamani, lakini Lamani alitoroka

Picha
Lamani akiongea na kaka zake

Lamani aliwaambia kaka zake kilichotokea. Alikuwa akiogopa na alitaka kukata tamaa na kurudi kwa baba yao nyikani.

Picha
Nefi akionge na kaka zake

Nefi alisema wasingeweza kurudi bila bamba za shaba. Aliwaambia kaka zake wawe na imani zaidi katika Bwana na wangeweza kupata bamba za shaba.

Picha
Wakikusanya dhahabu

Nefi na kaka zake walikwenda kwenye mji wao wa zamani huko Yerusalemu na kukusanya dhahabu yao na fedha ili kubadilishana kupata bamba.

Picha
Wakimwonyesha Labani dhahabu

Walimwonyesha Labani utajiri wao na kumuomba kubadilishana kwa bamba. Wakati Labani alipoiona dhahabu yao na fedha, aliitaka kwa ajili yake mwenyewe na akawafukuza nje.

Picha
Labani akionyesha

Labani Aliwaambia watu wake kuwaua wana wa Lehi Nefi na kaka zake walikimbia na kujificha pangoni. Labani aliichukua dhahabu yao na fedha.

Picha
Lamani na Lemueli wakiwapiga Nefi na Samu

Lamani na Lemueli walimkasirikia Nefi. Waliwapiga Nefi na Samu kwa fimbo.

Picha
Malaika akitokea

Malaika akawatokea na kuwaambia Lamani na Lemueli kuacha kuwapiga. Aliwaambia Bwana angewasaidia wao kupata bamba. Pia alisema kwamba Nefi angekuwa kiongozi juu ya kaka zake.

Picha
Nefi akionge na kaka zake

Nefi aliwaambia kaka zake kuwa na imani katika Bwana na kutomwogopa Labani na watu wake. Nefi aliwatia moyo kaka zake kurudi tena Yerusalemu

Picha
Nefi na kaka zake wakijificha

Usiku ule kaka zake Nefi walijificha nje ya ukuta wa mji wakati Nefi akijipenyeza ndani kwa kunyatia. Alitembea kuelekea nyumba ya Labani.

Picha
Labani akiwa amelewa

Wakati Nefi alipofika karibu na nyumba ya Labani, alimuona mtu amelala chini akiwa amelewa. Alikuwa ni Labani

Picha
Nefi akiuchukua upanga wa Labani

Nefi aliuona upanga wa Labani na kuuchukua. Roho mtakatifu alimwambia Nefi amuue Labani, lakini Nefi hakutaka kumuua.

Picha
Nefi akimuua Labani

Roho Mtakatifu alimwambia Nefi tena kumuua Labani ili kwamba Nefi aweze kupata bamba za dhahabu. Familia ya Lehi walihitaji bamba ili kwamba waweze kujifunza injili.

Picha
Nefi katika mavazi ya Labani

Nefi alimtii Roho Mtakatifu na alimuua Labani. Kisha Nefi akavaa mavazi na vazi la kivita la Labani.

Picha
Nefi akijifanya ni Labani

Nefi alikwenda ndani ya nyumba ya Labani na alikutana na Zoramu, mtumishi wa Labani. Nefi alionekana na kuongea kama Labani

Picha
Nefi na Zoramu

Alimwambia Zoramu alete bamba za shaba. Zoramu alidhani Nefi ni Labani, hivyo akampa mabamba. Nefi alimwambia Zoramu amfuate.

Picha
Nefi na Zoramu

Lamani, Lemueli, na Samu walimuona Nefi akija na waliogopa; walidhani alikuwa ni Labani. Walianza kukimbia lakini walisimama wakati Nefi alipowaita.

Picha
Nefi na Zoramu

Kisha Zoramu akatambua kwamba Nefi hakuwa Labani, na alijaribu kukimbia. Nefi alimkamata Zoramu na kumuahidi kutomdhuru kama angeenda nao nyikani.

Picha
Zoramu na kaka zake Nefi

Zoramu alikubali. Nefi pamoja na kaka zake walimchukua Zoramu na bamba za shaba na kurudi kwa Lehi na Saria.

Picha
Lehi na Saria wakifurahi

Walimpa Lehi bamba za shaba Yeye na Saria walikuwa na furaha wana wao walikuwa salama. Wote walifurahi na kumshukuru Mungu

Picha
Lehi akiwasomea wana wake

Lehi akisoma bamba za dhahabu. Zilizungumzia kuhusu Adamu na Hawa na Uumbaji wa dunia. Zilikuwa na maneno ya manabii wengi.

Picha
Lehi na Nefi

Lehi na Nefi walifurahi kwa sababu walikuwa wametii amri ya Bwana na walikuwa wameweza kupata bamba za dhahabu.

Picha
Lehi akifungasha bamba

Lehi na familia yake walibeba bamba za dhahabu pamoja nao safarini ili kwamba waweze kuwafundisha watoto wao amri zilizoandikwa kwenye bamba.

Chapisha