Sura ya 6 Ndoto ya Lehi Lehi aliiambia familia yake kuhusu ono muhimu alilokuwa ameona katika ndoto. Ndoto ya Lehi ilimpa furaha kwa ajili ya Nefi na Samu lakini ikampa huzuni kwa ajili ya Lamani na Lemueli. 1 Nefi 8:2–4 Katika ndoto yake Lehi alimuona mwanaume akiwa amevalia joho jeupe ambaye alimwambia Lehi amfuate. Lehi alimfuata mwanaume huyo katika nyika yenye giza na yenye kuhuzunisha. 1 Nefi 8:5–7 Baada ya kusafiri gizani kwa masaa mengi, Lehi alisali kwa ajili ya msaada. 1 Nefi 8:8 Kisha akaona mti wenye tunda jeupe. Tunda hili tamu liliwafanya waliolila kuwa wenye furaha. 1 Nefi 8:9–10 Lehi alikula tunda, na lilimjaza na shangwe. Alitaka familia yake ionje tunda kwa sababu alijua lingewafanya wawe na furaha pia. 1 Nefi 8:11–12 Lehi aliona mto ukitiririka kando ya mti. Mwishoni mwa mto aliwaona Saria, Samu, na Nefi. 1 Nefi 8:13–14 Lehi aliwaita mkewe na wanawe waje na waonje lile tunda. Saria, Samu, na Nefi walienda na kuonja tunda, lakini Lamani na Lemueli walikataa. 1 Nefi 8:15–18 Lehi pia aliona fimbo ya chuma na njia nyembamba na iliyosonga ikielekea kwenye mti. 1 Nefi 8:19–20 Aliwaona watu wengi wakitembea kwenye njia au kuelekea kwenye njia. Kwa sababu ya ukungu wa giza, wengine walitangatanga kutoka kwenye njia na wakapotea. 1 Nefi 8:21–23 Wengine walishikilia kwa nguvu fimbo ya chuma na kuongozwa kwa usalama kupita kwenye giza hadi kuufikia mti. Walionja tunda. 1 Nefi 8:24 Watu waliokuwa ndani ya jengo pana kwenye ng’ambo nyingine ya mto waliwafanyia mzaha wale waliokuwa wakila tunda. Wengine ambao walikuwa wamekula tunda waliaibika na kuondoka kutoka kwenye mti. 1 Nefi 8:26–28 Lehi aliwaona watu wengi katika ndoto yake. Baadhi walishikilia kwa nguvu fimbo ya chuma na kuongozwa kupita kwenye giza hadi kuufikia mti. Walionja tunda. Wengine walienda kwenye lile jengo kubwa au walizama ndani ya mto au wakapotea. Lamani na Lemueli walikataa kula tunda. Lehi alikuwa na wasiwasi juu yao na alijaribu kuwasaidia kutii amri za Mungu. 1 Nefi 8:30–38