Sura ya 26 Watu wa Amoni Wana wa Mosia walifundisha injili kwa Walamani. Maelfu ya Walamani walitubu na kujiunga na Kanisa. Alma 23:4–5 Walamani waliojiunga na Kanisa walijiita Wa Anti-Nefi-Lehi, au watu wa Amoni. Walikuwa wema, wenye juhudi katika kazi. Alma 23:17–18; 27:26 Walamani ambao hawakutubu waliwakasirikia watu wa Amoni na wakajiandaa kupigana nao. Alma 24:1–2 Watu wa Amoni walijua kwamba Walamani waovu wangekuja kuwauwa lakini walichagua kutopigana nao. Walikuwa wametubu kuua. Alma 24:5–6 Walizika silaha zao chini ardhini na kumuahidi Mungu kamwe hawangeua tena. Alma 24:17–18 Wakati Walamani waovu walipokuja na kuanza kuwauwa, waliinama ardhini na kusali. Alma 24:21 Kwa kuona kwamba watu wa Amoni hawangepigana na wao, wengi wa Walamani waovu waliacha kuwauwa. Alma 24:23–24 Walamani walijisikia vibaya kwamba walikuwa wameua. Walitupa chini silaha zao na kujiunga na watu wa Amoni. Hawangepigana tena. Alma 24:24–27 Walamani zaidi walikuja kuwauwa watu wa Amoni. Lakini bado hawakupigana nao, na wengi waliuwawa. Alma 27:2–3 Kwa kutaka watu aliowapenda wasiuwawe, Amoni alisali kwa ajili ya msaada. Bwana alimwambia kuwachukua watu wake kutoka kwenye nchi. Alma 27:4–5, 10–12 Wanefi huko Zarahemla walimpa Amoni na watu wake nchi ya Jershoni na kuwalinda. Walikuwa marafiki. Alma 27:22–23