Sura ya 17 Alma na Watu Wake Wanatoroka Siku moja wakati watu wa Alma walipokuwa wakifanya kazi katika mashamba yao, jeshi la Walamani lilivuka mpaka na kuingia nchini mwao. Mosia 23:25 Wanefi waliogopa na kukimbilia mjini kwa ajili ya usalama. Alma aliwaambia wamkumbuke Mungu na angewasaidia. Wanefi walianza kusali. Mosia 23:26–28 Bwana alilainisha mioyo ya Walamani, na hawakuwadhuru Wanefi. Walamani walikuwa wamepotea walipokuwa wakijaribu kuwatafuta watu wa Mfalme Limhi. Mosia 23:29–30 Walamani walimwahidi Alma ya kwamba hawangewasumbua watu wake kama angewaonyesha njia ya kurudi nchini kwao. Alma aliwaonyesha njia. Mosia 23:36 Lakini Walamani hawakutunza ahadi yao. Waliweka walinzi kuzunguka sehemu hiyo, na Alma na watu wake hawakuwa huru tena. Mosia 23:37 Mfalme Mlamani alimfanya Amuloni kuwa kiongozi wa watu wa Alma. Amuloni alikuwa Mnefi na kuhani mwovu wa Mfalme Nuhu. Mosia 23:39; 24:8–9 Amuloni aliwasababisha watu wa Alma kufanya kazi kwa bidii sana. Walisali kwa ajili ya msaada, lakini Amuloni alisema kwamba mtu yeyote ambaye angepatikana akisali angeuawa. Watu waliendelea kusali mioyoni mwao. Mosia 24:10–12 Mungu alisikia sala zao na kuwaimarisha watu hivyo kazi yao ikaonekana kuwa rahisi. Watu walikuwa wenye furaha na wenye subira. Mosia 24:14–15 Mungu alifurahia kwamba watu walikuwa waaminifu. Alimwambia Alma kwamba angewasaidia kutoroka kutoka kwa Walamani. Mosia 24:16–17 Wakati wa usiku watu walikusanya vyakula na mifugo. Asubuhi iliyofuata Mungu alizidisha usingizi wa Walamani wakati Alma na watu wake walipokuwa wakitoroka mjini. Mosia 24:18–20 Baada ya kusafiri kwa siku 12, watu waliwasili Zarahemla, ambapo Mfalme Mosia na watu wake waliwakaribisha. Mosia 24:25