Scripture Stories
Sura ya 7: Kujenga Merikebu


Sura ya 7

Kujenga Merikebu

Picha
Nefi

Baada ya familia ya Lehi kupiga kambi kwa siku nyingi ufukoni mwa bahari, Bwana aliongea na Nefi. Alimwambia ajenge merikebu ya kuwabeba familia yake kwenda nchi ya ahadi.

Picha
Nefi akitengeneza zana

Nefi hakujua jinsi ya kujenga merikebu, lakini Bwana alimwambia angemwonyesha. Alimwambia Nefi wapi pa kupata metali ili kutengeneza zana ambazo angehitaji

Picha
Lamani na Lemueli wakiwa na Nefi

Lamani na Lemueli walimcheka Nefi kwa kutaka kujenga merikebu. Hawakuamini kwamba Bwana angemwonyesha Nefi jinsi ya kuijenga. Walikataa kumsaidia.

Picha
Nefi akizungumza na Lamani na Lemueli

Nefi aliwaambia Lamani na Lemueli kutubu na wasiwe wakaidi. Aliwakumbusha wao kwamba walikuwa wamemuona malaika. Pia aliwaambia wao kwamba Mungu ana nguvu ya kufanya vitu vyote.

Picha
Lamani na Lemueli wanataka kumtupa Nefi baharini

Lamani na Lemueli walimkasirikia Nefi na wakataka kumtupa baharini.

Picha
Nefi akiwa na Lamani na Lemueli

Wakati walipokuwa wakimkaribia Nefi, aliwaamuru wasimguse kwa sababu alikuwa amejazwa na nguvu za Mungu. Lamani na Lemueli waliogopa kwa siku nyingi.

Picha
Lamani na Lemueli wakiangukia migongo

Kisha Bwana akamwambia Nefi awaguse Lamani na Lemueli. Nefi alipofanya hivyo, Bwana aliwatikisa. Lamani na Lemueli walijua Nefi alikuwa na nguvu za Mungu.

Picha
Nefi

Nefi aliwaambia Lamani na Lemueli wawatii wazazi wao na wamtii Mungu. Nefi alisema kama wangefanya hivi, wangebarikiwa.

Picha
Lamani na Lemueli wakijenga merikebu

Lamani na Lemueli walitubu na wakamsaidia Nefi kujenga merikebu.

Picha
Nefi akisali

Nefi alikwenda mlimani mara nyingi kusali kwa ajili ya msaada. Bwana alimfundisha jinsi ya kujenga merikebu.

Picha
Merikebu iliyokamilika

Wakati Nefi na kaka zake walipokuwa wamekamilisha kujenga merikebu, walijua ilikuwa ni merikebu nzuri. Walimshukuru Mungu kwa kuwasaidia.

Chapisha