Scripture Stories
Sura ya 24: Amoni anakutana na Baba wa Mfalme Lamoni


Sura ya 24

Amoni anakutana na Baba wa Mfalme Lamoni

Picha
Lamoni akiongea na Amoni

Mfalme Lamoni alitaka kumpeleka Amoni kukutana na baba yake. Bwana alimuonya Amoni asiende kwa sababu baba wa Lamoni angejaribu kumuua.

Picha
Amoni na Lamoni

Bwana alimwambia Amoni badala yake kwenda katika nchi ya Midoni, ambapo Haruni kaka yake alikuwa gerezani. Mfalme Lamoni alikwenda na Amoni.

Picha
Amoni na Lamoni wakiwa na baba yake Lamoni.

Wakati wakisafiri walikutana na baba yake Mfalme Lamoni, ambaye alikuwa mfalme katika nchi nzima. Alimuuliza Lamoni wapi alikuwa akienda na Mnefi mdanganyifu.

Picha
Lamoni, Amoni na baba wa Lamoni

Mfalme Lamoni alimwambia baba yake kuhusu Amoni na kaka yake aliyekuwa gerezani. Kwa hasira, baba yake Lamoni aliamuru Lamoni amuue Amoni na kurudi Midoni.

Picha
Baba wa Lamoni akijaribu kumuua Lamoni

Lamoni alikataa kumuua amoni na alisema yeye na amoni walikuwa wakienda kumtoa Haruni gerezani. Baba yake Lamoni alikasirika zaidi na akatoa upanga ili kumuua Lamoni.

Picha
Amoni akimjeruhi baba wa Lamoni

Amoni alisonga mbele na kumlinda Lamoni. Baba wa Lamoni kisha alijaribu kumuua Amoni, lakini alijilinda na akajeruhi mkono wa baba wa Lamoni.

Picha
Amoni na baba wa Lamoni

Wakati baba wa Lamoni alipoona kwamba Amoni angemuua, alimuahidi Amoni nusu ya ufalme wake kama angemwacha hai.

Picha
Amoni akiongea na baba wa Lamoni

Amoni alisema alitaka Haruni na wenzake waachiliwe huru kutoka gerezani na alitaka Lamoni abakie na ufalme wake.

Picha
Amoni akimfunga kidonda mfalme

Baba wa Lamoni alitambua kwamba Amoni hakutaka kumuumiza. Alishangazwa na jinsi gani Amoni alivyompenda mtoto wake. Alimwalika Amoni amfundishe injili.

Picha
Mfalme Lamoni akiongea na mfalme wa Midoni

Amoni na Mfalme Lamoni walikwenda Midoni. Lamoni aliongea na mfalme wa huko, na Haruni na wenzake waliachiliwa kutoka gerezani.

Picha
Haruni na wenzake wakiachiliwa

Amoni alikuwa na huzuni kuwaona jinsi kwa duni walivyotendewa. Walikuwa wameteseka kwa mengi lakini walikuwa wavumilivu.

Chapisha