Sura ya 14 Abinadi na Mfalme Nuhu Zenifu alikuwa mfalme mwenye haki wa kundi la Wanefi. Alipozeeka, mtoto wake Nuhu alikuwa mfalme. Mosia 11:1 Nuhu hakuwa mfalme mzuri kama baba yake. Alikuwa mwovu na hangetii amri za Mungu. Mosia 11:2 Aliwalazimisha watu wake kumpa sehemu ya kipato chao, mifugo, dhahabu na fedha. Mosia 11:3 Mfalme Nuhu alifanya hivi kwa kuwa alikuwa mvivu. Aliwafanya Wanefi kumpa kila kitu alichohitaji ili kuishi. Mosia 11:4 Aliwaweka makuhani waovu badala ya wale wema ambao baba yake aliwaweka. Makuhani hawa waovu waliwafundisha watu kutenda dhambi. Mosia 11:5–7 Mfalme Nuhu alikuwa na majengo mengi mazuri, ikijumuisha kasri kubwa lenye kiti cha enzi. Majengo yalikuwa yamepambwa kwa dhahabu, fedha na mbao za thamani sana. Mosia 11:8–11 Nuhu aliupenda utajiri aliochukua kutoka kwa watu wake. Yeye pamoja na makuhani wake walitumia muda wao kunywa mvinyo na kuwa waovu. Mosia 11:14–15 Mungu alimtuma nabii aliyeitwa Abinadi kwa watu wa Nuhu. Abinadi aliwaonya kwamba kama hawangetubu, wangekuwa watumwa wa walamani. Mosia 11:20–22 Wakati mfalme Nuhu aliposikia kile Abinadi alichosema, alikasirika. Aliwatuma watu kumpleka Abinadi kwenye kasri ili kwamba amuue. Mosia 11:27–28 Abinadi alipelekwa kwa mfalme. Mfalme Nuhu na makuhani wake walimuuliza maswali mengi. Walijaribu kumtega katika kusema kitu kisicho sahihi. Mosia 12:18–19 Abinadi hakuogopa kujibu maswali yao. alijua kwamba Mungu angemsaidia. Makuhani walishangazwa na majibu ya Abinadi. Mosia 12:19 Mfalme Nuhu alikasirika na kuamuru makuhani wake kumuua Abinadi. Abinadi aliwaambia kama wangemgusa, Mungu angewaua. Mosia 13:1–3 Roho Mtakatifu alimlinda Abinadi ili kwamba angemaliza kusema Bwana alichomtaka kusema. Uso wa Abinadi uling’aa. Makuhani waliogopa kumgusa. Mosia 13:3, 5 Akinena kwa nguvu kutoka kwa Mungu, Abinadi aliwaambia watu kuhusu uovu wao. Aliwasomea amri za Mungu. Mosia 13:6–7, 11–24 Aliwaambia Yesu Kristo angezaliwa duniani. Yesu angefanya iwezekane kwa watu kutubu, kufufuka, na kuishi na Mungu. Mosia 13:33–35; 15:21 –23 Abinadi aliwaambia watu watubu na kuamini katika Yesu Kristo au sivyo wasingeokolewa. Mosia 16:13 Mfalme Nuhu na wengine wote isipokuwa mmoja wa makuhani wake walikataa kumwamini Abinadi. Nuhu aliwaambia makuhani kumuua Abinadi. Walimfunga na kumtupa gerezani. Mosia 17:1, 5 Kuhani mmoja aliyemwamini Abinadi aliitwa Alma. Alimuomba mfalme Nuhu kumruhusu Abinadi aende. Mosia 17:2 Mfalme alimkasirikia Alma na akamfukuza. Kisha akatuma watumishi wake kumuua. Alma alikimbia na kujificha, na watumishi wa mfalme hawakumpata. Mosia 17:3–4 Baada ya kukaa kwa siku tatu gerezani, Abinadi aliletwa tena mbele ya Mfalme Nuhu. Mfalme alimwambia Abinadi kukanusha alichokisema dhidi yake na watu wake. Mosia 17:6, 8 Mfalme Nuhu alimwambia Abinadi kwamba kama hatakanusha yote aliyoyasema, atauwawa. Mosia 17:8 Abinadi alijua alikuwa amezungumza ukweli. Alikuwa tayari kufa kuliko kukanusha kile Mungu alichomtuma kusema. Mosia 17:9–10 Mfalme Nuhu aliamrisha makuhani wake kumuua Abinadi. Walimfunga, wakamchapa kwa mjeledi, na kumchoma moto mpaka kufa. Kabla hajafa, Abinadi alisema Mfalme Nuhu pia angekufa kwa kuchomwa moto. Mosia 17:13–15 Baadhi ya Wanefi walimpinga Mfalme Nuhu na kujaribu kumuua. Jeshi la Walamani pia lilikuja kupigana na mfalme na watu wake. Mosia 19:2–7 Mfalme na wale waliomfuata walikimbia kutoka kwa Walamani, lakini Walamani waliwashika na kuanza kuwaua. Mfalme aliwaambia wanaume waache famila zao na waendelee kukimbia. Mosia 19:9–11 Wengi wa wanaume hawakufanya hivyo. Walitekwa na Walamani. Mosia 7:12,15 Wengi wa wanaume ambao walikimbia pamoja na Mfalme Nuhu walihuzunika. Walitaka kurudi na kuwasaidia wake zao na watoto na watu wao. Mosia 19:19 Mfalme Nuhu hakutaka wanaume warudi kwa familia zao. Aliwaamrisha kubaki pamoja naye. Mosia 19:20 Wanaume walimkasirikia Mfalme Nuhu. Walimchoma mpaka kufa, kama Abinadi alivyotoa unabii. Kisha wakarudi kwa familia zao. Mosia 19:20, 24