Scripture Stories
Sura ya 54: Ahadi ya Kitabu cha Mormoni


Sura ya 54

Ahadi ya Kitabu cha Mormoni

Picha
Moroni akiandika kwenye bamba

Kabla ya Moroni kuzika bamba zile kwa mara ya mwisho, aliandika ahadi kwa Walamani na kwa mtu yeyote ambaye angesoma kumbukumbu hiyo.

Picha
mvulana akisoma maandiko

Aliwaambia watu wasome kumbukumbu hiyo, watafakari sana juu yake, na kisha wamuulize Baba wa Mbinguni kama ni ya kweli.

Picha
mvulana akisali

Moroni aliahidi ya kwamba kama watu wangeuliza kwa moyo wa kweli, na imani katika Kristo, Roho Mtakatifu angewasaidia kujua kwamba kumbukumbu hii ni ya kweli.

Picha
Moroni akiandika kwenye bamba

Moroni aliandika kwamba kama watu watatubu, wamfuate Yesu Kristo, na kumpenda Baba wa Mbinguni, wanaweza kuwa wakamilifu.

Picha
Moroni akizificha bamba za dhahabu

Wakati Moroni alipomaliza kuandika kwenye bamba za dhahabu, alizificha ndani a sanduku la mawe katika Mlima Kumora na kulifunika sanduku lile kwa jiwe kubwa. Kazi yake katika maisha ya kufa ilikuwa imekamilika.

Chapisha